Chereads / Ethiopian Hababity!! / Chapter 5 - CHAPTER 4

Chapter 5 - CHAPTER 4

Wakati naanza hii kazi Mama Junior alikua hayupo home, alikua kwao ni mimi ambaye nilimpa ruhusa aende akapumzishe akili baada ya dada wa kazi kwenda kwao. Niliona mazingira ya kubaki peke yake na mtoto bila mtu wa kumsaidia mke wangu angeteseka, uzuri kwao ni hapahapa dar. Mama Junior ni mwanamke ambaye ana wivu sana na mimi kiasi kwamba huwa anahisi mimi nachepuka, inshort niseme ni mwanamke ambaye ananipenda sana.

***

Naam! ilikua ni jumatatu tulivu sana, nikakurupuka kitandani kucheki muda saa 5 asubuhi. Wakati naangalia muda nakutana na mcd calls za kutosha, nikakutana na messages,

"Bro! Good morning, how you doing??" -Manuel

"I'm worried about you.."- Manuel

"Kaka habari yako, ni mimi maggy uliyenipeleka Airpot last week, nahitaji tuonane leo if possible"- 0712*********

"Bae! Kwanini hupokei simu zangu? Upo na nani?"- Mama Junior

Kabla sijajibu hizo message nikacheki missd calls

"Mama Junior, 6 "

"Manuel, 2"

"New number, 1"

Akili yangu ikawa inawaza nianze na nani kati ya hao, nikaanza kupigia Manuel kwanza akapokea nikamshukuru kwa kampani ya pale Kidimbwi akanambia kama ntapata nafasi nipitie pale Sea cliff kuna kazi nyingine ya kufanya.

Nikampigia simu Maggy tukaongea akanambia anytime ukifika Posta utanicheki nikamwambia "sawa".

Nikapiga simu namba ngeni, kupokea alikua ni mama mmoja hivi nilishawai mpakia, na yeye anafanyia kazi moja ya bank pale Posta, Azikiwe.

Nikampigia simu Mama Junior niliamua awe wa mwisho sababu namfahamu vzr, na kwa kitendo cha kutopokea simu zake na kujibu messages nilijua lazima atakua kafura.

Nikampigia simu …

Mama Junior: "Umeshaagana na wanawake zako ndo umeona sasa unitafute kwa muda wako…, Unaweza kunambia jana ulikua wapi? na umelala wapi?"

Mimi: " Jamani… ndo salamu hiyo?"

Mama Junior: " Baba Junior tafadhali naomba maelezo…, mwezi umepita hata kuja kutuona na mwanao hutaki, una mambo yako wewe"

Mimi: " Mke wangu usifike huko… jana nilikua na washikaji walinipa mwaliko, nikaingia night sana, hapa ndo naamka…, hata hvo nimekupigia nikupe habari njema"

Mama J: "Habari zipi..?"

Mimi: "Mwezi wa 12 huu Christmas nataka wewe na Junior mpendeze, piga hesabu na gharama zote then Nitumie". Hapa nilikua nimemmaliza hata hasira zikaisha kabisa.

Mama J: "Sawa haina shida, I love you. Takecare"

Nikaamka kitandani kwenda kuoga, kwanza nilikua na mahangover ya pombe, nilipeleka backet 2 za heineken sio mchezo, na ukicheki mpaka muda huo sijapata hata soup, kwa wanywaji nadhani huwa mnajua. Dizaini kama nikawa na kauvivu ka kwenda mzigoni, lakini nikasema hapana lazima niende nipige hata kidogo then nionane na hawa watu.

Nilikua napambana sana kutafuta wateja wa private ili niwe na uhakika wa kazi na kupata pesa nyingi. "Nakumbuka Dullah alinisisitiza sana nijitahid sana kuwa na wateja wa private maana hawa ndo kila kitu, App sometimes zinazingua kuna siku kazi zinakua ngumu". Mfano kwa kila trip kamisheni ya Uber/bolt ni 25% yaani kama ubao unasoma 100,000/= hapo 25,000 ni yao yako 75,000, kwenye hio 75 hujatoa cost za mafuta, parking fee nknk. Ili uweze kupata faida ya angalau 30,000 kwa siku inabidi uingize kuanzia 70,000.

