Chereads / Ethiopian Hababity!! / Chapter 8 - CHAPTER 7

Chapter 8 - CHAPTER 7

Baada ya Mwaka mpya kupita Mama Junior "Mama J" alirudi home tuendelee na maisha alikua kashapata dada wa kazi. Toka arudi sikutaka kumwambia lolote kama nimeanza biashara ya uber, nilijua kitendo cha kumwambia angeleta shida maana ni mwanamke ambaye ana wivu sana hivyo angenisumbua sana.

Niliamua kubadilisha ratiba zangu za kazi na kuwa Unpredictable nikaplan kuacha kukesha kwa weekend niwe naanza kazi mapema na kumaliza mapema lakini nihakikishe silali nje na home.

Mama J baada ya kurudi home alirudi ameimarika sana sijui mama mkwe alikua anamfanya nini huko kwao maana hata mikiki ya kitandani alikua anahimili sana, toka ajifungue ilikua ni miez 6 tayari.

Kwa upande mwingine Prisca aliendelea kunitafuta sana na mimi sikupenda kabisa kumpotezea maana niliona ni mteja tayari anaweza pia kunipa connection za kazi nyingi, mimi nilikua nawaza hela tu.

Kazi yangu ya kuwachukua Maggy na Mama wawili ilikua ikiendelea vizuri kabisa na mimi niliendelea kupambana na kazi huku nikiwa na mipango yangu mingi kichwani.

Prisca alinitafuta jumamosi ilikua ni week ya pili kabisa ya mwaka mpya toka uanze so akaomba tuonane jioni if possible, nilimkubalia.

Jumamosi mimi nilishinda home siku nzima sababu nilikua na wageni kutoka kwa wafanyakazi wa Taasisi X ambayo nilikua nafanyia kazi kipindi kile, walikua ni kama ndugu kwangu kwenye ile department. Kwa mara ya kwanza walikuja kunitembelea kwangu pamoja na kuijulia hali familia yangu.

Ile jioni tuliwasiliana na Prisca kumwuliza tunakutana wapi, tukakubaliana kukutane kidimbwi. Wakati nawasindikiza wageni mimi nikaenda na uelekeo wa Kidimbwi, muda huo Prisca alikua kashafika so alitext kunipa taarifa kuwa kafika. Niliamua kwenda kuonana naye sababu niliona kumkwepa sio solution sababu nilikua tayari najua nia yake hivyo nilisema nitatafuta njia ya kudeal naye lakini niendelee kumweka close.

Wakati nafika kidimbwi ilikua saa 1 usiku tayari, Kidimbwi kwa siku za kawaida panakuaga pametulia sana "very romantic place". Baada ya kucheki nilimwona alikua na mtu mwingine so nilihisi atakua ni dada yake tu.

Nilifika pale nikawasalimia, "bila shaka utakua ni dada yake na Prisca" akatabasamu dada yake huku akitikisa kichwa.

Prisca akanitambulisha huyo ndo dada yangu Insider anaitwa Mary (code). Ukweli Mary alikua ni pini kushinda Prisca na walikua wamefanana sana.

Na muda huo mhudumu alikua kafika tayari, ajabu mhudumu alokuja ndo yule ambaye alikua akituhudumia ile siku niko na kina Manuel.

"Kaka mambo za siku?" Mhudumu alinisalimia huku akitabasamu, ofcourse na mimi nilikua nimemtambua yule dada, nikamjibu afu nikamwagiza Bucket ya Heineken, hii siku nilikua najiskia kulewa sana maana toka nianze mikiki ya Uber sikuwai kutoka nika enjoy life, sio kwamba nilikua sina hela hapana bali niliamua kuweka kipaumbele kwenye kutafuta Pesa.

Sasa bwana akina Prisca wakawa wananiangalia hawakutegemea kama mimi nitakua najulikana maeneo yale baada ya dada kutusikiliza wote, wakaniuliza dada kanijuaje??, nikawaambia dada akirudi wamwuulize atawapa jibu lao.

Story zikaendelea pale sasa Mary akadakia…"nimeamua kuja kumwona Mwanaume ambaye anampagawisha mdogo wangu ambaye anafanya asilale."

