Chereads / Ethiopian Hababity!! / Chapter 7 - CHAPTER 6

Chapter 7 - CHAPTER 6

Muda huo dada naye dizaini kama alikua yuko dunia nyingine ameshapagawa tayari, nikimtazama na ule uzuri na lile paja lilivyokua jeupe huku kwangu mnara unasoma 10G. Mara dada akaanza kutafuta nzipu ya jeans yangu kitendo cha kuweka mkono pale ni kama akili ilianza kurudi, nikasema hivi nafanya nini? Who's this girl? palepale nikashuka kwenye gari nikanawa uso, nilikaa pale nje nikijifikiria maana kuna roho inanambia nimle nyingine inanambia nisimle, lakini roho ya kumla ilikua ikishinda.

Nikaingia kwenye gari kuchek map ni kama kidogo namaliza trip, dada alikua anakaa Shoppers kwa nyuma huku, dada akawa anaendelea kutaka kuingiza mkono kwenye jeans yangu nikawa namzuia, ndani ya muda mfupi tukawa tumefika, nika end trip akanipa pesa yangu. Dada hakutaka kushuka akawa ananambia tuondoke wote na yuko serious kabisa.

"Please bro! I'm horny", dada ntakucheki kesho now nipo kazini, "bhs ntakulipa muda wako" huku akilalamika, ghafla geti lilifunguliwa alikua ni mlinzi , nikashusha kioo "kaka naona umepaki muda sana sikuelewi " alivyomwona dada akanyamaza, "kaka unamjua huyu dada?", ndio namjua anaishi humu, "bhasi msaidie aende ndani hayuko sawa" kabla hajashuka akanibusu shavuni "I have your number, ntakupigia".

Nyie yule dem alikua mzuri sana kwakweli tuache utani "@riki boy atanisamehe kwakweli"

Na kwa mazingira ya pale nilompeleka nilijua dem ni mtoto wa kishua.

Sikuamini kama nimeushinda ule mtihani maana ulikua ni mgumu balaa yaani mpaka nafika home nilikua nikimwazia yule dada, huku roho ikinambia kesho mtafute.

Kutokana na lile tukio palepale baada ya kurudi home ilibidi niripoti kwa uber chap maana niliogopa dem nimemkazia asije akaniripoti vibaya kama "nimemharras", Uber wako serious sana maana hawachelewi kukutia bann.

Unajua madereva wengi wa Uber hapa ndo wanakofeli yaani ukiendekeza mapenzi na kazi ni kama unajichimbia kaburi mwenyewe. Hakuna kazi ngumu kama ya uber yaani ni kunavishawishi vingi sana haya matukio ya kutakwa kimapenzi ni mengi mno, hawa wanawake ambao hawajitambui ni wengi mno yaani kama huna self control utaishia kuwala tu. Na kwa upumbavu unalala nao humohumo kwenye gari unazidi kujiweke nuski, balaa na mikosi.

Hakuna watu wenye siri kama maderva wa Uber kama hapa Dsm usiku kuna mambo mengi ya siri na aibu yanafanyika kila siku. Usiku ndo muda ambao mashoga yanatoka ni mengi sana hapa Dar na usafiri wao ni uber ni masumbufu sana haya mawatu. Kuna illegals nyingi zinafanyika kwenye huu mkoa bado uzinifu ni hatari, kama weekend huwa tunapishana kwenye Apartments tunawashusha na kuwabeba dada zetu ni hatari sana.

"Ilifika stage nikasema hii kazi licha ya kupata pesa ila ni kijishushia hadhi mfano unabeba mishoga inaanza kukutongoza, hawa watu sijawai kuwakubali lakni kutokana na hii kazi lazima ukutane nao, na wanasumbua sana, ni waongeaji mpaka wanakera".

Mimi binafsi before ya kwenda mzigoni nilikua nasali kwanza ile asubuhi ndo naondoka, hata mambo mengi nilikua nayashinda sababu ya Mungu na sio akili zangu, ni ngumu sana kukwepa mishale yote pia.

*******

Asubuhi niliamshwa na simu ya Mama junior kama kawaida yake alikua akilalamika kwanini sijaenda jana na niliahidi ntakwenda, ikabidi nimpe sababu ili aelewe

Mama J: Toka nitoke hapo home sikuhizi sikuelewi kabisa ni umebadilika sana Baba J, hautujali kabisa, sasa kesho mimi narudi nyumbani na mtoto maana nikiendelea kukuacha nitakuta umeweka mwanamke humo ndani, hapana bora nirudi tu.

