Chereads / Ethiopian Hababity!! / Chapter 1 - About Author

Ethiopian Hababity!!

Allib
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 8.5k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - About Author

Ndugu zangu wana webnovel habari zenu.

Unajua kwenye haya maisha tunapitia mengi sana hasa katika utafutaji kwa upande wa Wanaume. Tunakutana na mambo mengi sana ya aibu, kukatishwa tamaa, kuachwa na tuwapendao na mauzauza mengi sana.

Nakumbuka mzee mmoja alinambia mapambano ya kupata maisha mazuri sio rahisi inatakiwa ujasiri, kujitoa na kuwa na maamuzi magumu sana. Kila aliyefanikiwa ana siri nyingi ambazo sio rahisi kushare na mtu mwingine, sometimes tunakutana humu jf, tuna marafiki zetu wote hapa duniani tuna matatizo lakini matatizo yetu yametofautiana.

Mimi INSIDER nimepitia mambo mengi sana kiasi kwamba nilikata tamaa ya maisha...

Na story yangu itaanzia hapa, ilikuaje mpaka nikaingia kwenye biashara ya uber??.

Hii ni story ya kweli na siyo ya kutunga, lengo langu nataka ndugu zangu mpate ujumbe kuhusu haya maisha. Kiufupi usikubali kukata tamaa hata kidogo, no matter what you fall, keep fighting, God has plans for all of us.

Kwa wale ndugu zangu wa Uber/Bolt ambao mnataka kuingia kwenye hii biashara utaweza kupata mwanga mzuri kuhusu hii biashara maana nina experience ya kutosha. Tusichoshane acha nianze kumwaga asalii.....,,