Ghafla simu yangu ikaanza kuita prirrr priirrr ilikua namba ngeni, nikapokea, halooo
SIMU: Kwa majina naitwa "Rose Mutesi" napiga simu kutoka taasisi "X" nitakua naongea na INSIDER MAN?, nikamwambia yes ni mimi karibu. Dada akanambia hongera kwa kufaulu interview umechaguliwa kupata mafunzo kazi (Internship) kwenye taasisi yetu, jiandae mwanzoni October tutakupigia simu kwaajili ya kuanza kazi. Baada ya kuongea nae akakata simu .
Kiukweli sikuamini kama nikweli maana niliona kama ndoto hivi, nikasema hawa wanaweza kuwa matapeli, inshort sikuwa interested na ile simu. Sikumwambia mtu yoyote juu ya hili jambo hata mama sikumwambia maana niliogopa wasije wakawa matapeli. Hapo nilikua tayari nina miezi 2 niko home, wakati nimefika mzee wangu alikaa siku 3 akarudi Zambia.
Mzee wangu ni engineer kule kuna kampuni anafanyia kazi na pia mzee wangu kurudi home ni nadra sana anaweza kukaa hata miezi 3 na zaidi bila kurudi nyumbani. Nilikua naongea na mama mambo mengi sana hasa alikua anataka kujua pale kwa Uncle kama ninaishi vizuri. Ni kwamba mama yangu anamjua vizuri sana Aunt ni mtu wa namna gani, sikutaka kumwambia mama lolote kuhusu pale kwa Uncle niliamua kuyaweka moyoni. Japo mama alihisi kuna jambo halipo sawa,lakini alinisistiza sana kuwa na adabu na heshima. "Kila siku usiku tulikua tunapiga maombi na mama" mama yangu ni mtu wa dini sana.
Mwezi wa 9 mwishoni 2019, nikaamua kurudi Dar ili kuwa karibu endapo ningepigiwa simu na ile taasisi. Nikamwaga mama, akanifungia mchele wa kutosha, unga, mafuta ya kupikia gallon, maharage akanambia mpelekee Uncle. Niliamua kurudi palepale kwa Uncle lakini this time nilikua naplan zangu kichwani tayari. Baada ya kurudi Dar haikupita week nikapigiwa simu nikareport kazini nianze training.
Uncle nilimwambia kwamba kuna sehem nimepata part time, kazi ya muda nitakua natoka asubuhi, lengo langu nipate mkataba niwe na uhakika wa kumwambia. Lakini alisisitiza niwe nahakikisha mbwa wake wanakula ontime pamoja na kumwagilia maua yake. Kutoka na kurudi jion Aunt hakupenda siku nimerudi jion akanambia wewe sikuhizi umepata kazi na husemi?… nikamwambia hapana ningekua nimepata kazi mbona ningeliwaambia ila Uncle nilimwambia nimepata kazi ya muda. Dizaini hakupenda akanambia kwahiyo ukamwambia Uncle wako tu?, nikamwambia Aunt kwan kuna shida?. Akanambia sikuhizi hata kazi hufanyi… daah! . Nikamwambia huoni napikia mbwa chakula kila nikirudi jion? bado namwagilia miti namaua au unataka nifanye kazi gani??.
Aunt yangu alikua mtu wa gubu sana alikua na roho mbaya sana kama mtu wa hasira unaweza mtukana kabisa. Alikua ananichongea maneno sana kwa Uncle mpaka nikaona dizaini mzee baba kama anakua mbali na mimi.Kuna siku niliondoka na gari ya uncle kwenda kumchukua dogo shule, Uncle mara nyingi alikua anapenda kutumia gari ya ofisi ile yake inakaa home tu.
Sasa Uncle alivyorudi Aunt akamjaza maneno kuwa niliendesha gari yake eti siku nzima na nimeichibua gari. Uncle aliongea sana ile siku usiku "Sitaki uendeshe gari yangu kwanza hujui kuendesha gari, umenichubulia gari yangu. Gari ikiharibika unahela ya kulipa?? ". Ukweli ni kwamba ile michubuko ilikua vilevile, yale maeneo yalinichoma sana nikahapa kutokuja gusa ile gari hata aombe nimpelekee wapi.