MIMI: "Mimi nafikiri angeanza kutupa mkasa kwa kile kilochotokea mpaka akaamua kwenda kulewa maana alinambia alikua na stress"

PRISCA: "Unajua Insider ile siku nilikua na stress sana na yote sababu ya mwanaume, niliamua ile siku niende kwa boyfriend wangu sikumpa taarifa kama nakwenda nilitaka kumfanyia saprise, you can't imagine nikamkuta na gal mwingine so nilipata hasira nikaamua kwenda kunywa pombe na best yangu"

MARY: "Yule mwanaume alikua bitch tu, nilikuambiaga mapema ukawa hunielewi, shida mdogo wangu unapenda mpaka unaoza"

MIMI: "Aisee pole sana siwezi kukutetea wala kumtetea ila nikwambie pole sana, usipende kunywa pombe ukiwa na stress za kuachwa utakuja kuliwa kimasihara afu yakawa majuto"

Tulikatisha maongezi yetu wakati dada akiwa amefika na vinywaji pale akiwa ameweka kwenye dishi la karai na ice za kutosha, kwa upande wa kina Prisca walikua wameagiza wine "4 cousins"

Palepale Prisca akamwuuliza yule dada, eti huyu kaka umemjuaje?

Dada alitabasamu akawa ananiangalia nikamwambia "go on"

"Ni mteja wetu muhimu" dada akatabasamu akaondoka.

MIMI: Mary unajishughulisha na nini?

MARY: Nasoma bado, nasomea Mastaz ya Business Administration.

MARY: Ukweli baada ya Prisca kunipa mkasa mzima na kutomfanya chochote then kumrudishia simu yale niliamini wewe ni mwanaume wa kipekee sana kwa dunia ya leo.

MIMI: Kama leo hii hata nikisema naenda kumla ni halali maana tushajuana tayari au nasema uongo Prisca?

Wakati naongea na Mary, Prisca alikua busy sana na simu yake.

PRISCA: Sorry, ulikua unasema?

MIMI: kama hujaskia bhasi.. Mary tuendelee na story zetu.

Mary baada yakuona Prisca hajaskia nilichokua naongea aliamua kunyamaza huku akicheka licha ya Prisca kuomba amwambie.

Tulikaa pale mpaka saa 5 lakini tulikua tumepiga sana story ila Mary alinifungukia kuwa mdogo wake ametokea kunielewa sana, kwa upande wangu sikumwambia chochote kile.

Niliwarudisha kwao Prisca akanambia anataka kuja kunisalimia kwangu, nikamwambia na mimi nakaa kwa wazazi kama wewe, niliamua kumdanganya tu.

*********

Kuna mteja nilimpakia Kariakoo mitaa ya Lindi/Congo huyu alikua ni dada pia alikua na mizigo ya ream paper, alikua anaelekea Masaki-Olive sasa ukiendelea kushuka kwa chini kuna shule, yule dada nilimshusha pale.

Baada ya mazungumzo kadhaa akaniuliza huwa napaki wapi gari yangu?

Nikamwambia mimi sinaga eneo maalumu lolote la kupaki hii ni Uber popote kambi tu, ila kama unakazi mimi sina shida tunafanya.

"Ok nina watoto hapa kila siku huwa nawakodia uber tofauti mmoja anakaa Mikocheni, wawili wanakaa Kunduchi kwanini usiwe unawachukua? na kwa kila mtoto ukipata pesa sio mbaya. Natamani kupata mtu ambaye nitamwamini niwe nampa hawa watoto hata usalama wao utakua wa uhakika, kuliko kila siku kupanda uber tofauti"

"Dada haina shida wewe ongea na wazazi wao sidhani kama watakupinga wewe madam, pia hili jambo ni kwaajili ya usalama wa watoto wao"

Tukabadilishana namba za simu huku akiahidi kunitafuta tufanye kazi.

*******

Ilikua jumatano "Mapinduzi day" hii siku nilikua zangu home nikicheza na Junior. Sikuingia mzigoni sababu ya sikukuu kazi zinakua chache hivyo niliamua kupumzika tu.

Hiyo siku niliamua kufanya usafi wa gari mwenyewe home na kuikagua gari kwa ujumla, mara moja moja huwa nafanya usafi wa gari pale home. Ilikua kama saa 9 mchana wakati nimetoka kuoga simu ilianza kuita kucheki ilikua ni namba ngeni kwangu ya tigo 0715*******, nikapokea ile simu.

ANONYMOUS: Kaka mambo mimi ni Iryn ulinishusha pale kijitonyama, "baada ya kuona bado mimi simkumbuki akaendelea"… ulinichukua pale Marina Towers, nakaa hapa karibu na Grand villa hotel.

MIMI: Dada nimekukumbuka, uko salama?

IRYN : Niko poa, sasa upo wapi?

MIMI: Niko home tu, leo sijatoka

IRYN: Nahitaji tuonane Mlimani city jioni by 18:00

MIMI: Sawa haina shida dada

Ukweli sikutegemea kama yule dada angenicheki licha ya kuchukua namba yangu, sikuamini kama alikua binadamu wa kawaida maana sio kwa ule uzuri aliobarikiwa.