Kuna wale ambao wanaendesha kwa mikataba unakuta kwa bossy anapeleka 25,000-30,000, inabdi apambane kwa siku apate kuanzia 100,000/=, hapo unaona inabdi akili ya ziada sana.

********

Nikaingia mzigoni kama kawaida nikapiga mzigo nikapata mteja wa kwenda pale Aga khan, baada ya kumshusha mteja nikawaza kuonana na Maggy nijue anaishu gani na pia nikakumbuka na yule mama wa azikiwe. Nikasema leo ni "Two birds one stone" napiga ndege wa2 kwa jiwe moja.

Nikamvutia waya Maggy, akanilekeza ofisi yake ni pale Golden Jubilee tower, bhasi mimi nikasogea mpaka pale mtaa wa Ohio nikapark gari oppositie na Golden jubilee. Nikamtext ilikua saa inasoma 9 kasoro mchana.

MIMI: "hey boss niko around"

Maggy: "Umepark wapi?"

Mimi: "Opposite hapa na jubilee, near kibanda cha Mpesa"

Maggy: "Ok nakuja soon, bossy!"

Haikuchukua dakika 10 Maggy akawa amefika kwenye eneo la tukio tayari, nikamsalimia na nikamsifia "you look great", akatabamu akanambia "nawe pia".

"So tunafanyia haya maongezi hapahapa, au ndani ya gari??". Nilimwuliza

Akanambia sijala kwanini tusiende cafe? nikakumbuka hata mimi nilikua sijala chakula cha maana toka niamke, lakini nilikua sisikii njaa.

Nilikokuwa nimepark gari kwa nyuma yake au tusema opposite na "IT plaza" kulikuwa na cafe pale, bhs ndo tuliingia pale, mimi nikaagiza "dona choma" yeye akaagiza "kiepe yai, kuku". Hiki kicafe ndo niliingia kwa mara ya kwanza, ofcourse nilikipenda wanachakula kitamu afu ni cheap, so kila nikija Posta hapa ndo nilikua nakula msosi.

Tukaanza pale kupiga story sana, Maggy alikuwa anaongea "mimi usafiri wangu ni Uber kila siku asbh pamoja na kurudi so kama upo tayari uwe unakuja asubuhi kunichukua unanipeleka ofisn then jion sa12 unanirudisha home. Pia ninakazi nyingi sana huwa zinatokea hata za siku nzima, Uber wengi gari zao sio safi na wateja wetu wengi ni foreigners, jinsi ulivyo smart na gari yako safi ntakua na amani na wateja wangu.

Nikamwuliza before mimi ulikua unafanyaje? Akanambia nilikua namtu nafanya naye kazi ila hazingatii usafi wa gari. Mimi nikatabasamu pale,

Mimi nikamwambia suala la kuja kukuchukua niachie nilifanyie kazi ntakucheki badae tuyajenge kama tutaafikiana tutafanya kazi lakini suala la wateja wako mimi sina shida hili naweza kupa jibu la direct hapahapa, nikamwambia hao muda wowote nipigie simu hata Arusha tunakwenda, hata kama unasafari nje ya mkoa mim sina tatizo.

Tukaagana pale huku nikimwahidi badae nitamtafuta, palepale nikamcheki mama yangu wa azikiwe, Palepale nikampigia simu lakini hakupokea ghafla ikaingia text "Call you letter", nikamtext back chap "niko Posta", akanijibu "Na kikao nitakupigia nikitoka". Nikamjibu "Ok".

Kucheki muda ilikua saa 10 kasoro tayari nikasema acha nimsubiri huyu mama then nielekee Masaki kuonana na Manuel. Ukweli nilikuwa natamani sana kupiga story na Manuel maana ni mtu ambaye alitokea kunikubali sana afu hakuwa na roho ya kinyongo ni mtu poa sana. Nilitamani kuongea naye mengi kuhusu Siwtzerland ( "Switzerland ni moja ya nchi nzuri sana kwa foreigners, kusoma, hata upatikanaji kazi"). Plan zangu kubwa ni kutengeneza connection nijue namna kufika kule na masuala mengine.

