Stela maswaga na maiko chazi ni wapenzi, ilipofika tarehe ya mwezi ule walielekea Newala ambako makaburi ya wazazi wa stela yalikuwepo, na hii ilikuwa kama tamaduni, kila ifikapo tarehe saba ya mwezi wa saba, stela utembelea makaburi ya wazazi wake.
Ni huko New Well neno la kizungu ambalo kiswahili chake ni kisima kipya, sehemu ambayo kwa sasa ujulikana kama Newala.
Safari kuelekea huko ilikua ndefu kiasi chake, kiasi cha kuchukua masulufu kadhaa kwa kujikimu, vitafunwa kama vile soseji, chokleti, karanga zilizokaangwa na kuchanganywa na mayai, bisi, na vinywaji vya kulewesha na visivyolewesha, redbull, safari, kilimanjaro, na vinywaji vingine viongezavyo nguvu, basi charles hakufanya ajizi, begi yake ndiyo iliyotumika kubeba masotojo, marotarota, mapochopocho na masaptasapta hayo, lakini begi ya stela ilikuwa kama meza ya kujirembea iliyobebwa mgongoni, kwani ndani yake kulikuwa na viurembo tu, ving'alisha mitomo, losheni, manukato na kioo cha kujipurua.
Kama si mapenzi yao, kama si jinsi wawili wale kushibana na kuzoweana utazani wamekua pamoja, safari ile ingekuwa ndefu, lakini haikuwa hivo kwa sababu stela na maiko ni watu walio kwenye mapenzi kwa mda mrefu, sio watu wanao tongozana, wamependana tayari, tena wanapendana sana kiasi cha kutamani kuwa karibu muda ote. hawajawahi kuacha kukisi hata wakiwa kwenye gari, na ndoa ilikua njiani mara tu wakisharudi safari ile, bila kujua ugumu ambao wangeenda kutana nao kiasi cha kuchelewa kurudi au wasirudi Masasi kabisa.
"Bebi, Tutarudi lini, !"
"Kesho, tunarudi kesho B",
waliongea wawili wale.
Walipanga kurudi kesho baada tu ya siku kutabasamu.
Walifika Newala, walifika hadi sehemu ambapo stela na wazazi wake waliishi zamani. walifika moja kwa moja hadi makaburini, kaburi moja liliandikwa "Anastansia" bila shaka alikuwa ni mama yake Stela na lingine "Maswaga, ni baba.
Waliisogelea ile nyumba baada ya kumaliza kufagia sehemu ya makaburi, jumba kubwa lililochakaa, jumba ambalo vyumba vyake havina madirisha na milango yake ni ya chuma.
"Mh!!! kwanini hii nyumba haina madirisha na milango yake ni ya chuma?", aliuliza maiko,
"Huku Newala kuna baridi sana wangu, madirisha yangeruhusu baridi kuingia ndani kiurahisi, na hiyo milango ni ya chuma kwa sababu za kimazingira, chuma usaidia kuongeza kiasi cha joto humu ndani na kutunza joto pia" alijibu stela,
"Mh upo vizuri Bebe, kumbe unajua sayansi eeh, "
"ahhahh sio sana bhana, kidogo tu, ni aidia ya kidato cha kwanza au cha pili".
Walipoingia ndani, walishangaa kidogo na kuanza kupasafisha ili wapumzike usiku ule mmoja tu na kesho warejee Masasi, bila kujua mambo yangebadilika.
Baada ya chumba kuwa safi, walibaki kwenye chumba kile kwa mda, chumba ambacho stela alikabidhiwa na baba yake kwa ajili ya kulala, ni chumba cha kulala sio sehemu ya kuhifadhia vikolokolo, tena, ni chumba cha kulala cha mtoto, mtoto wa kike, hakukuwa na nyundo wala chochote chenye ncha ili visije mjeruwi stela, mtoto wa maswaga ambaye alikabidhiwa chumba kile tangu akiwa na umri wa miezi sita.
Kumbe baada ya miezi sita tu, stela alianza kulala peke yake, mama yake alikuja usiku wa manane kwa ajili ya kumpa nyonyo kwa mara ya pili tukihesabu na ile ya kwanza kabla ya kulala, vinginevyo stela alilala peke yake hadi asubuhi labda pale atakapolia usiku hivo mama stela umchukua na kumtenga kwa aja kubwa na au ndogo na kumlaza tena.
Wakiwa katika chumba cha stela cha kulala, stela na maiko hawakuwa hata na chembe ya huzuni, kama sio fraha ni nini basi ningetawala usiku ule ndani ya chumba kile, haikuwa piknik, haikuwa fungate, bali ni siku moja ya kushangaza kwao ambayo wameipata wawili wale, wamefrahi kuwa mbali na nyumbani wakipungwa na upepo mwingine uvumao toka nyanda za juu za makonde.
Stela alikuwa ndani ya vazi la usiku jeupe alilolifunga kwa mikanda kwa nyuma, maiko alitinga kinjunga cheusi kilichokamata vizuri kwenye mapaja yake huku juu akiwa tumbo wazi.
Walikuwa wakicheza muziki wa taratibu ulioskika kutoka kwenye maiki za maskio, ni Nakeyi wimbo wa msanii Ruby kutoka Tanzania.
Walisakata rumba taratibu kwa mtindo wa kuzungukana, ballet, Salsa, au ni Mtindo wa Rok' na Rol, sijuwi ni staili gani, ila walikuwa wakishikana kwa huba huku stepu za stela zilipojaribu kumsogeza nyuma, maiko alimjuta kwa nguvu na kumtuaza taratibu kwenye kifua chake chenye vyumbavyumba.
"Ooh kuna kitu nimekigonga kwa mguu wangu wa kushoto mika"
"Mh, itakua ni nini hicho bebi"
"Sijuwi "
Subiri kwanza niangalie", stela alitoka kifuani mwa chazi maiko na kutizama chini,
"Mamaa!!!, ni funguo chale, kumbe ni funguo"
Kumbe wakati wanajongesha miguu yao, stela aliigonga funguo iliyodondoka toka kwenye kitasa baada ya mlango kugongwa na kutikisika pindi wanadansi. Funguo ilikuwa chini ya mlango , upande bado ilikuwa inaonekana kwa ndani na upande ilikua kwa nje, lakini, sehemu kubwa ya funguo ile ilikuwa kwa nje.