Chereads / penzi la bahati / Chapter 56 - chapter 55

Chapter 56 - chapter 55

Wanaendelea kutembea kimya kikitawala kati Yao, nyao za miguu yao zinaendelea kusikika zikikanyaga majani na kuwapeleka wanakohitajika.Wanatoka katika himaya ya mtemi na kuingia upande wa msitu unaolizunguka eneo hilo.wanatembea kwa muda wa nusu saa na mbele Yao wanaliona pango kubwa.

Pango ambalo sehemu ya kuingilia wamesimama walinzi na mikuki Yao,pembeni wakiwa wamesimama watu watano ambao mavazi Yao yanafanana na mtu anayeongozana nae wakiwa wameshikilia miale ya moto mkononi.

"wazee wasumbufu hawa" anaongea kijana kwa sauti ya chini ambayo kijakazi wake hakuisikia.Anafika katika mlango wa pango na walinzi wanainamisha vichwa vyao kutoa heshima pamoja na vijakazi nae anapita ndani kijakazi wake akisimama nje pamoja na vijakazi wengine.

Ndani anawaona wazee watatu wakiwa wamekaa kwenye viti vyao kama wanamiliki pango hili ikiwa ni kweli.Anainamisha kichwa kwa heshima na kusalimia.

" habari ya jioni wakubwa" moyoni akijiuliza kama ni aseme ni habari za usiku maana yeye alishalala lakini kwa nyuso za wazee Hawa kwao ni jioni.

" sio nzuri kama unavyoona,kaa" anajibu mzee mmoja wapo.Anatembea hivyo hivyo pasipo kunyanyua sura yake anatafuta kitu kilichowazi na kukaa katikati ya wanaume watatu walioinamisha vichwa vyao chini kama yeye wawili wakiwa watu wazima na wenye mvi lakini Mmoja akiwa na umri kama wake.

" nyanyueni nyuso zenu" anaongea mkuu wao na wote wananyanyua sura zao.

"Muda tuliokuwa tunauhofia kwa miaka mingi umewasili" anazungumza mkuu wao na wengine kutikisa vichwa vyao sura zao zikionyesha ni jinsi gani jambo hili lilivyo la muhimu.

" una maanisha nini mkuu?" anauliza mzee Mmoja kati ya wanne.

" huelewi nini Limbo,na tumekuwa tukiongea hili vizazi na vizazi vya uzao wenu" anaongea mzee mwingine akionyesha kukereka kwani Hali walionayo sio ya mtu kujifanya haelewi.

" Anamaanisha,hatima ya umiliki wako unafikia mwisho ukiendelea kujifanya mpumbavu hivyohivyo" anazungumza mzee mwingine.

" na atatumaliza na sisi tusipokuwa makini" anaongezea mwingine kwa sauti ya chini.

Mzee Limbo au mtemi Limbo na wengine macho yanawatoka pima kwa mshtuko wa habari.Ni habari wanayoijua kwa hadithi na hadithi za mababu wakirithishana vizazi na vizazi lakini hawakujua Kama mstakabali wake utakuwa mikono mwao.

" unamaanisha mmiliki wa ardhi kazaliwa au nguvu ya Ndesha imeongezeka?" anauliza mzee wa pili aliyekaa karibu na mzee Limbo.

" vyote viwili,na sio kama kazaliwa leo,kwa Hali ya hewa inayovuma inaonyesha amekuwa ni mtu mzima na Jana jioni amepokea baadhi ya uwezo wake" anaongea mzee mwingine mwenye nywele zimejisikota na ndefu kufikia kiuno chake,ndevu zake zikifunika mdomo wake.

" lakini mkuu Zulimo mlisema hawajazaliwa!" anauliza tena mzee aliyekaa karibu na Mtemi limbo.

" Sasa naelewa kwa nini baba yako hakukupa utemi licha ya kuwa mkubwa we Makiele una akili nzito kweli,ambacho hujaelewa kipi hapa?" anauliza mkuu Zulimo anayeonekana Hali yake inazidi kuwa mbaya kutokana na maswali ya Makiele kaka wa mtemi Limbo.Mzee Makiele hajapenda alichokisema mkuu Zulimo. lakini Hana jinsi zaidi kumvumilia.Kijana wake aliyekaa karibu yake anamshika mkono wake aliokunja ngumi akimwambia kwa ishara ajikaze.