Wakati narudi kwenye gari yangu nikaona kuna Uber kibao wametega around na mimi, nikaona kikundi cha washikaji wakipiga story nikajua wale ni Uber, bhs nikasogea pale kujumuika na mimi.

Matajiri kwema? za kazi?, wote wakajibu nikawaambia bila shaka nyinyi ni Uber, ndomana namimi nimesogea hapa nimevutiwa na story. Kwa muda mfupi tukawa kama watu ambao tunajuana kitambo.

Unajua story za madereva wa Uber nyingi ni kuhusu madem tu, ukiona Uber wamekaa kwenye vijiwe vyao hizo ndo story zo kubwa huji kuta wakipiga story za maendeleo hata siku moja. Inshort madem wanaliwa sana na madereva wa Uber.

Pale Posta najuana sana na maderva wa Uber wengi wananiitaga "Wakishua" sababu mimi muda wote niko smart na gari nayo ipo smart, hii ilipelekea kupendwa sana wa abiria.

********

Tulikua watu 6 pale lakini kadri muda ulivyokua ukienda na wahuni walizidi kupungua ikafika stage tukabaki wawili,, "Request ndo zilikua zinatupunguza maana kuanzia saa 11 jion ni muda ambao request zinakua nyingi sana Posta, demand ya ya Uber inakua juu sana hata rate ya nauli inakua juu sana.

Mpaka saa 11 naona kimya yule mama wa Azikiwe hajanitafuta, sikutaka kumtafuta kwanza nitaonekana kama mimi ndo nashida, then ataniona cheap sana, kwanza kitendo cha kumsubiri mpaka saa11 nilijiona fala sana.

Nika switch online App yangu nikaset destination ya kwenda Sea cliff, "ipo hivi kama unataka mteja wa kwenda Masaki au Posta, bhs kwenye App unaset destination, hivyo utapata request zinazoelekea usawa huo inaweza isiwe exactly point ila atlist inasaidia". So kitendo cha kuweka destinationa haikuchukua muda nikapata request ya mteja alikua anaelekea Coral beach.

Nikamshusha customer pale Coral beach nikachukua uelekeo wa Sea cliff, kutoka Coral mpaka Seacliff sio mbali sana, ilikua chap tu niko pale tayari. "Wakati nakaribia Coral nilikua nishampanga tayari Manuel so akanambia nitamkuta pale Karambezi".

Nikafika pale Karambezi nikamzoom Manuel kwa mbali ofcourse hapakua na watu wengi sana palikua kawaida tu. Tukasalimiana pale story zikaanza, story kubwa nilikua namwuliza namna ya kufika Switzerland na ishu za kazi especially unskilled jobs. "Njia rahisi ya kuingia chap ni scholarship au kusoma, hapo ni rahisi sana ila kama unakua umepata kazi bhasi mwajiri wako akupambanie visa japo huwa inachukua muda sana na gharama yake kubwa. Kama unataka kuingia wewe apply chuo, I recommend you to use this way, ukishafika ukaanza masomo kama mastars ni mwaka mmoja tu umemaliza, ukiwa unasoma kuna mishe nyingi sana za kufanya kule kama viwandani, mashambani, migahawani nknk" Manuel alikua akiongea.

Manuel mbinu nyingine ya kutumia ya haraka bhasi uoe mswiss hapo unapewa na uraia kabisa, "Nigerians wanatumia sana hii mbinu, wanaoa sana wamama watu wazima" nilicheka sana.

Ishu nyingine kubwa pia jumatano na alhamis nitakua na ratiba ya kutembelea vituo vya watoto yatima kwa Dar, ijumaa tutakwenda kibaha na Bagamoyo, ila kwa Jumamosi utaangalia wapi unatupeleka, then J2 tutaondoka kurudi Switzerland. Manuel alikua akiongea.

Akanionesha vituo tutakavyotembelea nikaona kuna sinza, tegeta, bunju, Kunduchi, Kimara, Kigamboni. Tukakubaliana 600,000/= ( 200,000/= per day) kuhusu jumamosi nikamwambia ntawapa offa, muda ule tulikua tunaikimbiza "pearly bay wine". Nikamwambia bro jana dizaini kama haukuwa free kule Kidimbwi, alicheka sana akanambia "bro! next time gonna be lit,". Tukaagana pale.

"The way nilivyomwona Manuel nilihisi kama mtu wa madem sana" huko mbele mtaona.

Before sijatoka pale Karambezi mama yetu alikua kanipigia simu ila sikupokea, so wakati natoka ilikua ishapita saa tayari, na saa yangu ilikua inaonesha ni saa 19:05. Nikampigia simu akanambia karudi home kama vipi niende kwake haina shida, "nikaona mama anaongea ujinga, yaani mimi niende kwake??". Nikamwambia mama haiwezekani kama muhimu sana tuonane pale Raibow , huyu mama alikua anakaa kule chini Mbezi Beach karibu na Rainbow. "So hakukataa akakubali tuonane pale tuongee".

Nikawa nawaza huyu mama anataka nini kwangu? Nikachoma mafuta mpaka pale Rainbow mbili kasoro dakika nikawa pale, wakati niko Kawe alikua kanijulisha kafika tayari.

Kufika pale nikaingia ndani nikamkuta amekaa anakunywa savannah, duu! nilijisemea huyu mama hatari au ndo anaongeza nyege!??.

Mimi: Habari yako bossy

Mama: Salama tu, ndo unatoka mishemishe?

Mimi: kama unavyoona, umeniweka sana pale Posta

Mama: jamani pole, kwani ulikua unanisubiri?!

Mimi: Ndio, maana hukusema niondoke! anyway nimeitikia wito bossy wangu, nakusikiliza, what's a deal?

Mama! Ninataka asubuhi uwe unanichukua na mwanangu, lakini mtoto unamwacha pale mikocheni Warioba( hii shule ipo karibu na msikiti wa mwinyi).

Mimi: Sawa mama, sasa mbona hili lilikuwa lakuongea kwenye simu tu na tukamaliza, au ulitaka kuniona??( nilikua nimekazia macho)

Mama: Huku akicheka, unaonekana mpole sana ila ni mwongeaji sana, unavituko sana.

Mimi: Una watoto wangapi?

Mama: Wawili tu, wakwanza wa kike yuko form 5, wapili yuko standard 3, wote wa kike.

Mimi: wow! am luckiest man, huyo wa form 5 nitunzie ntakua mkwe wako.

Mama: utanibakia mwanangu bure!!

Mimi: So unakunywa beer usiku huu, baba watoto akirudi inakuaje??

Mama: Mume namtolea wapi mimi?, naishi na wanangu tu. Unajua wewe haunywi kama unanichora hapa!

Mimi: Hilo tu usijali, siku ntakupeleka Kidimbwi tukanywe wote.

Mama: Huku akicheka, unavituko sana mimi nishachuja tayari huko wanaenda damu mbichi.

Mimi: unaweza kujiona umechuja ila mimi bado nakuona upo hot sana.

"Huyu ni mama wa kichaga mweupe anashepu nzuri, ni mama kijana afu anajipenda sana huyu age yake anavyoonekana ni 40s ni mama kijana.

Mama: huku akicheka, we kaka unavitukoa sana,

Kwa muda tulio kaa na mama nilikua nishamcontol kwa maongezi na kila kitu kama ningetupia voko angeingia king.

Tukakubaliana pale atanilipa 12,000 kwa trip ila nikamwambia nitaanza jumatatu ya week inayokuja, mama hakuwa na shida kabisa.

"Unajua hawa wateja sometimes nilikua nawapa utani ili kuendelea kuwasogeza karibu na awe huru, haipendezi muda wote kuwa kauzu."(Kanuni ni kwamba kama mteja ni mwongeaji na wewe kuwa mwongeaji, kama kauzu na wewe kuwa kauzu, hii ndo iliku principle yangu).