Mimi: Hapana mke wangu huko unafika mbali sana na plan mkesha huu wa mwaka mpya tuwe hapo home wote nina mpango wa kununua mbuzi kwaajili ya mkesha. Baada ya mwakampya nitakuja kukuchukua, wewe endelea kutafuta dada wa kukusaidia kazi.

"mama J ni mtu ambaye anakuaga na hasira sana ila ukishamalizana naye akaona sababu ina mantiki hanaga shida".

Hii siku ilikua jumapili boxing day hapo muda unasoma saa5 asubuhi nilikua nimechoka sana na ile mikiki ya jana, nikasema hapa acha nipumzike mchana nianze kazi. Soon Maggy akaanza kupiga simu, nikapokea "Bossy wangu naomba leo kama unaweza uje hapa home utupeleke Tabata Segerea, please". Sikutaka kumkatalia ukitegemea Maggy kashakua tayari familia na mteja wangu.

Palepale nikasema acha nipeleke gari car wash ikapigwe soap, gari mimi nilikua napenda kuoshea pale Juliana pub, wale jamaa wa pale ni washikaji zangu sana.

Kuna jamaa pale anaitwa "Kelvin" ndo mtu ambaye nilikua napenda sana kumpa gari aoshe, bhasi nikaona Kelvi anakuja kwangu akanmbia kaka ulidondosha simu huku anikabidhi mkononi, nilikua nashangaa simu!!??, nikajua lazima kuna mteja aliidondosha, kelvin akanimbia ilikua chini ya kiti cha pembeni kwa dereva upande wa chini karibu na mlango.

Simu yenyewe ilikua ni iphone 13 Pro Max latest kabisaa, wakati nikiendelea kufikiria itakua ya nani nikasema niiwashe lakini ilikua haina chaji. Nikaiweka mfukoni nikaingia zangu ndani kula kitimoto "Juliana wanakitimoto kitamu sana".

Nikarudi home ili nianze kujiandaa ili nikameet na Maggy kule Mikocheni, nikaichomeka ile simu kwenye chaji mimi nikaingia kuoga, sasa wakati niko bath Maggy alikua ameshaanza kupiga simu kwa kasi na 14:00 ilikua inabidi niwe nimefika eneo la tukio.

Kutokana na ile haraka mimi nikaisahau ile simu home, nikafika kwa Maggy mapema sana na nilikua nimependeza nimetupia jeans, raba yangu ya nike, shati ya jeans na cap , sikutoka kizembe.

Karibu ndani bossy wangu ilikua sauti ya Maggy huku akitabasamu "umependeza" nikamwambia sitaki kukutia aibu huko unakokwenda, kweli hata mimi naona sio kwa kuwaka huko.

Maggy alikua na best zake wawili hao tukaelekea Tabata tulitumia saa 2 kufika eneo la tukio sababu ile Mandela Road ilikua na foleni sana. Tukio lenyewe ilikua ni "BABY SHOWER" kama mnavyojua mambo ya wanawake matukio mengi, nikajisemea kweli "Mama Junior Bora haya mambo alikua hana time nayo".

Kutokana na wageni wengi walikua ni wanawake pale japo na baadhi ya wanaume walikuwepo, hivyo niliamua kutafuta sehem niende kupoteza muda. Sasa ile natoka Maggy akanifata akanambia usiondoke please, nimewaambia wewe ni ndugu yangu hivyo ukiondoka haitakua vizuri.

Nilibaki kwenye hilo tukio lakini sikuwa na mzuka nalo wala nini maana niliona hayo ni mambo ya wanawake sana.

Event ilikwenda mpaka mida ya saa 2 usiku ndo ikaisha hivyo tukaanza kurudi, wakati tuko njian wakawa wanadiscus jamani na hili vibe tunakwenda malizia wapi??

"Kidimbwi..? aahh pale sipapendi nyie…, shoga pale pana watu wengi sana, sasa twende wapi?? Maana wewe kila sehem hutaki…." Walikua wanajadiliana mwisho wa siku wakakubaliana waende Samaki samaki, Mlimani city.

Kuna dada akaniuliza "eti kaka Samaki samak pazuri??", ndio kwa jumapili pale Mlimani pana vibe na leo sikukuu bado kitawaka sana.

