"Okeee tuliza presha Teya, ivute taratibu"
stela alitingisha kichwa kwa hofu, aliinama na kupeleka mkono chini ya mlango.
Maskini stela, aliigonga tena ile funguo kwa kidole chake cha tatu kutoka dole gumba, kidole ambacho ni kirefu kuliko vingine, funguo ikasogea nje zaidi kiasi cha kutoweza kuigusa tena kwa mkono.
"Tutatokaje sasa maikoo!!!"
"Subiri mai, naomba hiyo fimbo hapo kwenye kona ili niivute kwa ndani," alisema maiko.
Stela alichukua fimbo ya ufagio na kumpa maiko, alipojaribu kupitisha chini ya ule mlango, haikuweza kupita,
"Ni nene, ni nene hii, "
Maiko akaipasua ile fimbo kati kati kwa meno yake kisha kuichanua kwa mikono, baada ya ile fimbo kuwa mithiri ya mbao iliyochanwa kwa msumeno, ilifaa, ikapita chini ya mlango, lakini kutokana na wepesi ikavunjika, nayo ikaigonga ile funguo kwa mara ya tatu na kwenda mbali zaidi.
Maiko alichungulia chini ya mlango, hakuamini, funguo ilikuwa mbali, hakuna kitu kingeweza kuivuta tena kuja ndani.
"Duh dadeQ, ila usijali Teya, tutaondoka tu"
"Kweli mika!"
"Yah! si unaniamini!"
"Ndiyo"
"Nikumbatie"
Walikumbatiana huku wakihema, macho ya maiko yakielekea mlangoni, akijaribu kutafuta mbinu nyingine.
Ile ilikuwa ni siku ileile ya kwanza amabyo ndiyo kwanza wameingia ndani ya kile chumba.
Walibaki na tabasamu la kujilazimisha, na fraha ya kujitaftia wenyewe, kila mmoja anaigiza kuwa na fraha, lakini ukiyaangalia macho yao utajua wana uzuni pana na hofu ndefu.
Usiku ulipoingia kimya kilizidi kuwa kizito, hakuna kilichoskika zaidi ya sauti za wadudu, wanyama na ndege, walianza kula azina yao ya chakula.
Wakati wanapata Sabaha, Maiko Chazi alichukua simu yake ili kuomba msaada, angalau simu yake yeye ilikua na asilimia tano, kuliko ile ya mchumba wake ambayo ilizima tangu wakiwa njiani, stela aliitumia simu yake kuchati snap, twita, na kurekodi video pamoja na picha.
Alipojaribu kupiga, mtandao haukuweza kuunganisha mawasiliano yao, labda kwa sababu ya umbali wa sehemu waliopo.
"Hamna mtandao dia"
"Mh! basi piga namba ya dharura"
Sio siri, stela alikuwa mbunifu sana, ndio mwalimu wa mipango, lakini maiko alikiwa mvumilivu, hakuchoka kumpa moyo mpenzi wake. Alipoipigia namba ya dharura simu inatoa taarifa ifuatayo kwa maandishi ya kiingereza "Out of service area".
Walielewa kilichomaanishwa lakini, hawakujua kwa nini.
Maiko alionesha kukasilika kwa mara ya kwanza, aliipasulia mbali ile simu kwa ghadhabu.
Kadri muda unavyozidi kwenda, mawazo yao yanazidi kupoteza uelekeo, wanazidi kuchanganyikiwa, chumba kile kinazidi kuwapa mbinu chache za kujiokoa.
"Bebi, jaribu kutumia hicho kisu"
Maiko alikitazama kile kisu na kujua kabisa hakiwezi kufaa, alipojaribu kupenyeza kwenye tundu la kitasa kile cha mkoloni, kilipita kama aja kwenye shimo la choo, hakikutaka hata kugusana na sehemu yoyote ya kitasa.
"Jaribu hii" alisema stela,
Maiko akajaribu ile funguo ndogo ya gari yake.
"Teya, inazungusha, hii inazungushaa".
"Sawa zungusha taratibu, endelea tu"
"Ooh shenzi! , ni ujinga gani huu!"
"vipi tena bebi" aliuliza Teya, kama maiko anavomuita.
Kipande cha funguo kilidondoka chini tayari, ilikuwa funguo ndogo laini ya gari aina ya i.s.t ambayo imeshindwa kusukuma masinga ya kitasa kile.
Maiko alirudi kitandani, alikaa kwa mda, akamtazama stela kwa huruma huku macho yake yakilengwa na machozi.
Ukweli ni kwamba, binaadamu tunaishi kutokana na vyakula na vinyaji tunavoingiza mwilini mwetu kila sku, chakula ambacho kikishaingia katika miili yetu ugeuzwa kuwa nguvu.
Hata hivyo, hakuna majibu ya moja kwa moja ya kuwa ni siku ngapi binaadamu anaweza kuishi bila kuingiza kitu chochote tumboni, hii ni kutokana na utofauti tulionao, wengine ni matukunyema na wengine ni vimbaombao.
Kadri mnene ulivyo ndivyo unauwezo wa kuishi siku nyingi bila kula na kadri mwembamba ulivyo ndivyo siku chache unaweza kuishi, je, wataishije wawili wale ndani ya chumba kile pindi chakula kitakapo kwisha?. Naskitika kusema, Stela ni mnene kuliko mpenzi wake Maiko, hivyo napatwa na huzuni pia kusema huwenda Maiko atakata kamba mapema zaidi kuliko Stela.
"Bebi tutafia hapaa.."
"Mi staki kufia hapaa, nataka nikafie nyumbani kisha ndo nije kuzikwa huku, staki kufa kizembe hivi, nataka kufa kishujaa nikipambania nchi yangu, nataka kufa vitani mimi" stela aliendelea kulia.
"Uwezi kufa, labda mi nife we ubaki, kama itabidi tufie hapa, mi nitakua wa kwanza kufa maana mi ni mwembamba, mwili wangu hauna mafuta, baada ya siku tatu tu nitashindwa kuinua hata kope zangu, hata kidole changu cha mwisho sitoweza kukitikisa" alijibu chazi maiko.
Aliendelea, "Hata hivyo hatuwezi kufa hapa, lazima turudi Masasi, lazima tutafute namna ya kutoka humu.
Siku ilikasilika tayari kwani kiza kilikwisha kuingia, kile chumba kisichokuwa na taa wala dirisha kilikuwa na giza, macho yao tu ndiyo yaliyoweza kuonekana.
Walilala.