Chereads / penzi la bahati / Chapter 13 - chapter 12

Chapter 13 - chapter 12

Tulya akizunguka chumba Chao kidogo hawezi kukaa kama kitanda kina misumari,baada ya kufanya varangati kwenye kikao."mjomba kaenda wapi mbona haniiti" anamuuliza sinde aliyekaa akimwangalia kwa kutokuamini alichikifanya,sinde hajibu swali lake naye anamuuliza " si ulisema hutafanya fujo wewe? si ulisema utakubali tu kuolewa hata na Mzee Sasa imekuwaje umekataa kuolewa na manumbu kijana kabisa" tulya anasimama na kumwangalia " yaani ni mara mia ningeolewa na Mzee kuliko yule manumbu,nilisema nitavumulia tu lakini niliposikia jina lake" anatulia kidogo "damu ikanuka puani, hapana,siwezi hata Sasa hivi siwezi kabisa kuolewa na manumbu simpendi hata kidogo we mwenyewe unajua"

"Mimi ninavyoona ilikuwa afadhari ya manumbu kuliko Mzee" tulya anashika kiuno kwa mikono yake yote miwili na Kisha anautoa Mmoja " unajua ni jinsi gani Mimi na manumbu tuliko anzia,ni mguu tofauti kabisaa na hatuwezi rekebisha hilo,siwezi kuishi nae atanipiga aniue kwa ujeuri wangu kwani sitamsikiliza kwa amri zake za kijinga,afadhali niolewe na Mzee najua Hana miaka mingi atakufa nibaki mjane peke yangu"

Sinde Anacheka " kweli unamchukia manumbu" anatulia kidogo na kumwangalia " kilichokufanya useme unampenda nzangamba nini wakati umewahi kumuona mara Moja tu" tulya anaenda kukaa kitandani akikumbuka vurugu la mwisho alilotoka nalo " hata sijui,nilikuwa sina mpango,nilipoulizwa kwa nini nakataa kuolewa,nikasema Kuna mtu nampenda wakaniuliza nani,jina sina, nikasema nzagamba" anaongea kwa sauti ya chini mikono yake ameiweka juu ya mapaja yake kama anataka kunyanyuka lakini anauchezesha tu mwili kwa miguu yake ambayo haijafika chini ikining'inia

" Sasa ndio umtaje nzagamba,si ungesema hata kijana mwingine tu" sinde anamuuliza na kumfanya aache kujitikisa " ningemtaja nani? hapa Kijijini tangu nifike watu ninaowasikia ni nzagamba, manumbu,na Tinde" anaongea akionyesha vidole vyake " Sasa hapo ningemtaja nani hembu niambie mwenyewe mhh!" sinde anakaa kimya "unadhani mjomba atanifanya nini?amekasirika sana" " hata sijui tangu wazee waondoke na yeye akaondoka hata sijui ameenda wapi,tusubiri mpaka arudi" wote tulya na sinde wanavuta pumzi ndefu wakiwaza nini kitatokea akirudi Mzee Shana.

Giza limeanza kuingia na Mzee Shana hajarudi,wote sinde na tulya wanatoka na kwenda kuandaa chakula Cha jioni,runde kwa upande wake hakutia neno alikuwa kimya tu muda wote akisaga Karanga kwenye jiwe. tulya anasogea karibu yake na kuongea kwa sauti ya chini " samahani mama,sikutaka kuwaaaibisha" runde anaendelea kusaga Karanga mikono yake juu ya jiwe dogo " hayo ni maamuzi yako mwanangu kama hujaridhika nae usijilazimishe kwani ndoa sio kitu Cha kuchezea,hata hivyo Mimi mwenyewe sikuridhika uolewe na manumbu" anaongea pasipo kumwangalia tulya usoni.

tulya kusikia hivyo moyo unapata faraja kidogo akijua Kuna mtu mwingine Yuko upande wake "mjomba atasemaje mama" anauliza na runde anaacha kusaga na kumwangalia "unaniuliza kwani Mimi mjombaako,kukwambia sikuridhika na manumbu sio kama nimefurahishwa na ulichokifanya Mbele ya wazee na unajua kabisa mjombaako anavyoheshimika hata sijui atafanyaje,haya kapike huko akirudi akute hata chakula sina uhakika hata kama atakula" tulya anaamka akijivuta na kurudi jikoni anamkuta sinde akisonga ugali anakaa pembeni na macho yake kuelekea kwenye moto "unadhani mjomba atanifanyeje" sinde anacheka kidogo " mhh!sijui mpaka Sasa hajarudi atakuwa amekasirika sana,lakini usiwaze sana hawezi kukufanya kitu kibaya,kawaite kina kaka tuje kula" tulya anaamka na kuelekea njee.

