Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

LAIVILANI:amani ya moyo

🇹🇿Bahati_Idd_Rigambo
--
chs / week
--
NOT RATINGS
3.4k
Views
Synopsis
nani alidhani kwamba atapitia kwenye maumivu makali sababu ya upofu wake?...
VIEW MORE

Chapter 1 - kuzaliwa

Ulikuwa ni usiku wenye mvua na baridi Kali sana.Ndani ya jumba kubwa la kifahari anaonekana mwanadada aitwaye Dora akiwa amebeba watoto wawili (wakike )ambapo ni mapacha ila mmoja alikuwa kipofu na alijifungua muda mchache uliopita.mbele yake alisimama mumewe aitwaye Bryson akiwa amekamata kisu chenye ncha Kali na kumueleza Dora

"Nipatie huyo mtoto aliye laaniwa haraka!umethubutuje kunizalia kipofu Mimi?"

Dora alimtazama mumewe huku akitokwa na machozi kisha akamjibu kwa ujasiri

"Sikupatii huyu mtoto kheri tuachane tu kuliko kukubali mwanangu auawe.umeelewa"

"Kimyaaa!!!hii ni laana katika ukoo wetu!isitoshe nitachekwa ikigundulika kuwa Nina mtoto kipofu Mimi!"

"Basi sawa Mimi naondoka ili upate heshima unayolilia lakini mtoto ni mtoto tu!naelewa hahuwezi kuelewa uchungu wa mtoto na hauto elewa

Kwaheri naondoka na wanangu"

Dora alimpita mumewe na kutoka taratibu mule ndani usiku huo huo.Alilisogelea gari na kuingia tayari kwa kuondoka ila kabla hajawasha gari aliitwa na mumewe .Dora akamtazama na kumpa ishara aongee.

"Rudi ndani na watoto nimeridhia wabaki hapa mbaka huyo kipofu.Nitawalea wrote bila upendeleo wa aina yoyote!Usiondoke tafadhali."

"Kweli Bryson?"

"Ndio mke wangu,rudi ndani"

Dora akatabasamu na kuteremka na wanae wote wawili.Bryson alimkobatia mkewe lakini moyoni akajisemea

"Nyoo kamwe siwezi kukubali huyo kipofu aishi ndani ya nyumba yangu labda kama Mimi sio Bryson. Hahahaha!"

Akamshika Dora na kumuingiza ndani.

Siku iliyofuata Bryson aliita mbatizaji kwa ajili ya kuwapa watoto majina.Chap kwa haraka mchungaji aliwasili tayari kwa zoezi hilo ambapo alianza na mtoto ambaye sio kipofu

"Huyu ataitwa...."

Watu wote walitega sikio kusikiliza jina la mtoto.

"Laixilani!"

Watu wote wakatabasamu kwa furahana kushangilia.Zamu ya mtoto kipofu ikafika ambapo mchungaji aliomba mtoto aletwe

"Hapana hawezi kubatizwa huyu maana hana muda mrefu!"

Bryson alitamka jambo ambalo lilishangaza watu wote hasa mama wa watoto,Dora