Baada ya kumaliza training hatimaye nikapangiwa kituo cha kazi na nikaambiwa kesho niripoti pale ofisini. Sikuamini nilovyopewa ule mkataba kweli kesho yake nikaanza kazi nikapangiwa moja ya Idara kwenye ile ofisi. Hii ni moja ya taasisi kubwa sana hapa nchini na inategemewa sana sana.
Nilianza hii kazi bila malipo then nilikua niko vibaya sana kiuchumi ndugu zangu, mama Junior ndo alikua ananipiga tafu za nauli sometimes. Ilibidi nimwambie Aunt kwamba nimepata kazi kwenye taasisi X that day Uncle alikua safari nikaplan ntamwambia Uncle officially akirudi kwamba nimepata kazi face to face, Ukweli hizi taarifa Aunt hakuzifurahia ni kama nilimpiga na kitu kizito sana akaanza kuulizia mambo ya salary sikutaka kumwambia lolote.
Uncle akarudi toka safari nikaongea naye kuhusu kupata kazi na taasisi "X" japo hakuonesha ile furaha halisi niliona kuna unafiki hapa hajapenda. Akaniuliza nani kakutafutia nikamwambia nilifanya interview nikapigiwa simu, akauliza mambo ya mshahara nikamwambia hili suala bado ila ni kama nafanya kujitolea, kama kuna malipo nitakuambia. Huwezi amini Uncle hata hakusema neno "hongera", nikaanza pata picha ninaishi na ndugu wa aina gani, hata mama alinambia niwe makini sana.
Pale ofisini baada ya mwezi nilikua nimeshazoeana na maofisa wa pale hasa idara yangu kama incharge/supervisor wetu alikua na roho nzuri sana. Alitokea kunikubali sana hizi ten ten nilikua nakula sana kila siku, yaani nilikua nafanya kazi kwa bidii sana na kujituma nikaweka urafiki na watu wa idara.
Pale kwenye kile kitengo chetu interns tulikua wawili mimi na dada mmoja hivi. Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda nikawa nimezoeana na maofisa wa idara zingine wakawa wananipa kazi zao nafanya wananipa hela sikuwa nakataa kazi. Ikafika muda nikajikuta kwasiku sikosi 20,000 kuna kipindi napata mpaka 50,000/= au zaidi, hizi hela nikawa naziweka maana nilikua na mipango yangu kichwani ya kwenda kupanga.
Hii Taasisi niliyokuwa nafanyia kazi ina deal sana na wafanyabiashara hivyo nikaanza kupata connection na wafanyabiashara mbalimbali hasa pale Kariakoo.
Baada ya miezi 2 taasisi ikasema itaanza kutulipa 450,000 kwa mwezi zitusaidie bhasi kwangu ikawa sherehe. Nikaanza kununua vitu taratibu naacha madukani kwaajili ya kuanzia maisha. Nikawa nawaza njia ya kutokea pale kwa Uncle maana wangeanza maneno kapata kazi ameondoka sikutaka hizi kelele. Nikawaza hapa nitawaambia naenda safari ya kikazi Dodoma ndo itakua gia yangu ya kusepa pale.
Baada ya hapo sikuchelewa nilikua na iphone 7 plus nikaiuza 740,000 nikawa kidogo napesa ya kuanzia maisha. Nikamtafuta dalali tukapata chumba sebule na jiko kodi ilikua 180,000 kwa mwezi, nikalipa kodi ya miezi 4 kwanza. Eneo nililopata ilikua ni salasala (Mabanda mengi) pale Mbuyuni mataa ya kwenda tegeta na kunduchi, sasa kwa mbele kama unakwenda Tegeta kuna kibarabara kinakata kushoto kwenda salasala, kule ndo nilikoanzia maisha.
Nikaweka godoro langu chini, nikaweka jiko langu la gas, nikanunua gas mtungi mkubwa, sufuria na baadhi ya vyombo vya kuanzia maisha bila kusahau subwoofer "Sea piano" , raha ya geto mziki uwe unasikika.
Baada ya hapo nikaanza kuamisha vitu vyangu bila kushtukiwa mpango wangu. Baada ya hapo nikawaaga nitakwenda kikazi Dodoma sijui nitarudi lini wakaniambia safari njema, maisha ya geto niliyaanza March 2020.