Baada ya mda anarudi akifuatiwa na kilinge na zinge,wanakuta tayari sinde na mama yake runde wakiwa wameweka chakula nje kwenye mkeka mbalamwezi ikiwaangazia,tulya na kaka zake Wananawa mikono na kukaa tulya akikaa chini na kunyoosha miguu yake,kilinge na zinge wakikaa kwenye vigoda vya miti wote wanakizunguka chakula na kuanza kula kimya kikiwa kimetawala.

Zinge anauvunja ukimya huo "tulya ni kweli unampenda nzangamba" moyo wa tulya unazima kwa mda kutokana na mshtuko wa kusikia swali hilo,na wote wanamwangalia Kila mtu akiwa na hamu ya kusikia jibu lake isipokuwa sinde "Mimi mwenyewe nataka kujua umemjulia wapi nzagamba" kilinge nae anachangia "hampendi alilopoka tu kujinasua kuolewa na manumbu" anadakia sinde na kumfanya zinge acheke,tulya anaendelea kula huku moyoni akiomba waiache maada hiyo angalau ugali upite kinywani " baba hajarudi mpaka Sasa hivi atakuwa kakasirika kweli" anaongea kilinge akinywa maziwa yaliokuwa kwenye kipeo chake na kugeuka kunawa mikono yake "umeshiba" anauliza rude " ndio,nimechoka nataka nikalale mapema" anasimama.

"umefanya vizuri kumkataa manumbu lakini hatujui baba atakuja na maamuzi gani tusubiri mpaka arudi" anaongezea macho yake ykiangalia juu utadhani anaongea na mwezi" harudi Leo huyo atakuwa ameenda kwa mama mdogo atalala huko" anaeleza zinge akijua baba yake atakuwa kwa mke wake wa pili ambaye ni mama Yao mdogo " usijali,itabidi tu atafute mchumba mwingine" sinde anamalizia na wote wanakubaliana nae,kilinge anawataikia usiku mwema na kuondoka akiwaacha wakila.Wanamaliza kula zinge anaaga na kuondoka,tulya na sinde nao wanamuaga mama Yao na kuelekea kulala.

Asubuhi imewahi kufika kwa tulya na kuamka kufanya majukumu ya hapa na pale lakini bado hajamuona Mzee Shana na Sasa inakaribia mchana na Mzee Shana bado hajarudi,tulya anaona ni afadhali mjomba ake akae huko kwa mda mpaka hasira zake zipungue lakini hakuwa na bahati kwani Mzee Shana anafika muda huo na kumfanya tulya atoke jasho jembamba " shikamoo mjomba" anamsalimia kwa adabu akikunja mguu wake wa kushoto kido na kumfanya ainame lakini Safari hii anakunja zaidi mguu wake na kufanya goti lake kugusa chini kumpunguzia Mzee Shana hasira "kaka zako wako wapi" anauliza Mzee Shana asijibu salamu yake kumfanya tulya ajue bado amekasirika lazima akasirike zaidi sio kwa utovu wa nidhamu aliouonyesha Jana licha ya Mzee Shana kumwonyesha ishara za kumwambia anyamaze yeye hakusikia wala kuelewa na kuendelea kuvuruga

" watakuwa ndani kwao mjomba" anamjibu akiangalia chini " kawaite umwite na huyo mjinga mwenzio aje hapa" anaagiza na kuingia ndani kabla hajafika mlangoni anapokelewa na mkewe runde aliyekuwa ndani anatoka baada ya kusikia sauti yake.Tulya bila kusita anatoka mbio kuelekea nyumbani kwa kaka zake asitake kuchelewa asije akamuudhi zaidi mjombaake,anawaita kaka zake na kwenda nyumba wanayolala anaingia na kumkuta sinde akiwa amelala " sinde amka" anamwamsha huku akidaka pumzi zake zinazoenda pasipo mpangilio kutoka na mbio alizokimbia " Kuna nini kazi zote nimemalaza" analalama sinde akijinyoosha kwenye kitanda chake Cha kamba kilichotandikwa ngozi juu "mjomba kaja anatuita wote amaka"

sinde anakurupuka na kuweka miguu yake chini akitafuta viatu vyake,wakati huo tulya Yuko mlangoni akiondoka " nisubiri" anaongea akitupia viatu miguuni na kumfuata nyuma " sitaki kuchelewa nikamuudhi zaidi mjomba" tulya anatembea mbiombio sinde nae akimfuata kwa mwendo ule ule.wanafika na kukuta watu wote wakiwa wamekaa tayari,Wanaingia na kukaa Kila mtu akiwa na hamu ya kutaka kujua Mzee Shana anataka kusema nini,wote wakiwa wanajua kuwa kikao kinahusu tukio la jana ila wasiwasi ulikuwa ni Mzee Shana kaja na uamuzi gani.