Nikawarudisha mpaka Mikocheni ilikua ishafika saa3 muda huo, wakabadilika chap aisee walikua wamewaka sana hapo nikagundua kumbe Maggy naye ni pini sana, tukaanza safari ya Mlimani city. Nikawadrop pale Maggy akanambia nijoin nao maana mimi nilitaka kusepa, nikaamua kuwajoin.

Tulikaa pale mpaka saa7 usiku nikamwambia Maggy kesho kazin vipi? akanmbia kesho haendi wako off. Muda ule nikawarudisha Maggy na best yake pale kwake best yake mmoja ambaye alikua anakaa Kimara ali request usafiri wa kumpeleka kule kwake.

Baada ya kuwadrop pale tulikua tukipiga story na Maggy baada ya best ake kutangulia ndani, akanambia jumla itakua kiasi gani? nikamwambia leo nakupa offa angalia pesa ambayo haitakuumiza wala kuniumiza mimi, akanipa 70k, mimi nikarudi zangu kulala.

Wakati nimerudi home niliangalia ile simu kuangalia kama kuna watu walipiga kama nilivyohisi nitakuta watu wamepiga sana. Nilikua siwezi kufanya chochote maana ilikua na password.

Asubuhi niliamka mapema sana kwenye saa1 asubuhi ile simu ilianza kuita nikapokea chap.

Anonymous: Mambo Prisca(code), mbona hupokei simu zangu toka jana mchana?

Mimi: Kaka mambo vipi, unamjua mwenye hii simu?

Anonymous: Ndio kwani wewe ni nani? na inekuwaje unapokea simu zake??

Mimi: Bro tulia kwanza, mimi ni dereva Uber jana nimepakia wateja wengi sana kama unavyojua ilikua ni sikukuu, jana nimeiona simu saa6 baada ya kuipeleka car wash ilikua iko off, baada ya kurudi nikaisahau kwenye chaji mimi nikawa nimekwenda mzigoni, kama unamjua huyu mtu naomba anitafute nimpe simu yake.

Anonymous: Ok, kuna best yake namjua ngoja nimpigie simu, nitumie na namba yako.

Mimi: No problem, 0765*******

Nikatoka hapo chap kuelekea kumchukua Mama wawili nimpeleke kazini, this time mama wawili alikua peke yake. Vipi mke wangu yuko wapi leo?,,Aah hizi week 2 zilizobaki nimeona apate likizo, sikutaka afunge shule mapema ili apate mafunzo ya computer.

Baada yakufika pale Posta na kumdrop mama wawili haikuchukua muda simu ikaanza kuita ile iphone 13, nikapokea ile simu "Kaka mimi ni Prisca ndo mwenye hii simu ulinichukua pale Maison ukanileta mpaka kule Shoppers,

"Sawa dada nimekukumbuka sasa simu yako ntakupaje..?"

"Mimi niko home tu, niletee ntakulipa pesa yako"

Ok haina shida, nipe namba ya kuwasiliana na wewe.

**********

Mimi niliendelea na majukumu yangu ya kazi kama kawaida tena hii siku nilikua na bahati sana. Nilipiga kazi mpaka jioni nikampigia simu yule dada kwamba niko njian nampelekea simu yake, akaniambia ukifika wewe piga honi nitatoka.

Kwenye saa1 jion nilikua nimefika pale akatoka,

Prisca: Kaka mambo!

Mimi: Safi mzima? za toka siku ile!

Prisca: Ukaniacha na hisia zangu, wewe ulikua wangu tu mpaka nikasahau simu jinsi nilivyokua nimepagawa na wewe.

Mimi: Sema uliacha kwa makusudi ili nikutafute, huna lolote.

Prisca: Karibu ndani bhasi,

Mimi: Huko ndani mimi siingii.

Prisca: Ok ngoja niingie kwenye gari!

Mimi: Simu yako ni aina gani?

Prisca: Kwa madaha, Iphone 13 Pro Max, colour gold, na nimeweka wallpaper yangu.

Mimi: Nitajie password, huku naitoa simu kwenye droo

Prisca: 234567

Mimi: kweli dada simu yako, nikamkabidhi

Prisca: Kaka ahsante sana yaani sijui nikupe zawadi gani, maana nilikua najua nimeipoteza kule Maison yaani idea itakua nimesahau kwako sikua nayo kabisa. Nilijua nimepoteza simu yangu, una roho nzuri sana.

Mimi: Usijali hii ni vitu vya kawaida!, mimi nataka kuondoka.

