Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 147 - TENDO JEMA

Chapter 147 - TENDO JEMA

Edrian alirudi nyumbani majira ya usiku sana akitokea ofisini. Linus alikuwa pamoja nae. Wote walionekana kuchoka lakini nyuso zao zilikuwa na tumaini. Walimaliza maandalizi yote ya Mkutano wa Bodi ambao ungefanyika kwenye jengo la Ashanti.

"Usiku mwema bro" Li akamuaga kaka yake mara walipoingia ndani, akielekea chumbani kwake...

"Sawa. Na kwako pia" Edrian akaelekea chumbani kwake.

Mara alipoingia chumbani akakumbuka ujumbe wa Aretha ambao alimtumia baada ya kushindwa kupokea simu, alimtumia ujumbe mfupi angemtafuta mara baada ya kumaliza kikao kifupi walichokuwa nacho na 4D.

"Ooooh sorry princess" akasema mara alipokumbuka. Akaweka begi lake ndogo mezani kisha akaketi kwenye kochi lake pembeni kidogo ya kitanda. Akapiga simu huku akisali Aretha apokee.

Simu ikaita upande wa pili na sala yake ikawa imesikika maana ilipokelewa mara moja.

"Hello Rian" Aretha upande wa pili akaitika..

"Uko macho hadi sasa princess?" Akauliza Edrian japokuwa alifurahi kuwa simu yake ilipokelewa maana kama Aretha angekuwa amelala asingepata nafasi ya kumsikia.

"Aaah.. . ndio, je umefanikiwa kumaliza Rian?" Aretha akauliza kwa haraka na katika sauti yenye kujali

"Nimemaliza kabisa. Hakuna kilichosalia" akamjibu na kuendelea kuuliza

"Mambo yameendaje kwa upande wako?"

"Aaaah yameenda vizuri, Beruya amesema picha zitawekwa usiku wa kuamkia jumapili"

"Eeeh kwa nini usiku wote huo ina maana na wewe utatakiwa kuwepo?" Sauti ya Ed sasa ilibeba mashaka

"Ni utaratibu maana ukumbi utabaki umefungwa mpaka muda wa onesho." Aretha akamuelezea lakini bado Edrian hakupenda wazo la usiku ikabidi tu aridhie

Edrian akaendelea kumsikiliza Aretha ambaye alionekana kuwa na shauku na onesho lile.

"Rian" Aretha akamuita baada ya kuona amenyamaza

"Aaahmmm" akaitika Edrian

"Kuhusu hiyo kesho usiku, unaweza kuongea na Derrick anipeleke?"

Edrian ambaye alikuwa akimsikiliza Aretha muda ule wote, aliposikia Aretha akimsihi akaachia tabasamu na kisha akasema, "Kwa nini hujaniomba mimi nikupeleke Retha?"

"Eeehm!!" akashtuka Aretha

"Kwa nini unataka Derrick na sio mimi eeeeh?"

"Oooh no, unajua Rian utakuwa umechoka na ra_?"

"Retha, unanisemea mimi au unaweka makisio yako kwangu?" Edrian akamkatisha huku akitabasamu maana alijua kwa kiasi gani alimbana Aretha kwenye kona

"Aaaaahm!! Hapana ..lakini Rian ni vizuri pia nawe ukawa na_"

"Ni vizuri niwe na wewe usiku huo. Nawezaje kujiaminisha kuwa uko salama halafu nikalala?" Edrian akaendelea na uchokozi wake

"Rian...please usifikiri mimi nitakuwa hatarini wakati niko na Derrick" Aretha akajitetea

"Aretha Thomas utanisubiri, nitakuchukua na kukurudisha, kuna shida yoyote nikifanya hivyo princess?" Akauliza huku akiweka tabasamu la kichokozi usoni

"Aaamhhhm...sawa Rian. Sina shida kabisa ni vile niliwaza ungehitaji kupumzika. Nimekubali utakuja kunichukua" Aretha akaona ajisalimishe tu maana alijua Edrian hawezi kumruhusu na hasa kwa usiku.

"Mama amesemaje?" Akaendelea, "ulimtaarifu?"

"Ndio nimemwambia amekubali, alisema atakutafuta akuulize kitu"

"Eeeeh?" Edrian akashtuka

"Rian....atakuuliza kama utakuwepo au la huna haja ya kushtuka!" Akamwambia

"Hahaha kawaida kumbe...hata mama anajua ni tendo jema kukusindikiza!! Edrian akacheka taratibu.

Maongezi yao yakaendelea hakuna aliyetaka kukata simu japo wote walionekana kuchoka. Edrian alipoangalia saa akaamua awe wa kwanza kukata simu ili Aretha awahi kulala japokuwa alitamani kuendelea kuisikia sauti yake,

"Retha, nafikiri ni muda mzuri wa kupumzika. Una safari ndefu ya kuwa macho kesho usiku"

"Na wewe je Rian?, ulale kesho ni siku ndefu kwako!" Akamkumbusha kwa sauti ya kujali

"Aaahhh kawaida princess, mimi naweza kuwa macho hata siku mbili. Basi tulale mpenzi."

Ilikuwa ni bandika bandua ya mazungumzo mpaka walipoafikiana kulala baada ya Edrian kukumbuka alihitaji kuoga kabla ya kulala. Akarudisha simu na kujiandaa kuelekea bafuni. Maji ya baridi yalipomgusa ngozi ya mwili wake alisikia ahueni.

"Maongezi yalikuwa ya kawaida lakini joto si la kawaida hili" akawaza Edrian alipoyaacha nani yaendelee kutiririka.