Chereads / Kisanga / Chapter 3 - Siku ya pili

Chapter 3 - Siku ya pili

Asubuhi na mapema waliamka, maiko alikuwa wa kwanza kuamka.
Alimuangalia mpenzi wake akamuona bado yupo kwenye usingizi mzito juu ya lile godoro kubwa lililowekwa juu ya sakafu nyekundu bila kitanda, maiko akausogelea mlango, akashika kitasa kwa nguvu na kukivuta, haikufaa, akashindwa kujimiliki, akaanza kupigana na mlango kwa kuupiga mangumi na mateke kwa hasira.
Kumbe, Stela alikuwa macho mda ote, na alikuwa akiona jinsi mume wake mtarajiwa anavyoangaika na mlango, alitoka kitandani na kwenda kumkumbata mpenziwe kwa nyuma.
Hakukuwa na namna, mambo yanabadilika kabdri mshare wa saa unavyosogea, jana Maiko alitoa faraja kwa Stela, leo Stela anatoa faraja kwa Maiko ambaye anaonekana kutoka kwenye mstari wa uvumilivu.
Begi ya chakula ilianza kukonda, Kilichobaki ni pepsi moja na biskuti tu!
Waligawana kile kile kidogo walichokuwa nacho, walikunywa ile pepsi kidogo na kuibakiza, walitafuna biskuti kadhaa na zingine kubakiza pia.
Baada ya kufikiri kwa muda, Maiko aliona hamna kifaa chochote cha kuwasaidia mle ndani, ni kama chumba chao wenyewe kinawasaliti, chumba cha stela kinataka kuwaua, ni bora kufa ikiwa haujuwi saa wala siku kuliko kufa ikiwa unajua ni leo au kesho.
Maiko akagundua kuwa zana pekee ambayo anaweza kuitumia ni mwili wake, nguvu zake na uwezo wake kama mtoto wa kiume, lazima awe jembe.
Alipanda kupitia mlango, na kuanza kugonga gonga dali ya kile chumba kwa kutumia kichwa chake na ngumi yake, haikuwa rahisi kuvunja, ile nyumba ilijengwa kizamani sana, tena kikoloni, pale juu ni zege tupu maana hata vumbi halikudondoka.
Alishuka kwa kujidondosha, hoi kitandani huku akiwa na madonda kichwani na mikononi.
Chali kitandani, hakuna namna ya kwenda nje.
Njaa iliwagonga zaidi, wakachukua pepsi na biskuti zilizobaki na kuzimalizia .
Kwahyo, kuanzia dakika ile, vyakula vyote walivyokuja navyo viliisha.
Ilikua ni majira ya saa mbili, bado ni asubuhi sana hadi kupandisha mlima wa masaa yaliyobaki angalau hadi kukata nusu siku ili usiku uingie wapumzishe mwili na akili.
Midomo yao ilianza kukauka kwa kiu na baridi, miili yao ilianza kuchoka kwa njaa, sura zao hazikuwa na nuru tena, zilikuwa chafu zilizojaa vumbi na kutokana na kukaa mda mrefu bila kuoga, zilikuwa nyeusi kama watu waliopakaa masizi.
Stela alichukua kipimajoto chake na kutoa mafuta haina ya gresalini na kuipaka midomo ya maiko iliyokuwa imepasuka kama keki kwa sababu ya baridi, alichukua na losheni yake na kujipaka na yeye pia ili angalau kulainisha ngozi yake.
Hata iweje mwanamke hawezi kusahau urembo, pamoja na matatizo yote waliyonayo, Stela bado anaipenda ngozi yake, ngozi yake ya brown ambayo siku mbili nyuma ilikuwa iking'ara kama jongoo.
Walibaki mle, maskani yao mpya, maskani ambayo yenyewe ndo imewachagua, wao hawakuchagua kuishi mle.
Kwenye maisha kuna mda Mazingira yanatulazimisha kuishi yatakavyo hayo, hivyo sio kila wakati tunaweza kuyaamulu mazingira vile tutakavyo sisi.
Hata hivyo, tatizo sio kuishi kwenye kile chumba kidogo, wataishije? watakula nini?
Baada ya kujaribu kufanya jitihada nyingi lakini bado walinasa, wakakubali chochote kiwakute, kiufupi, walikata tamaa na tamaa ikakatika.
Wakabaki juu ya godoro wakicheza majandimu, mchezo wa kupeana mikono na kupiga makofi kwa kuviziana na atakayepiga makofi peke yake uhesabika ameshindwa.
Giza likafunika tena sura ya dunia, wakalala.