Chereads / MFALME WA KESHO / Chapter 9 - Muda baada ya muda

Chapter 9 - Muda baada ya muda

Ecca akabaki kuutazama mkono wake tu.Akajilaza tu kitandani na punde usingizi ukampitia.

Asubuhi na mapema sasa,Ecca akaamka baada ya kuhisi maumivu makali hivi na kama mkono wake unavuta.Kiuchovu akaamka na kuutazama mkono wake.

"Ah!" Akashangaa baada ya kuona mkono wake ukiwa unavuja damu mno alafu jeraha likawa linaongezeka muda baada ya muda.Kwa uoga akasimama na kuutazama mkono kwa makini.Haraka akaelekea bafuni kukiosha kidonda chake ingawa alikuwa akipata maumivu makali mno.

Akaamua kutengeneza dawa ili ajifanyie matibabu.Kadri muda ulivyokuwa unasogea mbele ndivyo kidonda kikawa kinazidi kukuwa.

~........~

Alicia alikuwa dirishani akitazama mazingira kwa mbali.Akiwa pale,akaja Mesel na kusimama pembeni yake.

"Hapa ni wapi Mesel?" Akauliza Alicia akimtazama Mesel.Mazingira yalikuwa tofauti na pale walipolala awali.Ni kama walikuwa mjini vile.

"Hapa ni kwangu sasa."Akajibu Mesel na kumfanya Alicia ashangae.

"Tumefikaje hapa?Mbona unanishangaza sasa?"

"Napenda kukushangaza." Akajibu Mesel akitabasamu.Huyu mwanaume huyu ana nini jamani?Alicia akameza mate tu na kumtazama tena.

"Aah.....aya sawa.Naweza kwenda kuangalia?"Akauliza Alicia.

"Sitaki kujua kuangalia nini,we nenda tu"

"Asante."Alicia akakimbia na kwenda nje na alipokuwa.

"Pazuri jamani." Akasifia Alicia akiendelea kupita maeneo mbali mbali.Ghafla akasikia sauti za watu kuongea ndani ya chumba fulani.

Kwa mwendo wa taratibu ajausogelea mlango na kutega sikio.Hakuna kitu alichokielewa hivyo akaamua tu kufungua mlango asikie vizuri maongezi hayo ambayo ameyavamia.Walikuwa wanawake wawili ndani ya chumba hicho wanaongea.Mmoja alionekana kuwa kama malikia na mwengine kijakazi.

Baada ya kumuona Alicia,wote wakaacha kuongea na kumtazama.

"Samahani kwa kuingilia maongezi yenu jamani." Akaomba radhi Alicia.

"Bila samahani.Kwani watakaje?" Akauliza Isabel yule kijakazi.

"Hakuna kitu,nilikuwa naangalia angalia tu mazingira."

"Inaonekana wewe ni mgeni hapa sio?"

"Ndiyo.Ni mara yangu ya kwanza kuja hapa."

"Unatokea wapi?"

"Atlas."

"Atlas!Hiyo ngome si ilipigwa vibaya sana?"

Alicia kaamua kuondoka bila kujibu lolote.Ghafla wakasikia mlio wa ngoma ambao ulimaanisha wakusanyike kwenye baraza kuu haraka sana.