Mkuu wao ananyoosha mkono juu kutuliza mzozo unaotaka kutokea na wote wanakaa kimya." safari hii wamecheza vizuri kweli,walificha nguvu zao tangu walipozaliwa ndio maana hatukuweza kunusa chochote.na Sasa wameona ni muda muafaka kuzitoa au Kuna kitu kimetokea kilichofanya kuvunjika ngome hiyo" anajibu mkuu wao " Dunila" anaita.

" ndio mkuu Lukumo" anaitikia Dunila akiinamisha kichwa chini kupokea amri.

" unahitaji kuanzisha msako na uhakikishe unampata mmiliki wa ardhi umuoe na kulala nae siku mwezi mkubwa utakopotokea Ili upate nguvu, na wewe Inkula" anaita tena.

" ndio mkuu Lukumo" anaitikia Inkula akiachia mkono wa baba yake aliokuwa anaushikilia na kuinamisha kichwa kupokea amri.

" hakikisha unaanzisha msako wa kumtafuta msichana Nyota na ulale nae kabla ya mwezi mkubwa haujafika,kwani tunamuhitaji akiwa na mimba wakati wa mwezi mkubwa na mwekundu iwapo Dunila atashindwa kumpata mmiliki wa ardhi huyo mtoto atakuwa ni mbadala wetu ingawa hatakiwi kumkosa" anasisitiza macho yake yakimwangalia Dunila.

" vipi kuhusu mtoto wa utabiri?" anauliza mtemi Limbo ambaye amekuwa kimya tangu habari imshtue.

"yupo tayari na hicho ndio kinanitia wasiwasi,endapo mmiliki wa ardhi akiishia mikononi mwake Hali itakuwa mbaya zaidi" anasema mkuu Lukumo akichezesha ulimi wake.

" acha niseme Manangwa kacheza vizuri safari hii,kutupumbaza wote watatu" anaongea Zulimo.

"hata Onduwa nae,harufu ya wamiliki wa ardhi huwa haifichiki sijui aliificha na nini yule mwanamke" anaongea mkuu mwenye mandevu na nywele za kujisokota anayejulikana kwa jina la Pyulilo.

" makosa ya nani hayo,ungemuua kipindi kile haya yote yasingetokea ukaenda ukapumbazwa na uzuri wake na kututia matatizoni sisi" anang'aka Zulimo na Pyulilo kumkata jicho,kwani hiyo ni habari ambayo ikiguswa humfanya awe kama kakalia figa. lakini kabla hawajaendeleza ugomzi wao ambao ungetumia shoka kuukata mkuu Lukumo anawanyamazisha.

" mnaona huu ndio muda wake?" anawauliza.

" mkuu tutawajuaje hao wanawake ?" anauliza Dunila asitake kuendelea kusikiliza ugomvi wa wazee Hawa usioisha,maana akiendelea kukaa hapa watapasua ngoma za masikio yake hapo alipo tayari yanapata moto.

" mtawajua tu,hizo dawa mlizokuwa mnakunywa tangu mkiwa wadogo ndio kazi yake" anawajibu.

" na mtoto wa utabiri je?" anauliza Inkula

"huyo tuachieni sisi,ingawa kapata nguvu kidogo asipompata mmiliki wa ardhi zitakuwa sawa na kazi Bure" anajibu Pyulilo.

" na pasipo Makandelo ndio Amna kitu kabisa" anaongezea Zulimo kifua kikiwa juu tabasamu likijaa usoni kwake akikumbuka namna alivyomuua Makandelo. Pasipokujua kuwa watu wanaowatafuta wako pamoja na siku wakifnya tendo la kukamilisha ndoa Yao tu.Puuuuu! Hali ya hewa ya Mpuli nzima inachafuka na hata himaya zingine.

" yule mshenzi Zulimo,siku Moja nitakuja kumfanya ajikojolee" anaongea mzee Makiele baada ya kutoka pale akiwa na mwanae kuelekea nyumbani.

" makosa ya nani sikuwa mtemi,figisu zao ndio zilizofanya nisiwe mtemi" anaongea mzee Makiele.

" usijali baba nitahakikisha nakuwa mtemi" anaongea inkula.mwenye wazo la kuwa tafuta wanawake wote wawili Ili awe na nguvu zaidi na kuwafyekelea mbali wazee hawa wenye midomo mirefu.