Prisca: Nisubiri nakuja, huku akiingia ndani.

"Prisca aliingia ndani nikawa namsubiri pale nje getini, baada ya dk5 akawa amerudi kashika kibahasha."

Prisca: Kaka hii mimi ndo Shukran yangu huku akinikabidhi ile bahasha ndogo na hii ni nauli yako alitoa cash 20,000.

Mimi: Ahsante mrembo ila sikuhitaji shukrani yako!, sasa ilikuaje mpaka ukalewa vile siku nyingine utabakwa, shukuru Mungu ulikutana na mimi mstaarabu.

Prisca: hivi ulinichukulia mimi kama malaya hivi?

Mimi: Ndiyo au hapana ila kwa Mwanaume anayejitambua hawezi kusex na mwanamke ambaye hajitambui kama ulivyokua wewe jana, pale ningekua nakubaka.

Prisca: Ni wanaume wachache sana wenye kariba kama yako ambao wanaweza kujizuia, natamani sana kupata mwanaume dizaini yako.

Mimi: Biblia inasema utapata wa kuendana nae kama wewe ni mlevi utapata hivyohivyo mlevi mwenzio, sio unataka mwanaume anayetambua afu wewe hujitambui, thubutu!

Prisca: Sawa bhana naona unanikandia, jana nimelewa kwa stress tu lakni mimi siko hivyo kaka, I swear

Mimi: Ina maana jana angekua mtu mwingine ungeliwa sio kwa zile ny*ge.

Prisca: Sijui hata niseme nini, ukweli wakati na request nikaona ID yako nilitokea kukuelewa na nilikua nafeel niko sehem salama.

Mimi: Wewe jitetee kama ni tabia zako ntakuotea tu!

Prisca: kweli, so bado upo kazini au unakwenda kwako?

Mimi: Vipi unataka tuondoke wote?

Prisca: Muda umekwenda mzee anarudi sio muda, wewe niambie nikutafute lini?

Mimi: Muda wowote utakaohisi mimi niko free!

Baada ya kuona story haziishi ndokama zinazidi kupamba moto nikamwambia mimi nasepa, tutawasiliana. Ofcourse Prisca alitokea kunielewa na kile kitendo cha kutokumla inaonekana kilimpa maswali sana, hata yeye alikua haamini kama nilimwacha salama.

Nilivyorudi home kucheki kile kibahasha nikakuta dada aliweka 300,000/= ya shukran. Ilikua ni saa 3 kasoro tayari simu ikaanza kuita kupokea alikua ni Prisca akanishukuru sana akampa simu na dada yake niongee naye. Dada yake anashukuru pia "kaka una roho nzuri afu inaonekana huna tamaa, maana kwa maelezo yake jana Prisca hakutegemea kama ingekua kwako, tutakutafuta siku tufahamiane nakama na kazi ntakua nakutafuta", nikamwambia haina shida dada karibu.

******

Ilikua alhmisi tukiwa week ya kumalizia mwaka 2021, nikiwa mzigoni kama kawaida yangu simu ikaanza kuita ilikua namba ngeni, nikaipokea ile simu kumbe alikua ni mchepuko wa mzee so alikua ananiambia mzee anasema hakupati kwenye whatsapp yeye yuko Egypt, nimtafute kupitia whatsapp.

Baada ya kuanza kazi niliamua kusajili namba nyingine kwaajili ya mambo ya Uber sikupenda kuchanganya mafile, wateja wangu wote nilikua nawapa namba ya voda.

Palepale nika download "Whatsapp business" nikamtext mzee, ilipita 1hr akaja kunicheki, akaniambia yuko safari anarudi ijumaa so nikamchukue Airpot afu nitampeleka Bagamoyo na mchepuko wake na watarudi jumapili.

Nikawa na mawazo mzee anakuja ijumaa na sijui ataingia muda gani na pia itakua 31/12 nlishamwambia wife lazima niende kwenye mkesha kwao. This time mama J hawezi nielewa kabisa na mzee kumkatalia siwezi so hapo nilikua naomba sana Mungu mzee awai kufika.

Ile ijumaa asubuhi mzee akanitext kwamba mchana atakua amewasili airpot niwe ontime pale, aisee nilifurahi sana kusikia mzee ataingia mapema, nikaenda kukutana na jamaa ambaye nafahamiana naye pale tegeta nyuki ni anauza bucha, nilimwagiza dume la mbuzi lenye afya lije limeandaliwa kabisa. Nikamwagiza boda apeleke ukweni.

