Chereads / LAIVILANI:amani ya moyo / Chapter 3 - ninii????

Chapter 3 - ninii????

"Dora!Dora !Dora !"

Aliita sana Mariam lakini tayari gari lilifika mbali .Akarudi mpaka chumbani kwake na kuchukua simu kumpigia Dora lakini mara ghafla akagundua kuwa simu ya Dora inaitia mule mule ndani .Kwa bahati mbaya Dora alisahau kubeba simu.Mariam alilegea baada ya kushindwa kuwasiliana na Dora .Alichofanya tena ni kurudi kwenye chumba cha watoto ambapo akamkuta Laixilani akiwa bado amelala,alipogeuka tu alimuona Ema akiwa anachimba shimo.pembeni akamuona Laivilani akiwa analia kutokana na kupigwa na baridi la nje.

Haraka Mariam alitoka nje akitaka kumfuata Esma.

" Esma una..."

Alikatiza kuongea baada ya kutomkuta Esma pale alipomuona .Aligeuka kila sehemu lakini wala hakumuona.Akasogea porini zaidi na kufanikiwa kumuona Esma akiwa amesimama na pembeni alikuwa amesimama Bryson.Maria akashtuka...

Kwa upande wa Dora naye akarudi kwake maana alikumbuka kuwa amesahau simu .Alielekea mpaka chumbani kwake na kwa bahati nzuri aliikuta simu yake kitandani.

"Mmmh mbona missed calls ni nyingi hivi alafu zote ni za Mariam ?"

Akajiuliza Dora baada ya kufungua simu na kuziona.akatoka nje na kwenda kwenye chumba alichowalaza watoto na kuingia ndani.Alisogea karibu ya viwanda lakini ghafla alishtuka baada ya kukuta mtoto mmoja hayupo.

Dora akachanganyikiwa ghafla.Hapo akili ikamjia kuwa huenda Mariam alitaka kumuambia kuhusu mtoto kuibiwa.

Taratibu akatoka huku akimpigia simu Mariam.Akiwa anafanya vile,ghafla akakutana na mumewe mbele tena akiwa amebeba nguo yenye damu nyingi.

"Bryson nini kimetokea ?mbona simuoni Laivi wangu"

"Mariam....."

"Mariam !kafanyaje Mariam ?"

"Kamuiba Laivi wetu alafu kakimbia "

"Ninii!!!!!!?"

Pale pale Dora akapoteza fahamu

Bryson akambeba mkewe haraka na kumkimbiza hospitalini