*****

Nikatoka pale na furaha sana, hesabu kichwani ni kumalizana ma Maggy hapo tayari na vichwa 2 na vyote vinakwenda Posta. Ilikua saa 3 usiku tayari nikamtext Maggy, palepale akani text back ni kama alikua anasubiri text yangu. Nikampandia hewani nikamwuliza anakaa Mikocheni gani akanambia karibu na shule ya Alpha. Nikamwambia nitakuwa nampeleka tu ila kurudi kama nitakua around nitakuwa namcheki, hakuwa na noma akakubali, tukakubaliana 10,000.

Mnajua kwanini sikutaka kazi ya kumpeleka na kumrudisha? niliwaza nitakua mtumwa, kwanza utakua na stress upo zako mbweni huko afu sa11 umfuate mteja Posta unakua mtumwa, sikutaka hii kitu kabisa, au jambo lingine muda wa kwenda kazini unaeleweka wakati wa kurudi hauleweki, sikutaka kuchoma mahindi bila sababu ya msingi.

Palepale nikapata idea ya kutengeneza mkataba wa kazi, nikachukua laptop nikadizaini mkataba wangu vizuri kabisa, nikaweka mpaka sehem ya kusaini mwanasheria, sikutaka masikhara na kazi kabisa, na pia nilitaka wateja wanione niko serious.

******

Jumatano ilifika huyo nikaenda Seacliff pale kumchukua Manuel lakini this time alikua yeye na Alex tu, tukasalimiana pale. Tulielekea kwenye hivyo vituo walikua wanafanya research zao na kupiga picha. Tulitembelea vituo vyote tukamaliza kwenye sa11 jioni, nikawarudisha mimi nikaendelea na kazi yangu. Kesho yake tukatembelea vituo vingine ile kazi tuliimaliza jioni pia.

Ijumaa ndo siku ya kwenda kibaha na Bagamoyo, kama kawaida tukaenda huko wakafanya mambo yao hii siku tulirudi usiku sana, nikawadrop pale Seacliff lakini Manuel akaomba tukapate dinner then niondoke, sikukataa tukaelekea Karambezi pale.

Ile tunaingia mlango mkubwa wa kwenda Karambezi nakutana na Ex wangu, Tangu nimemaliza chuo sikuwai onana naye ilikua ishapita miaka 3 na yeye alikua 2nd yr that time, nilikua nimemwacha mwaka 1 mbele.

Yeye ndo aliyeniona akaniita jina langu "INSIDER", Manuel ndo aliyeskia wakati akiniita. Bro somebody is calling you, kucheki namwona Angel (code), wow akaja akanihug kwa nguvu, mpaka Manuel akashangaa!!!

Nilishangaa sana kukutana naye pale ofcourse alikua na rafiki yake afu walikua wakitoka, huyu alikua dem wangu wa chuo enzi hizo baada ya kumaliza chuo aliniacha asee!!, this time tunakutana nimebadilika, nimenawiri,afu niko na wazungu.

Akaomba namba yangu sikutaka kumpa, nikamwambia anipe yake ntamcheki…..

Angel ni mwanamke ambaye nilianza naye mahusiano wakati niko chuo, so wakati wao wanaanza first year mimi ndo nilikutana naye na kuweka ukaribu hatimae tukaanza mahusiano. Tulidumu kwa kipindi chote cha miaka 2, tulipendana sana mpaka masela zangu wa chuo walikua wanaamini huyu mrembo namwoa. Kilichotokea baada ya kumaliza chuo zilianza sababu, mara hapokei simu, ubusy mwingi, nikaanza pata report kutoka kwa masela anaonekana na mwanaume uyo moja kila maeneo, mimi kama mwanaume nikajua hapa sina mtu, nika move on.