Wakati tunachat na mzee alikua anauliza kama na mimi ntabaki huko Bagamoyo au laah, nikamwambia mzee mimi siwezi kubaki huko ntawapeleka then ntakuja kuwafata siwezi kulala huko usiku 2 ntakupa sana cost. Nikamweleza mzee kazi jinsi ilivyo tukakubaliana 300,000/=. Huyu mzee tumuite (Mzee Pama), alinipa sana maisha huyu mzee kwakweli, alikua na roho nzuri sana.

Nikawasiliana na mchepuko wake nikamwuliza tunakwenda wote kumpokea mzee au niende afu yeye nimpitie Posta?, akasema nimpitie Posta tunavyorudi itapendeza.

Mzee aliwasili 11 jioni nikampokea safari ilikua kwenda Posta kumpick dada then twende Bagamoyo. Ilikua kama bahati ile tunafika pale kivukoni na Panton ilikua ndo inashusha, tukamchukua dada hao Bagamoyo.

Tuliingia Bagamoyo kwenye saa 2 kasoro kuna Hotel niliwapeleka ipo karibu na Beach pazuri sana pale sipakumbuki jina. Mzee akanipa 100,000 akanambia nenda kale sikukuu kijana wangu hakikisha unakuja mchana mapema kutuchukua, ntakupigia simu pia. Nilimshukuru sana mzee nikageuka kurudi Boko kwa wife maana hapo alikua anapiga simu mpaka bhasi.

Nilitumia nusu saa tu kufika pale Boko nilikuta mbuzi ishaanza chomwa pale watu walikua kama wote nazungumzia dada zake, nk tulikesha pale kuupokea mwaka mpya. Kiukweli mwakampya 2022 niliupokea vizuri sana mambo yalikua mazuri sana siku ile.

Nilitoka pale saa 7 nikaenda moja kwa moja home kulala, nikaplan asubuhi niende church then niingie mzigoni "leo lazima nikeshe". Wakati nimeingia home tu Prisca akanipigia simu eti ananiwishi "Happy new year" nikamwambia ahsante, akaendelea Insider kesho tuonane bhas if possible nitakua na dada yangu anataka akuone…, "mmh dada yako umemwambia nini wewe mbona spidi sana?"…. Sikia mimi kesho ntakua busy sana siwezi kukupa ahadi yoyote kwa sasa tutacheki siku nyingine itakua vizuri zaidi.

*********

Ile jumamosi nilianza mzigo saa6 mchna baada ya kutoka church nilipiga sana kazi hii siku maana request zilikua zinaita tu afu sasa zilikua zile trip ndefu na hizi trip zinakuaga na hela sana.Hizi trip ukipiga zako 4 unakuta ubao unasoma 100k tayari.

Nilipiga kazi mpaka inafika saa 2 usiku nilikua nishaingiza laki na point kadhaa, bhasi nilikua pale karibu na 5N pembeni kuna jamaa huwa anauza soup ya pweza ni mtaalam sana. Nilikua napata soup yangu pale mdogo mdogo hapo nilikua nimezima App sikutaka usumbufu kabisa pia nilikua navuta pumzi.

Nilitumia 1hr kupumzika na kujiweka fiti kwenye saa3 tayari nilikua nimepata request tayari ya kwenda Madale huko, mimi nilikua sichagui request sehem yoyote kambi kama mteja anaingia barabara mbaya namkodia bodaboda impelekee.

Nilimpeleka mteja Madale kwa bashasha zote siku nzma nilikua nasikiliza album ya The weeknd "After hours ", gari safi inanukia vzr na kale ka mziki kwa mbali ilikua burudani sana.

Nilimmdrop mteja pale wakati nageuza gari naitafuta barabara kuu, nikapata request nikampgia mteja "Kaka njoo haraka niko Montana hapa" nakumbuka mteja alikua anakwenda Ilala, pale Ilala nikapata request nyingine ya kwenda Slip way Masaki.

Pale Slip way nilisubiri subiri kama nusu saa nikapata request ya kwenda Mbagala- Rangi tatu, lakini nikawa nawaza niende au laah, nikaamua kwenda, nikamwambia mteja nakuja, "kaka siamini kabisa maana Bolt hawataki kwenda kule". Yule alikua ni mama mpemba alikua mwongeaji sana ile trip ilikua ni stori sana, nilimdrop mteja palepale Rangi 3.