Baada ya kimya kifupi Mzee Shana anasafisha Koo lake akivuta usikivu wa wote waliopo pale, zaidi tulya ambaye tumbo linamkata kwa wasiwasi " zinge itabidi kesho ufunge safari kwa shangazi yako" wote wanamwangalia kwa kutokumuelewa, tulya akijua wazi kuwa anarudishwa nyumbani 'nikirudi baba ataniua,nifanyeje' anawaza akijua safari hii kavuruga kweli hakuna kurudi nyuma lakini hata kama angejikuta katika Hali kama ile ya Jana Leo ana uhakika angefanya maamuzi Yale yale bila kujali matokea yake." kwa nini baba" anauliza zinge na kumrudisha tulya kundini " nenda ukawataarifu taarifa za harudi ya Binti Yao ikiwezekana uje na shangazi yako kwa ajili ya maandalizi" anarusha bomu Mzee Shana na yeye anakaa pembeni akiangalia likiteketeza " harusi?" wote wanauliza kana kwamba hawajasikia " mjomba Mimi sitaki kuolewa na manumbu" tulya asifunge mdomo Wake anatetea bahati yake tena kwa mara ya mwisho akiongea kwa sauti ya chini machozi yakimzidi uwezo machoni " aliyesema unaolewa na manumbu nani?" anaongea Mzee Shana na kufanya wamwangalie kwa mshangao

" Sasa kama haolewi na manumbu anaolewa na nani" runde anamuuliza mume wake kwa sauti ya kutetemeka asitake kumuudhi zaidi, tulya anaitikia kwa kichwa akimshukuru runde kumsaidia kuuliza swali " kwani hamkumsikia Jana alivyosema au mnataka nirudie kama nataka kurusha kombeo" anaongea akianza kukereka Mzee Shana " baba anaolewa na nzagamba?" anaongea kilinge sentensi yake isijulikane kama ni swali au jibu kumsaidia baba yake kutoa jibu kwa mama yeke " si kasema anampenda na Mimi sitaki kumnyima furaha mpwa wangu nimempa anachotaka"

wote wanabaki midomo wazi kwani hawakutarajia kama Mzee Shana angekuja na hitimisho hilo na wanamwangalia tulya.

Mwili wa tulya unakufa ganzi Kila kiungo kinashindwa kufanya kazi yake kwa muda asijue Cha kusema kwani mdomo Wake ulikuwa haunyanyuki hata kidogo.Hakuna anayetaka kubishana na Mzee Shana wakijua itakuwa ni hatari kwani hicho ndo alichokisema tulya hata kama hampendi kwa Sasa Hana namna nyingine kukubaliana na Hali halisi "nimetoka kwa bibi sumbo kabla ya Kuja hapa,na kakubali posa kesho anakuja na wazee kumwangalia na maandalizi ya harusi kufuatia,kwa hiyo zinge uamke mapema upeleke taarifa kwa shangazi yako na wewe mama kilinge" anamgeukia mke wake "eheee" anaitikia runde ambaye akili yake haukuwa pale kwa muda " Anza maandalizi ya kumwandaa mwali na akae ndani huyu mpaka siku ya harusi kama ilivyo Mila mtaongea mengi zaidi na bibi sumbo akija kesho" anamaliza Mzee Shana na kusimama kuelekea chumbani "ndio mume wangu" runde anamsindikiza na jibu lake lilochelewa kufika.

wote wanabaki wakimwangalia tulya " uko sawa" sinde naye anapata nguvu za kuongea kwani muda wote alikuwa amebana pumzi asije akaingizwa kwenye mkumbo " unaweza kunisaidia kusimama" anongea tulya mwili wote ukimtetemeka " ndio" ananyanyuka na kumsaidia, tulya anasimama" nipeleke chumbani nataka kulala kichwa kinauma"