********

Tuliagana ma Manuel pale Seacliff ili asubuhi niwai kuwabeba twende misele, ile jumamosi asubuhi by saa 3 nilikua pale. Wakatoka wote hao tukaanza safari plan yetu tuanze na "Ununio beach", Manuel akaomba twende na "Haile Selasie Road" kuna vitu akanunue vya asili. Sehemu yenyewe tuliyokwenda ni karibu na filling station ya Puma au kama unatokea "Samaki samaki" kuna barabara inakunja kulia kama unakwenda CCBRT, sasa kwenye ile kona kushoto kuna supermarket inaitwa "Shrijee", sasa pembeni ya supermarket kuna jamaa wanauzaga vitu vya asili kama, picha, vinyago, kacha nknk.

Manuel aliingia na ndugu zake wakanunua picha, vinyago, kacha kuna vingine waliweka kwenye mfuko vingi. Wakati tunatoka pale akanambia tupitie pale Puma, akamwambia dada ajaze full tank, "nilivyosikia full tank, nilihisi moyo wangu kupasuka kwa furaha", huyu Manuel anaroho nzuri sana, ni moja wa wazungu wenye roho nzuri sana.

Kwenye saa 5 tulikua tuko pale Ununio Beach Ofcoz walipapenda sana na ile mandhari walienjoy sana, mimi ndo nilikua kama director pale. Nakumbuka tulikwenda "Mahaba Beach" kule kulikua kuna samaki wengi sana wabichi, wavuvi ndo kama centre yao, bhs tulichoma sana samaki pale.

Tulitoka pale mchana tunaenda "Coco beach" tukala sana mihogo pale na mishikaki, usiku ilikua imefika muda unagonga kwenye moja kasoro, Manuel akasema twende tukapate dinner moja ya cafe nzuri pale Masaki afu tukamalize bata letu Samaki Samaki. "Wakati tunapita pale samaki samaki asubuhi Manuel alipaona akanambia badae tunakuja hapa".

Nikawadrop wajiandae then tukaenda pale "The tribe" tukapata dinner hao tukamalizia pale Samaki samaki. Kama mnavyojua vibe la Samaki samaki tulienjoy sana lakini hawakukaa sana maana jumapili ndo walikua wanatakiwa kuondoka. Nikawarudisha Seacliff na mimi nikarudi kulala ili asubuhi mapema niwe pale kuwachukua kuwapeleka Airpot.

Naam asubuhi mapema saa 2 na madakika nilikua pale, wao walikua wanatakiwa "kuchek in " pale Airpot 10:00 AM. Nikaingiza gari mle ndani Seacliff karibu na mlango wa kuingilia tukapark vitu hao safari ya Airpot, ndani ya nusu saa tulikua tumefika Termninal 3, hakukua na foleni kabisa.

Tulipiga picha za pamoja pale kama ukumbusho, wale wazungu walifurahi sana, nilipata nafasi ya kuongea na Sophie lakini sikuchukua namba nikaopotezea.

Nikawa escot mpaka ndani pale tunaongea sana na Manuel akanambia "You are my brother here in Tanzania, I'll never stop calling you bro!", alitoa noti 2 za Dolla 100 akanipa, nilimkatalia akanambia "bro hizi pesa sio zako nampa Junior, mfikishie". Pale nikaishiwa pozi ikabidi nipokeee tukapeana hug na mimi nikatoka zangu kurudi parking ili niondoke.

Niseme kwamba kukutana kwangu na Manuel ilikua baraka sana kwani ndani ya week 2 niliingiza pesa nyingi sana na pia niliishi maisha mazuri sana. Nikapiga hesabu ndani ya siku ambazo nimefanya nao kazi nilikua nimeingiza $1,050 na bado alikua ananipa offa za lunch, dinner nknk.

Nikawaza hapa leo niende kwa Mama J nikamsalimie na Junior maana ilikua inakwenda mwezi wa 2 hatujaonana live zaidi ya video call tu. Nikasema hizi pesa nimepewa kwaajili ya junior acha nikanunue baadhi ya mazaga niwapelekee itakayobaki ntampa mama J.

Nikaingia Mlimani city nikanunua baadhi ya vitu nikaelekea boko kwenda kuiona familia yangu, ile nimeingia kwenye gari nikamkumbuka Angel, nikasema ngoja nimpigie maana alionesha anahamu sana ya kuongea na mimi, nikachukua simu ili nimpigie..