Nimeingia pale sasa akili ya maisha ikaanza kuja kichwani, kwanza nimelala pale kuna baridi hatari sina hata shuka la kujifunika, madirisha hayana mapazia. Week ileile niliyohamia kwangu nikapambana nikanunua mapazia mazuri nikayaweka. Bad news haikupita hata week nikaibiwa yale mapazia na laptop .
Pale palikua na wapangaji watatu na wote tulikua tunatoka afu fense ilikua fupi mtu rahis kujua kama hakuna mtu, na pia geti lilikua tunarudishia si unajua tena maisha ya kupanga geti huwa halifungwi. Uzembe ulikua wangu maana sikufunga madirisha ilikua rahsi kuibiwa jama alichomoa mapazia yote mpaka seblen. Nilihisi aliyeniibia ni mzoa taka wala sio mtu mwingine maana ndo alikua na mazoea ya kuja pale home.
Mungu akaendelea kufungua milango, kutokana na kuwa na changamoto nikipika chakula kikibaki kinachacha nikaona kuna umuhimu wa kununua fridge. Nikafanya research yangu pale Kariakoo nikaona bora ninunue fridge la size ya kati bei ilikua ni 720,000 kwa kipindi kile.
Nikapambana sana pamoja na kukopa nikaweza kununua fridge, mama Junior naye hakua mbali akaniletea Micro wave ya kupashia chakula na mazaga mengine kama mashuka nknk. Ndani ya muda mfupi nikawa nimekamilika na kila kitu ndani kiasi kwamba ukiingiza pisi ndani lazima ipagawe. Baada ya hayo niakaanza kusave hela kila senti nayopata nikawa nasave kupitia vicoba na kucheza michezo.
November 2020, mama junior akaja kwangu akanambia ana mimba yangu hivyo kwao amekimbia hawezi kurudi anamwogopa baba yake. Hapo alikua anasoma chuo na mzee wake katoka kulipa ada afu sasa mzee wake ni mkorofi hatari ndomana akakimbilia kwangu hakutaka kutoa ile mimba.
Zile habari hazikunishtua niliona mtoto ni jambo la kheri then hata yeye nampenda nikamwambia kama mtoto ni wangu bhasi utakaa hapa huko kwenu tutaweka mambo sawa, si unajua wazee wa kichaga.
Nikampigia simu mama yake kumwambia bint yake yupo kwangu asihangaike kumtafuta mimi naandaa utaratibu nitakuja, mama yake alikua anajua natoka na bint yake hakua nashida na mimi. Akanambia kama yuko kwako mimi sina shida najua yuko sehem salama ila sasa baba yake ndo shida.
Tulikwenda hospital kuchek mimba ilikua na week 6, ikabd nichukue hatua zingine za haraka ili kukamilisha hili jambo, hatimaye tukalipa mahari.
Baada ya kuanza kukaa na mama Junior hapo ni mjamzito mambo yangu yakazidi kunyooka sana, nikawa mtu wa bahati sana. Kuna mwanamke ukiwa naye mambo yananyooka yenyewe. Nikaanza kutengeneza connections na wafanyabiashara wakubwa, stakeholders na watu mbalimbali maana sikuwa naona future ya kuajiriwa na hii taasisi.
Nikaanza kujiongeza mlemle Kariakoo na kufanya deals zingine nyingi, nikafungua biashara "workshop" ya kupaka rangi magari, services, lubricants, polishing nknk pale gerezani. Kwa kufupisha hii story baada ya kumaliza mkataba tukastopishwa kwenda kazini na mimi sikutaka kuhangaika na kuomba na kutafuta kazi. Hapo ilikua ni September 2021.
Sikushtuka sana, mimi binafsi nilikua nishajipanga tayari na nilishaona dalili mapema, savings binafsi nilizokuwa nazo za haraka cash in hand ni 24 million. Nikaagiza Toyota IST kutoka Japan iwe inanisaidia mishe zangu za hapa napale. Baada ya kununua gari, kukamilisha kila kitu nilitumia 14 million, nikalipa deni la kiwanja full 5,600,000/=nikamwekea wife 3 million kwa account maana mwakani 2022 alikua inabidi arudi chuo kuendelea na masomo alikua kashajifungua tayari. Nakumbuka sikubaki na kitu katika ile saving lakini nilikua na shares zangu kwa watu hivyo hata bila kazi ningesurvive.