Ile jioni nikatoka home 17:30 maana kutoka mbezi shule mpaka Mlimani city haikua mbali hivyo niliona nitawai tu na siku ile sikukuu hakuna foleni.

Ile natoka namkuta Mama J yuko seblen na dada wakiangalia tamthilia zao.

"Nilijua tu lazima unatoka jion, nilikua nakuangalia unavyoosha gari mwenyewe upo busy kumbe una appointment zako"

"Mama J unawazaga mbali sana, hata hivyo kuna mtu nakwenda muona hapo Mlimani city sichelew narudi soon, nikuletee nini ?"

"Ni nani huyo?, mwanaume gani huwezi hata kutulia na mwanao ukacheza naye, niletee mafuta ya nazi Ya Alinda (mafuta ya nazi ya kupakaa kwa watoto)"

"Sichelewi mke wangu soon niko hapa"

******

Wakati nimefika pale mataa ya Mwenge Iryn alikua kasha piga simu kuwa kafika amekaa "Samaki samaki" pale nje.

Hesabu zangu zilikua kamili kwani 18:00 ndo nilikua napark gari kwenye parking ambayo inatizamana na Samaki samaki.

Nilishuka pale huku nikielekea Samaki samaki sikutaka kupiga simu maana dada alikua kashaniambia alikokaa na mimi sio mgeni na maeneo ya pale hivyo nilikwenda direct huku nikitizama zile meza za nje.

Nilimwona Iryn akiwa peke yake huku akiwa mbele yangu akinitizama so akanipa ishara lakini

nilikua nishamtambua mapema kabla hajaniona.

Alikua ni mrembo ambaye namwona kwa macho yangu huku watu wakiniangalia baada ya kunipungia mkono, dizaini kama hawakuamini kama ndo mimi naenda kuonana naye pale.

Tulisalimiana pale ghafla niliona kama naanza kupoteza confidence taratibu lakini nilionyesha uanaume wangu pale.

IRYN: Kaka nimekupigia karibu mara 2 leo lakini hukupokea simu zangu, nilihisi utakua kazini.

MIMI: Hapana leo nimeshinda home nafanya usafi wangu binafsi na gari. Vipi lakini za toka ile siku?

IRYN: Safi, nilichukua namba yako nikasema nitakutafuta ili tuongee biashara kama utakua tayari.

MIMI: Kama ni biashara halali mimi sina shida nakusikiliza bossy wangu.

IRYN: Ok, nina biashara zangu ambazo huwa nafanya usiku mara nyingi ni weekend from Ijumaa- sunday lakini kwa sunday huwa inadepend na wateja, na mara chache siku za kawaida. Nataka tuongee deal la weeknd tu hizi siku za kawaida kama inatokea nitakua nakupigia kama utakua tayari sawa. Na pia nina saloon yangu Sinza huwa naagiza mizigo mbalimbali utakua unakwenda kuchukua.

MIMI : Sawa dada nimekuelewa labda ungenielezea vizuri hilo deal la weekend muda wa kuanza na kumaliza.

IRYN: Muda wa kuanza ni saa mbili usiku muda wa kumaliza ni complicated tunaweza wahi maliza au tukachelewa lakini haiwezi kuzidi sa10 usiku. Nilichopenda gari yako ina private plate No., then-you're so gentle.

MIMI: Ok nimekuelewa sasa nasikiliza offa yako maana hiyo itakua kazi ya kukesha ni ngumu sana, kama una offa nzuri nitaconsider proposal yako.

IRYN: Mimi siwezi kupanga bei inatakiwa wewe useme bei ili nione kama nitaweza au laah, au mwisho wa siku tubargain ili iwe "mutual benefit "

MIMI: utanipa 150 per night (niliamua kujilipua tu nione kama atakubali au laah).

IRYN: mhh kaka that is huge amount, naomba upunguze kama nililivyosema kuwe na Mutual benefit

Tuliongea pale mwisho wa siku tukakubaliana 300k kwa 3 nights na akasema kazi tunaanza weekend hii jumamosi.

Dada akaomba nimpeleke kwake kijitonyama, sasa wakati tunatoka pale aisee watu walikua wananiangalia balaa, labda walidhani natoka na mrembo IRYN. Kwanza hata mimi nilijiona kidume kuweza kuongozana na yule mrembo, nilimdrop IRYN pale kwake nikamwambia leo sitaki nauli yako nimekupa offa.

"Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.

Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana.