Ah!" Nora akashika kichwa chake kwa maumivu makali.Sauti hiyo ikamstua Ecca na kuamka kumtazama.
'"uko sawa wewe?"
akauliza Ecca akiinuka kuisogelea glasi ya maji.Akamimina maji na kumpa Nora anywe.
"nimekujaje hapa?" akauliza Nora akizifungua bandage alizofungwa.
"hapana,usizitoe prince.kidonda kitaanza upya"
Ecca akazuia lakini Nora akamshika mkono na kumsogeza karibu yake.Wakawa wanashea pumzi zao.
"wewe ni nani hasa Ecca?"
akauliza kwa sauti isiyo na utani ndani yakr hata kidogo.
"mimi Ecca ila yule mwanamke aliyekushambulia ni malaika asiye na hu
ruma hata kidogo."
"sio jibu la swali langu."
akasema Nora kwa hasira.
"laki...laki...lakini..."
ghafla Ecca akapoteza fahamu pale pale na kudondokea kifuani kwa Nora.
"Wewe!Wewe!"
Nora akaita na kumtazama Ecca,hapo akagundua kuwa ameumia maeneo ya mgongoni.
Nora akayatazama majeraha yake na pale pale yakajifunga.Akamsogelea Ecca na kuweka mikono yake juu ta jeraha la Ecca.Pale pale yakajiponesha.Akatabasamu na kunyanyuka kutoka pale haraka.
~muda baadae~
Ecca ndio akapata fahamu baada ya kuzimia na kujikuta kwenye mazingira tofauti na ya mwanzo.
"Dada unaniona?"
Scan akauliza na kumfanya Ecca amtazame kwa makini.
"Nani amenileta hapa?"
akauliza baada ya kuona mazingira ni mazuri mno.Scan akasogea mezani na kuchukua barua kisha akampa Ecca ausome
"Sawa nimeuelewa."
"amesemaje?"
"hii nyumba ametupa Nora na atakuja leo usiku nimsomee angalau kitabu.Bora tu alale pia."
Akasema na kumfanya mdogo wake ashangae.
"dada huogopi?"
"kalale Scan."
Scan hakubisha.akaenda kulala ingawa kinyonge.
Alicia na mumewe nao wakaaga na kuanza safari ya kwenda kwa ufalme wa Mesel ulio mbali kidogo.
Safari ilikuwa ndefu mpaka giza likatanda.
"Uko sawa wewe?" akauliza Mesel baada ya kumuona Alicia akihema kivivu na kiuchovu.
"nimechoka sana.nahitaji kupumzika."
akasema
"sawa subiri...simamisha msafara!!!"
akaagiza na haraka msafaara ukasimamishwa.Mazingira yakaandaliwa kwa kupumzika viongozi hao.
Ecca sasa akaandika barua kumtaarifu Nora kuwa aje maana muda tayari uliwadia.Baada ya kumaliza kuandika akampa ndege mpeleka ujumbe ambaye akapaa mpaka kwe kasri kuu na kutua dirishani kwa Nora.Kwa bahati mbaya Nora alikuwa bafunina chumbani alikuwa kaka yake ,prince Alexander.Alexander akainuka baada ya kumuona yule ndege na kumsogelea kisha akachukua ule ujumbe .Taratibu akaufungua na kuusoma kisha akaurudisha kwa yule ndege.
"mpuuzi sana." akasema na kutoka mule ndani kwa hasira.Nora alipo maliza kuoga na kurudi chumbani akakutana na ule ujumbe.Akausoma na kutabasamu tu