Chapter 210 - RIAN

Edrian akaweka mazingira ya chumba chake vyema kisha akatoa kwenye begi lake kompyuta mpakato na kuiweka mezani kisha akafungua na kusoma barua pepe!

Dakika kumi na tano zikapita na bado Aretha hakuwa ametoka bafuni, akapata wasi wasi, akainuka na kusogea kwenye mlango huku akisikiliza kama kuna dalili za maji kumwagika, lakini palikuwa kimya. Ed akajiuliza iwapo agonge au aache. Akarudi pasipo kugonga.

Akarudi tena kwenye kompyuta yake, akiamini huenda ni hofu isiyokuwa na maana. Akaangalia mabadiliko ya soko la vito vya thamani, wanunuzi wakuu wa SGC wakionesha kupungua. Akakuna kichwa akifikiri nini hasa ni changamoto. Akashtuka na kuangalia saa yake sasa dakika kumi na tano nyingine zilipita, akainuka na kusogelea mlango akagonga huku akiita lakini Aretha hakuitika.

"Retha nakuja huko sasa" akaamua kuingia kwa wasi wasi mwingi uliomshika. Akasukuma mlango taratibu na kuchungulia ndani lakini Aretha hakuwapo sehemu ya kwanza. Akaita tena huku akivuta mlango ule wa kioo pasipo kuchungulia akaita lakini hakuitika, akaingia Aretha hakuwapo. Sasa ilibakia sehemu moja ya mwisho kabla ya kuita akamsikia mapovu ya sabuni yakifurumia.. akaita lakini hakuitika, Ed akavuta ile pazia ya plastiki kwa haraka na kuangalia kwa kuhofia usalama wa Aretha...

Edrian akabaki akitabasamu kwani mtu aliyemhofia alikuwa kwenye sinki la kuogea huku akiwa amepitiwa na usingizi. Alipoyagusa maji, yalikuwa vuguvugu, akaogopa

"Retha" akamuita akiinama usawa wa uso wake, Aretha akafumbua macho ambayo bado hakuweza kumtazama vyema Ed sababu ya usingizi mzito aliokuwa nao!

Akainua mkono na kumshika Ed usoni huku akitabasamu akafungua kinywa kutaka kusema kusema lakini maneno hayakutoka zaidi akarudi kulala

"Umhhh" akashusha pumzi, akimwangalia Aretha ambaye mwili wake ulifunikwa na povu la sabuni harufu safi ya vanilla ilijaa mle bafuni.

Edrian akamwangalia kisha akatoka na kuchukua taulo, akawaza amfuate Coletha lakini akalitupilia mbali wazo hilo, akamuinua kutoka kwenye maji huku akizungusha ile taulo kubwa kuanzia kifuani.. akamuinua kwa kumweka begani!

Akamfikishia kitandani huku Aretha akijikunyata asijue kinachoendelea lakini Ed alisikia maneno aliyosema huku akikunja miguu yake "I love you Rian"

Edrian akachukua shuka akamfunika kisha akaivuta ile taulo. Wakati huo Aretha akageuka tena na kufanya shuka ifunuke, sehemu ya mapaja yake ikawa wazi, kwa haraka Edrian akamfunika kisha akasimama pembeni ya kitanda huku akihema kwa nguvu. Alipoona akili yake ni kama ilianza kupoteza utulivu akabeba ile taulo na kuelekea bafuni kwa haraka, akafungua maji ya baridi yakamdondokea mwilini mwake. Alipojitazama chini akabana midomo yake na kuendelea kusimama kwenye maji yale kutoka bomba la juu.

Baada ya dakika ishirini, Ed akajisikia vyema, akavuta taulo na kujifuta kisha akatoka ili kuchukua nguo nyingine ya kulalia. Akakumbuka mdogo wake Coletha akachukua simu na kupiga. Simu ikaita muda mrefu lakini haikupokelewa.

"Atakuwa amelala nini!" Akaamua kumtumia ujumbe akimwambia alale tu kwa kuwa Aretha angelala kwake.

KIsha akaelekea kwenye kochi akaamua kulala hapo. Akamwangalia Aretha aliyelala kwa amani akatabasamu na kuchukua mto na shuka kisha akajifunika. Ilimlazimu kukunja sana miguu yake sababu kochi lilikuwa fupi kwa yeye kulala.

Asingeweza kulala kwenye kochi lile

kwa muda mrefu! Edrian akainuka na kuangalia kitanda chake ambacho kwa ukubwa wake bado Aretha alilalia sehemu ndogo sana. Akamuangalia Aretha aliyelala akiwa amejikunyata, akaamua kulala upande mkubwa wa kitanda uliobaki! Akakumbuka hakumvika nguo Aretha, akaamua kumvisha kabla ya kulala.....

Alipomaliza akashusha pumzi na kuamua kuelekea ofisini kwake ili kupata utulivu.

****************

Aretha alikuwa wa kwanza kushtuka kutoka usingizi akajaribu kujinyoosha lakini hakuweza maana mikono yenye nguvu ilimkumbatia akashtuka. Akafumbua macho akakutana na kifua kikiwa mbele yake.. akili yake ikafanya kazi haraka akainua kichwa chake kumwangalia usoni, "Rian" akasema taratibu

Akajitazama alikuwa amejifunika shuka ila ilikuwa tofauti na ile aliyojifunika Ed.