Siku ya tatu ilipoingia, jua lilipanda, kama Stela Maswaga na maiko chazi wangekuwa nje, basi jua lingekuwa linawapiga utosini, lakini hadi mda huo bado walikuwa wamelala, hawajaamka bado.
Sina hakika kama bado wapo hai wawili wale.
Baada ya dakika kadhaa maiko alijitingisha, kumbe bado yupo hai, na stela je, nae akatingishika, kumbe wote wawili walikuwa hai bhana, lakini wamechoka sana, wapo hoi bin taabani.
Kiu na nenge vilizidi kumnyong'onyesha Mika, hakuwa hata na nguvu, kama itafika jioni hawajapata msaada, itabidi wasubiri tu kifo kiwachukue.
Stela aliweza kutoka kitandani, labda ile nadharia ni ya kweli, unene wake unamfanya aendelee kuwa na uwezo wa kusogeza miguu yake hadi sasa. Alipata wazo, uzuri ni kwamba, Stela ni Mbunifu, alichukua ua ambalo alichuma kwenye kaburi la baba yake, akalifinyanga kwa mkono ili walitumie kama chakula.
"Subiri" sauti ya maiko iliskika ikimkataza stela asile kwanza lile ua.
Maiko akaomba aanze kula yeye kwanza, kama lina sumu basi aanze kufa yeye kwanza.
Mwanaume siku zote ni mlizi wa familia, hayupo tayari kuona familia yake inaangamia na yeye akiwepo, ndivyo maiko anavyo tuthibitishia.
Alitafuna yale majani, baada ya kusubiri kwa dakika bila kurudisha chenji, aliona yaweza kuwa halina sumu.
Stela akatafuna yale majani huku akimlisha maiko ambaye alionekana kuchoka mbaya.
Kisha, Stela aligundua kuwa mumewe mtarajiwa amebanwa na kiu, alichukua tambala na kuuviliga ule udongo uliotoka kwenye kopo ambamo lile ua lilipandwa.
Aliukamua ule udongo hadi ulipoanza kudondosha vitone vya maji, alidondosha vile vitone viwili vitatu kwenye mdomo wa maiko.
Stela ajuwi angefanya vile hadi lini, anachohitaji yeye warudi masasi ili wakafunge pingu za maisha na maiko, Stela anamsidia maiko ikiwa na yeye ajuwi kama atatoka mle hai, au atakata kamba, hajuwi msaada utakuja mda gani.
Ilipofika jioni, wote wawili walikuwa hoi kabisa, uchovu na njaa vikawafanya waonekane kama wamelala usingizi.
Bila shaka ule ndio ulikuwa mwisho wa stela na maiko, mwisho wa hadithi yao ya kusisimua, ulishafika mwisho wa hadithi yao ya mapenzi ambayo watoto wa vizazi vingine wangekuja kusimuliwa, hadithi ya wapendanao kama ile ya jaki na rozi wa titaniki au samsoni na delila wa kweli biblia, au romeo na julieti, hayo alikuwa akiyawaza stela akiwa kwenye usingizi mzito.
Usiku ulipokuwa mwingi wakajikuta wamepitiwa na usingizi.
Asubuhi ilifika, ilikuwa ni asubuhi na mapema kiasi cha nje kuwa na mwanga lakini ndani bado kulikuwa na giza, nadhani umeshawaza kwamba itakuwa ni asubuhi ya saa ngapi, kumi na moja au mbili hivi.
Sauti za ndege vipingo waamkao asubuhi kwenda kuishi zimeanza kuskika, ndege ambao maisha yao hakuna asiyeyajua, maisha ya kuokota okota, na uishi ivyo milele, hawalimi lakini wanaishi, mungu mwenyewe ndo anayejua jinsi anavyowapa rikizi, ni ndege weusi wenye ufito mweupe shingoni.
Waliruka huku na huku kuzunguka jumba lile lakini makelele yake hayatoshi kuwaamsha.
Mh! baada ya mda kidogo na mwanga wa jua kuchanua vizuri, Maiko alianza kuhisi kama anapigwa na jua usoni, ni kweli jua lilikuwa linampiga usoni,
"Ni nani anayenimulika taa usoni,? aliwaza maiko akiwa kwenye usingizi mzito hivyo alikuwa anahisi kama yupo ndotoni tu,
"inawezekanaje nipigwe na jua usoni wakati nipo ndani?"
ila ni kweli jua lilikua likimmulika.
Baada ya kupigwa na jua kwa mda mrefu alianza kujitikisa japo alitumia nguvu nyingi angalau kufumbua tu macho maana hakuwa na nguvu.
Alipofumbua macho aliona mlango upo wazi, hakuelewa wala hakuamini anachokiona.
"Mh, au naota"
alijisemea maiko mwenyewe.
Alipata kijinguvu kidogo, kijinguvu kilichotokana na tumaini aliloliona, akainuka huku mchumba wake akiwa amelala bado hana ili wala lile.
Aliapoamka akajaribu kutoka nje, kweli akatoka nje, alikuwa anajaribu kwasababu alikuwa haamini anachokiona.
Alirudi tena ndani na kutoka tena nje, kweli yupo nje,
"Ooh ni kweli, ni kweli tupo nje, tupo nje"
Alimuamsha stela.
Stela aliamka, alishangaa kwa maana hakuelewa imekuaje, maiko akamwambia hata mi sijuwi naona tu mlango umedondoka wenyewe.
"Mungu ametusaidia bebi" alisema mika.
Stela ni mschana mwenye akili sana, pia ni mdadiai hapendi kuyaacha mambo yapite hivi hivi.
Baada ya kuuchunguza ule mlango vizuri akagundua kuwa bawaba zake zilikuwa zimeshaliwa na kutu, pia, namna maiko alivokuwa akiugonga gonga ule mlango kwa mateke na mangumi tangu juzi ilichangia kuudhohofisha, hivo bawaba zilishindwa kuendelea kushikilia mlango ule mzito, ndio maana mlango ukajidondokea wenyewe.
Walikumbatiana, huku wakiangalia namna ya kujikokota hadi seheme ambayo watapata msaada mwingine.
MWISHO.