Pale mbagala nilikaa karibu nusu saa lakini sikupata request, nikachoma wese mpaka zakhiem pale nikashuka kwenye gari ili nipunge hewa. Nilikaa pale kama nusu saa nikapata mteja alikua anakwenda Kigamboni kibada nilitaka nigome lakini nikasema acha niende, nikamdrop mteja, kama zali ile namshusha mteja napata request ya kwenda Masaki "Havoc pale Barometer", nilifurahi sana.

"Kaka fata ramani nachelewa toll fee pale darajani ntalipia" ilisikika sauti nzuri ya mrembo, nilifika dada alikua ananisubiri kama alikua na haraka sana.

Nilimdrop pale mteja, kucheki ubao ulikua ushafika 200k tayari, hii siku nikasema hivi kama ningeanza asubuhi si ningekua niko parefu sana. Nikaamua kwenda kupark gari pale Masaki mwisho zinakogeuzia daladala. Pale mara nyingi huwa navizia requests za maeneo ya pale, coral beach, na seacliff "kuna jamaa alinipaga hii trick kwamba niwe natega pale ni pazuri, unachomoka haraka".

Muda huo ilikua saa 9 tayari wakati naenda kuchili maeneo yale, ninakuta wahuni wa 2 wa uber washatia kambi tayari, zikaanza story kila mtu anaonesha ubao wake, kila mtu ubao ulikua uko vizuri siku hiyo. Nilikaa pale jamaa mmoja akatoka alipata request tukabaki na jamaa kidogo jamaa nae akatoka nikabaki mimi pale peke yangu.

Nikaingia kwenye gari baada ya kuona niko peke yabgu, iliku sa10 kasoro tayari muda huo nakumbuka, nikasema acha nikalale tu nipumzike zangu tu kwa leo inatosha sana. Nikaamua kuset destination ya Mbezi beach home, baada ya dk 5 hivi nilipata request mteja anakwenda mwenge lakini alikua mbali nikaamua potezea.

Sasa baada ya dk 10 nikaona kama sipati request nikaamua kucancel tu nikomae na za kawaida kama ntabahatisha inayokwenda huko sawa. Haikuchukua dk 2 nikapata request mteja alikua "Marina Towers" apartments, hapo tayari nime accept ile request lakini nikawa nawaza niende au nipige chini??, ghafla text ikaingia "Niko Marina Towers, ukifika nijulishe". Nikawaza nimeshakaa sana pale acha niende tu, nikafika pale Marina Towers hii ndo ilikua siku ya kwanza naingia kwenye hizi apartments.

Baada ya kufika pale mlinzi akafungua geti "Uber eeh, ingia paki pale" hawa walinzi bwana wakionaga IST tu wanajua uber. Nikaingia ndani nikamtext "Niko parking"….. nikasubir mpaka dk 10 kimya mtu hatokei, kutokana na kuwa na usingizi nikaamua kuegemea kiti palepale nikapitiwa na usingizi.

Nilishtuka baada ya kuona mtu anahangaika kufungua mlango maana ulikua locked, nika unlock akaingia "kaka samahani nimekuweka sana" nikamwambia si umeona karibu dk 40 nakusubiri, "kaka usijali ntakurefund", wakati tunatoka getini "kaka si umeona wapi tunakwenda?" ndio si Sinza??… "Mmhh mmh wewe ni kijitonyama karibu na Grand villa hotel"… Ok nishakusoma dada.

"Kaka sorry can I sleep?", dada alikua anauliza, nikamwambia dada hii gari ya abiria wanapanda watu wengi kama utakua comfortable unaweza lala ni wewe tu. Muda huu nilikua simzingatii kabisa huyu dada maana nilikua na usingizi si unajua ile ukiwa unadrive afu unahisi usingizi.

Nilifika mpaka kijitonyama nikamdrop dada, before hajashuka akaniambia kaka ntakupigia simu ili tuongee kuhusu biashara, naomba namba yako, nikamwomba simu nikachora 0765******, ahsante uwe na kazi njema.

Sasa ile ametoka anafungua geti sindo namwona dada vizuri aisee moyo ulipiga "paaahhh", aisee mbona hii pisi kali sana ni huyu dada ambaye nimempakia??, nilikua nawaza pale huku nikishuhudia dada akimalizia kuingia ndani.

Ndugu zangu yule dada alikua ni mzuri sana tuache masikhara kwakweli japo ilikua usiku lakini nilisema sijawai pakia dada mzuri kama huyu….