wwww
Endeleaa...pale alikuwepo mama yake Bryson mwenyewe hivyo alimsogelea mwanae ambaye ni Bryson na kumueleza
"Bryson kijana wangu,mpeleke tu mtoto apewe jina,hata kama unachuki binafsi sio vizuri kuonyesha hadharani hivi"
Bryson akamtazama mama yake na kukubali.
Akampeleka mtoto kwa mbatizaji.mbatizaji akatabasamu na kutoa jina
"Huyu ataitwa Laivilani"
Mbatizaji alisema.Watu wote walifurahi isipokuwa Bryson ambaye aliamua kuondoka kabisaa..basi baada ya tukio lile watu wote walirudi majumbani kwao.Laixilani na Laivilani walikuwa wamelazwa ndani ya chumba chao.Kwa Bryson alimuita kijakazi wa pili wa mke wake aitwaye Esma na kumuagiza kumuua Laivilani haraka iwezekanavyo
"Sawa boss nitafanya hivyo bila kufahamika na yeyote!"
Alihakikisha Esma na kutoka kuelekea chumbani kwa watoto.Alipowasili alimnyanyua Laivilani taratibu lakini kabla hajatoka alisikia sauti ya mtu kuja maeneo yale.Haraka akamrudisha Laivilani na kwenda kujificha nyuma ya pazia huku akiomba mungu asionekane.Aliyekuwa anaingia ni Mariamu (kijakazi mkuu wa Dora),alipoingia tu alisogelea kitanda cha watoto lakini aligundua Laivilani amelala vibaya tofauti na mwanZo hata shuka alilo mfunika halikuwepo tena mwilini.Hakushtuka sana hivyo alimfunika tena na kisha akatoka nje lakini alijibanza pembeni ya ukuta
"Lazima kuna mtu humo sasa subiri"
Alijisemea Mariamu.Ndani Esma alijua kuwa Mariamu ameondoka kuwa sivyo.Akamnyanyua Laivilani na kutazama pande zote bila kuona mtu,haraka akakimbia na mtoto!
" eeh anampeleka wapi huyu mtoto?lazima nikamwambie Dora ukweli"
Mariamu alisema hivyo kisha akatoka mbio kuelekea alipo Dora.Dora kwa muda huo alikuwa anajiandaa kwa ajili ya kwenda hospital maana alidai kichwa kinamuuma.Mariamu naye alikuwa spidi kumfuata Dora amueleze kuwa mtoto kaibiwa.
Kwamuda huo tayari Dora alimaliza kujiandaa na kutoka mule chumbani.Ile anatoka tu ndani,Mariamu naye ndio anawasili mlangoni.
"Madam Dora fungua mlango tafadhali"
Aliita