" vizuri mwanangu" anamsifia kijana wake na kuendelea "naona wanaonekana vizuri Leo kuliko mara ya mwisho nilipowaona"

" watakuwa wametoka kutoa sadaka muda sio mrefu" anajibu Inkula.

" hawapati nguvu kutoka kwa Ndesha kwa mda mrefu na Sasa nimejua ni kwa sababu gani wamekuwa dhaifu" anaongea Inkula.

" ni kwa nini?" mzee Makiele anauliza kwa shauku.

" kwa sababu Ndesha sio mmiliki wa ardhi tena,ndio maana nguvu haziji kwao" anajibu.

" aaa,lakini mbona bado ana nguvu,Ndesha namaanisha"

" nadhani nguvu zake zile ni kutokana na kuwa yeye Sasa hivi ni mzimu tu,tena mzimu mbaya"

" kijana wangu ana akili sana,we subiri tutawafyeka wote." Makiele anaongea machoni akiona kabisa anavyowapelekesha Hawa wazee wanaoijiita wakuu hasa yule Zulimo.Pasipokujua kuwa hata kama Wana nguvu pungufu wake bado ni mizimu na kuwaua haitakuwa rahisi.

Katika Kijiji Cha Ntungu Leo kumekucha mapema na watu wote wamekusanyika wakisherekea sherehe ya vijana waliotoka lindoni,ngoma na michezo mbali mbali ikiendelea,watu wakinywa na kula.

Wageni wawili wanawasili ambao watu hawawaoni kwa macho ya nyama.

" mambo yamebadilika tangu nije kijijini miaka ishirini iliyopita" anaongea Manangwa akipita katikati ya watu kichwa akikichezesha kwa muziki ulivokuwa unaendelea.

Mnelela aliyekuwa juu ya mti kama popo anaziona sura hizo anashtuka na kupotea alipo ghafla anatokezea mbele Yao.

" Mkuu Manangwa,mkuu Gulumo" anainamisha kichwa kuwasalimia.

" sogea kwani lazima utokee mbele yangu,naangalia sherehe Mimi" anaongea Manangwa akimsukuma Mnelela kumtoa mbele yake huku akiendelea kutikisa kichwa kwa mziki kitendo kinachomfanya Mnelela amshangae kama huyu kweli ndio mzee mwenye busara anayemuonaga siku zote.

" nini? nisicheze au?" anauliza baada ya kumuona Mnelela akimshangaa

" Amna kitu mkuu" anajibu Mnelela akiendelea kumwangalia mkuu wake akijifanya kijana.

"hujakamatwa kweli?"Gulumo anamuuliza.

" ndio,Niko Salam kabisa." anajibu Mnelela kifua juu akijisifia kwa kazi nzuri aliyofanya.

" Nina uhakika umeshashtukiwa na utakamatwa mda sio mrefu,labda huyo Nzagamba awe ana hisia nzito kama zako,ambako sidhani" anajibu Manangwa ambaye kwa wakati huu anachezesha Hadi kiwiliwil.

" hapana,na mmefuata nini?" anauliza Mnelela .

" Hali ya hewa ya juzi ilivuma tofauti,tukaona tuje kuona kinachoendelea" anajibu Gulumo.

" juzi ile Nza...." kabla hajamaliza Mnelela anaacha baada ya Manangwa kuacha kucheza na kuanza kunusa.

" Kuna nini?" anauliza Gulumo.

" hiyo harufu huisikii au?" anauliza Manangwa akiendelea kunusa.

" ni nyama zinachomwa na kupikwa" anajibu Mnelela." aaah" anashika kichwa baada ya kupiga kwenzi na Manangwa.

" sio hiyo mjinga wewe kwani Mimi sijui harufu ya nyama,harufu Fulani ya zamani naisikia" anaelezea Manangwa.

" kama naijua vile" anajibu Gulumo nae akinusa.

" aaaa! itakuwa ya Nzagamba,nilitaka niwaambie juzi ile jioni aliwinda swala" anajibu Mnelela akitabasamu.

" sio ya Nzagamba,hiyo unaisikia mpaka mlimani sio lazima ufike kijijini,hii imekuwa Kali hapa na inazidi kusogea inatokea upand..." anajibu Gulumo akigeuka kuelekea harufu inakotokea kitendo ambacho Manangwa nae anakifanya na maneno yake kukwama mdomoni baada ya macho Yao kukutana na ya mtu ambaye hawakutegemea kumuona maishani mwao tena.

" MAKANDELO??!!"