Maendeleo ya Biashara yalikua mazuri sana nilikua na wateja wengi sana na pesa nilikua naiona kama faida. Ile September mwisho wa mwezi mwenye eneo/Landlord akanipigia simu.
LANDLORD: Kijana wangu hujambo? sasa nina habari mbaya nataka kukupa maana ipo chini ya uwezo wangu. Kutokana na ujenzi unaoendelea na upanuzi wa barabara nimepewa order ya kwamba nyumba zetu zitaweza bomolewa muda wowote. Na wewe kodi yako inaisha mwezi ujao, itabidi utafute eneo lingine mambo yatakapo kamilika nitakutaarifu kijana wangu.
Ukweli taarifa za Mzee zilinipa stress sana maana biashara ilikua imechanganya sana na kwa ile location ilikua nzuri sana. Niwaambie biashara ya workshops inalipa sana faida inaonekana sana. Mchawi ni location tu maana pale nilikua nakamata magari yanayotoka bandarini nknk.
Ofisi yangu ilikua Gerezani karibu na Round about ya kwenda Kurasini. Kama unatokea central before hujafika kwenye ile Round about kuna yard ya magari bhs mitaa ileile. Baada ya kuongea na mzee nikawa sijui niende wapi maana nilikua dilemma, pia watu wakanishauri ujenzi wa barabara unaondelea biashara itakua ngumu sana maeneo yale hivyo nisubiri niangalie upepo. Ikabidi nistop kwenye hii biashara kwanza,nikaplan nitarudi barabara ikikamilika. Ilikua kama mkosi naacha kazi na biashara nafunga niliona kama mtu ananichezea hivi.
Nikafunga biashara katikati ya October kodi ndo iliisha tarehe hizo, baada ya hapo nikawa sina hela maana hakuna nilichokua naingiza. Ile ile october kuna mhindi alikua jamaa yangu sana niliweka kiasi cha pesa kwenye biashara yake ni muda. Jamaa alinicheki akanambia anakwenda India na pale watasimamia ndugu zake itaweza sumbua kupata gawio zangu hivyo akanipa pesa magawiwo yote 6,000,000. Nikakusanya na madeni yangu na pesa zingine nikapata 3,400,000 jumla nikawa na 9,400,000/=.
Ikabidi nikae na wife chini tupange mipango maana alikua anajua kinachoendelea. Nikalipa kodi ya nyumba 1,800,000/= kwa miezi sita. Nikampa wife 2,500,000/= kwaajili ya matumizi ya mtoto, mshahara wa dada, bill za umeme na maji na mahitaji ya nyumbani yote (Miezi 6). Nikamlipia mtoto bima pamoja na mama yake kama 245,000/=.
Ilibaki kama 4,800,000 tukaplan hii amount tufungue biashara ya vinywaji. Lakini kuna dogo langu anayenifuatia yeye alikataa shule alisema anapoteza pesa za wazazi na muda. Toka muda alikua ameniomba nimkopeshe million 3, "alipataga hasara walimtapeli" dogo anaduka la vifaa vya simu na Huduma za kifedha. Dogo pia alinisave sana kipindi kile nakosa nauli za kwenda kazini, so nikampa dogo million 2 kama kaka yake. Nikamlipia dogo ada "yule ambaye mama alisema anataka sayansi ila math haipandi" nililipa million 1. Hapo unaona jinsi ambavyo pesa haikai kabsa.
Nilibakiwa na 1,500,000/= hivi nikasema hizo nilizotoa nitajazia. Ukitaka kuona mambo yanabadilika acha kazi ndo utaona kila rangi. Bhasi nikaanza kuwaza namna ya kutafuta pesa nikisema nisubiri pesa iishe nitakuja aibika huko mbeleni. Nikafikiri kuingia kwenye uber maana gari nilikuwa nayo tena yangu, kumpa mtu hapana bora nikomae mwenyewe tu. Kuna jamaa yangu wa uber alikua mshikaji sana nikamcheki…
DULLAH: oya tajiri vipi hatutafutani sikuhizi umenitenga hunipi kazi kama zamani hali ni mbaya.
