Chereads / MFALME WA KESHO / Chapter 1 - ulazima

MFALME WA KESHO

🇹🇿Bahati_Idd_Rigambo
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 13k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - ulazima

MRAIBU KWAKO WEWEMraibu kwako wewe:ulazima

Bahari ilikuwa tulivu mno siku hiyo na kufanya usafiri wa maji uwetnjia salama sana.Siku hiyo...meli ya usafiri ya kifalme ya Atlas ilikuwa ikisafiri kupitia bahari kupeleka mizigo na vyakula kwenye ngome ya kiarabu ya alchoraz

Wakiwa katikati ya bahari ghafla lïkaibuka joka kubwa jeusi lenye mdpembe kutoka majini na kuizunguka meli iĺe yote.Watu wote waliopo ndani ya meli wakaanza kupata uoga na kulia.joka lile likaachama mdomo na kuimeza iĺe meli yote na na watu wake

Upande wa ufalme wa Angalan wenye asili ya i misri,anaonekana yule joka akiibuka majini na baada ya kuibuka tu akapiga kelele.punde sauti ya vîkuku ikasikika kuja madneo yaĺe na hapo akaja mwanamke aliyevalia nguo nyeusi .juu kiblazia na chinï sketi nyeusi yenye mpasuo karibia kiunoni.cheni za almasi zilizatawala mwilini .ni mwanamke mzuri mno kuwah kutokea duniani mwenye miaka 20-22

Jina lake ni Zebrana mtoto wa mwisho wa firauni Hadas.

Uzuri wake haukuwah kumpata mshindani lakini tatizo na kasoro kubwa ni roho mbaya..mtoto alirith roho mbaza sana

Mbali na huko,kwenye ngome nyingine kubwa ya kizungu ndoa ya kijana wa kwanza na wa kipekee wa mfalme,Setaph ambaye ni Mesel alikuwa akipata mke kutokea ngome jirani ambapo ndoa hiyo ilikua ni ya mpango tu yaan ili kuunganisha nguvu maana ngome ya mrembo Alicia ilipata kipigo kikali kutokea ngome ya Animas.

Wala hakukuwa na mapenzi kati yao.ukumbini sasa anaonekana mrembo Alicia akiwa anaingia taratibu huku akiwa amevalia gauni kubwa la rangi ya udongo.uso wake ulifunikwa kwa kitambaa kizuri cha kuangaza.Mesel akamsogelea Alicia na kumshika mkono alafu akasogea naye mbele taratibu alipo padri.

"Nyote muinue vichwa vyenu kumtzama kila mmoja wenu"

Padri mkuu akawaagiza na haraka wote wakatii.

"Prince Mesel mtazame mkeo mtarajiwa kwa kumfunua kitambaa "

Akasema padri na haraka Mesel akatii lakini Alicia wala hakuthubutu kumtazama Mesel."Hebu miangalie Alicia " akasema Merel kibabekidogo na kumfanya Alicia amtazame ingawa kwa aibu.Hata hivyo...Alicia hakufanikiwa kuiona sura ya Mesel maana alivaa mask.

"Alicia nawe mtazame mumeo" akasema padri na kumfanya Alicia amtazame tena Mesel.

"Mbona umevaa mask sasa ?" akauliza Alicia kwa mshangao mkubwa mno.Mesel akatabasamu na kuinama kumtazama Alicia kwa ukaribu zaidi .

"Nataka kukufanya ushangae zaidi na zaidi Alicia ,huu ni mwanzo tu ,mengi yatafuata ."

Akasema Mesel kisha...akatabasamu na kurudi nyuma .Alicia akabaki kimya tu.Pete zikaletwa ambpapo maharusi wakaveshana .

"Alicia umekubali kuolewa na mimi ?"

Akauliza Mesel lakini mawazo ya Alicia haykua pale hata kidogo.

"Alicia ..." mama yake akamshtua

"Ndiyo nimekubali kuolewa"

Akakubali ingawa alikuwa akiumia moyoni .

"Nyie ni mke na mume kuanzia saSa"

Padri akatangaza rasmi.

MRAIBU KWAKO WEWE

Animas sasa.....siku hiyo kwenye kasri paliandaliwa kalamu kwaajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya kijana wa pili wa mfalme Li Shi,Nora akitimiza umri wa miaka 27.Asilimia kubwa ya wanawake walikuwa wakimtamani mno Nora kutokana na nguvu na uzuri wake.Licha ya hivyo hakuna mwanamke yeyote aliyepata nafasi ya kukaa na Nora hata kwa sekunde .Mfalme pia alikuwa akimpenda Nora sababu ya nguvu za ajabu alizokuwa nazo .Burudani kubwa ya Nora ni kuimbiwa ,anapenda sana kuimbiwa na alitamani sana kumpata mwanamke wa kumtuliza masikio yake.Akaamua aende kuwinda siku hiyo na kutembea tembea tu ili kupoteza muda.


"Hapana jamani usinifukuze .Tutaishije sasa jamani bilakazi."

Kwa maeneo ya sokoni anaonekana binti mdogo Ecca akiwa analia baada ya watoza ushuru kuvuruga biashara yake kwa kosa la kutolipa ushuru.Ni mwanamke wa miaka 22 tu,mzuri mno.