Chereads / MFALME WA KESHO / Chapter 4 - malaika asiye na huruma hata kidogo

Chapter 4 - malaika asiye na huruma hata kidogo

"Nataka kumuona akiwa amekufa!!"

"Alicia...."kabla Mesel hajasema neno,Alicia akaachia mshale!Nora akiwa katikati ya mawazo,akashtukia mshale umemchoma kifuani mwake..hajakaa sawa,Alicia akaachia mshale mwengine tena.

"Kwanini umefanya hivi Alicia!!!!"

Mesel akafoka.Hakuelewa hasa kwanini

"Ujue unachofanya adhabu yake ni kifo!!!"

Alicia akamgeukia Mesel kisha akaruka kutoka juu ya farasi.

"Walinzi!!!!!"

akaita na haraka walinzi wakaja.

"Nendeni mukammalizie yule mjinga!"

"Sawa malkia." walinzi wakamsogelea Nora ambaye alilegea mno na kumtazama.

"Alicia kwaninï?"

Mesel akauliza kwa upole kidogo

"Huyu ni prince kutokea Animas na ndiye aliyevamia ngome yetu.Yeye na kaka yake wameharibu furaha yetu.Nataka wafe leo!"

Alicia akasema kwa ukali.Akaachia mshale mwingine tena.

"Alicia achaa!"

"Funga mdomo Mesel!"

Walinzi wakamsogelea Nora ambaye alikua amelegea kupitiliza.

"Nimekuja kwa amani jamani..kwanini munataka kuniuwa?"

akauliza Nora kwa tabu mno.Walinzi wakacheka kwa dharau

"Uwa!!" wakavuta hasira lakini kabla hata g?awajafanikiwa kumkata...kuna mtu akaingilia tena mwanamke.Sura yake aliifunga kitambaa cheupe ili asionekane na kuanza kupambana na wale walinzi.

"Huyu nani tena?" Alicia akajiuliza kwa namna ambavyo yule mwanamke alikuwa fundi wa kutumia upanga.Mwisho akawamaliza wale walinzi na kumsogelea Nora alafu akampapasa kuhakikisha kama yupo hai ama la.Alicia akakamata upanga na kumfuata yuld mwanamke kwa hasira.Bado yule mwanamke hakutaka kumruhusu Alicia amfikie Nora.Akafanikiwa kumsukuma mbali kisha akambeba Nora na kuondoka naye.

"Huyu mwanamke mbona kama namkumbuka kwenye kumbukumbu zangu za utotoni??"

Alicia akajiwazia

taarifa za kupotea kwa Nora zikamfikia mfalme Blooden sasa.....