MIMI: Tajiri sijakutenga sema pale nimetoka ndomana unaona kimya mwenyewe sina maisha ndomana nimekucheki unipe ramani.
DULLAH: Sasa tajiri mimi nakupa mchongo gani hapa nakomaa na uber tu hapa, siku za kati ya wiki tunafanya kuokoteza, cha muhimu mkono uende kinywani.
MIMI: Tajiri nahitaji tuonane nina jambo langu muhimu sana unipe code nianzie wapi ili kufanikisha.
DULLAH: Jambo gani tajiri unanitisha, kesho nitakua home siku nzima, leo nitakudanganya boss wangu. Wewe kesho njoo muda wowote tutayajenga.
MIMI: haina noma kesho asubuhi nitakucheki unipe code.
DULLAH: Imeisha hio tajiri
Asubuhi nikamcheki Dullah ilikua kama saa 2 asubuhi hivi akapokea akanielekeza anakaa Sinza madukani unakunja pale kwa vunja bei. Bila kupoteza muda nikaenda chap nikafanikiwa kufika kwa jamaa, tukaanza story…
DULLAH: Tajiri karibu sana naona upo na chombo mpya kabsa hii hata week haina. Hii chombo umechukua yard au umeagiza?
MIMI: , Tajir huoni kabisa hadi alama za bandarini hizo chuma imetoka Japani. Sikia ndugu yangu mchongo wenyewe naotaka tuongee ndo huo unaoushangaa.
DULLAH: Sijaelewa Tajiri unauza hii IST?? au
MIMI: Nataka kusajili Uber tajiri unanisaidiaje? Nataka maelekezo kutoka kwako wewe una experince ya muda mrefu.
DULLAH: Unataka kuendesha wewe au nikutafutie dereva?
MIMI: camon mimi bro!
DULLAH: Kama wewe sikushauri hii gari ubadilishe vibao tumia hivyohivyo vya njano, akaifungua ndani akaona gari nimetia seat cover, full unyunyu, Android Tv nch 10 imekaa pale, chini carpet. Mzee hii gari utapiga sana hela niamini mimi kama hawa mademu watakutafuta sana, utapata root privates nyingi, kama nilivyokwambia usiweke vibao vyeupe.
MIMI: kwanini nisiweke vibao vyeupe?
DULLAH: Vibao vyeupe miyeyusho ndugu yangu traffic mikono mingi, bado TRA yaani tunapata shida wahuni sikuhizi wanatumia vya njano.
MIMI: Basi poa nimekuelewa sasa najisajilije?
DULLAH: Kuna jamaa namjua ila sijawai kumwona kwa sura ni kama "Ghost" anakusaidia chap wewe andaa 100k. Kama unayo hata leo anaanza kazi baada ya siku 3 kila kitu kinakua sawa. Hapa anza na Bolt hii haichelewi huku unasubiri uber hii kidogo utasubiri.
MIMI: ongea na jamaa then nipe namba yake mwambie huyu ni ndugu yangu wa damu. Afu unaongeaje na mtu usiyemjua?? Kama tapeli?
DULLAH: , Tajiri nishafungua account nyingi sana na yeye hana noma usiwe na wasiwasi.
Dullah akaongea na jamaa walitumia muda kidogo baada ya hapo akanirudia akanambia nimeongea naye Freshy utampa 90,000 atafanya hiyo kazi. Nikamshukuru nikampa 10,000 ya Ahsante.
Nikampigia simu Ghost tukaongea maana alikua anajua tayari kuhusu mimi. Akanambia nimtumie baadhi ya documents kama kadi ya gari, ID, bima na picha ya gari na taktaka zingine. Akanambia ndani ya siku 3 itakua tayari.
Baada ya siku 3 akanicheki ghost akanambia account yako ipo tayari, akanipa password akanambia download bolt driver app kwa simu then anza kazi. Kweli nikafanya nikaona mambo yako supa nikaona sehem ya kwenda online kama unataka request, nika touch pale nikaona inasearch nikazima data nikalala, nikaplan kuingia mzigoni jioni.
Nimeshapata account ya bolt tayari nini kitaendelea? Mama Junior hajui kama nimeamua kufanya hii kazi atakubali?? Usikose mwendelezo story tamu ndo zinaanza sasa, usikose bando tu.