Chereads / penzi la bahati / Chapter 60 - chapter 59

Chapter 60 - chapter 59

Kamba za uvumilivu zinamkata kabisa Nzagamba.Anatakiwa kujivunia kuwa mke wake ni mchezaji mzuri wa ngoma,vizuri hajapata kuona lakini yeye anacho hisi ni kumchukua mke wake na kumficha ndani kumpa adhabu ambayo itamfanya asirudie tena kucheza hadharani namna hiyo.Adhabu ambayo akisikia mrindimo wa ngoma kitakachokuja akilini mwake ni adhabu aliyompa na sio kwenda kuunga mduara kucheza.Uvumilivu unakatika zaidi anapomuona akichezesha maziwa yake na pasipo kujua miguu yake inampeleka katikati ya ulingo na anachokifanya ni kumvuta Tulya na kuanza kuondoka nae.

" Nzagamba?!" anaisikia sauti ya Tulya ikimwita na watu wakiongea kupinga kukatishwa starehe lakini hayo yote hakuyasikia kabisa.Wivu na hasira vilikuwa vimetawala kichwa chake na uwezo wa kufikiri.Na ndani ya dakika moja walikuwa wame shatoweka eneo hilo nyuma wakiacha gumzo.

" Nzagamba kafanya nini?nilitaka nione mshindi" Mkita analalamika.

" Mshindi ameshapatikana hata kama hajafika mpaka mwisho.ona" Kilinge anajibu.Mkita anaangalia huku na kule na kuona watu wakiondoka wengine nyumbani na wengine wakirudi kukaa katika makundi makundi wakiendelea kunywa huku hadithi midomoni mwao ikiwa ni Tulya.Kwenye mduara wa ngoma akiachwa Mbula na wenzake wakiendelea kucheza,viuno ambavyo watu wameshazoea kuviona Kila siku.

" yule mwanamke hajui kukata tamaa" anaongea Mkita akimwangalia Mbula ambaye kwa sasa kaamua kufunga na mdundiko kiunoni." Wivu sio mzuri kabisa,Leo Nzagamba kaamua kwenda kulala mapema kama kuku hata kuaga tu" Mawazo ya Mkita yanarudi kwa Nzagamba akicheka.

" sikutegemea kama angeonyesha hadharani" Kilinge anaongezea." nilimuona akijikaza tangu mchana,hii ni kama imemfanya kutekeleza alichokuwa anawaza kwa mda mrefu" Lingo anaongea wakienda kukaa huku akicheka.

Njiani Nzagamba anaendelea kumkokota Tulya pasipo kumwachia mkono wake.Majaribio ya Tulya ya kumwambia amwachie yamegonga mwamba hivyo kaamua kukubaliana na hatima.

Giza na kimya Cha usiku kikiwa kimegubikwa na sauti za hatua wanazopiga zikiambatana na njuga alizovaa Tulya miguuni.Tulya anaendelea kutembea akimfuata Nzagamba hatua zake zikiwa za haraka kama mfikisha habari na pasipo kujali Nzagamba anaendelea kupiga hatua kubwa zaidi na kufanya pumzi za Tulya kuongeza hesabu ya kupumua.

Hatimae wanafika nyumbani, Nzagamba anafungua mlango pasipo kumwachia mkono na baada ya mlango kufunguka anaingia nae ndani anafunga mlango na kuuegemea.Anaanza kuvuta pumzi ndefu akijaribu kujituliza lakini hali ilikuwa mbaya.

Tulya anaangaza macho yake ndani asione kitu kutokana na kiza kilichotanda ndani mwao.Macho yake yanarudi upande aliko Nzagamba asimuone anachosikia ni sauti ya pumzi zake akivuta na kutoa.Tulya anaendelea kusimama asijue afanye nini maana Nzagamba anaonekana hayuko sawa na tangu amuone mchana alikuwa amekasirika na Sasa hali inaonekana kuwa mbaya zaidi.Hataki kuongea asije akatifua vumbi kwani mara ya kwanza alipomuona Nzagamba akiwa amekasirika ilikuwa ni mbaya.Mwili una msisimka akikumbuka siku aliyosema anataka kuolewa nae alipomfuata akijua anamfanyia masihara.Ni kitu ambacho hataki kukumbuka namna Nzagamba alivyomwangalia kama anataka kummeza kwa macho.

Fikra zake zinakatishwa baada ya Nzagamba kumwachia mkono wake.Na mara moja Tulya anauvuta kifuani kwake akiushika kupoza maumivu akijua lazima Kuna alama za vidole.Anasikia Nzagamba akipiga hatua na kuona kiwiliwili chake kikielekea upande wanapoweka taa,anajua anaenda kuwasha taa.

Nzagamba anapapasa na kufanikiwa kushika vijiwe vya kuwashia moto na baada ya majaribio kama matatu anafanikiwa kuwasha taa.Macho ya Tulya yaliyokuwa na ukubwa zaidi ya saizi yake wakati wa giza yanarudi kawaida.Anaendelea kumwangalia Nzagamba anayeendelea kusimama hata baada ya kuweka taa mahala pake.Baada ya kimya Cha mda mrefu Tulya anaamua kuondoka na kwenda chumbani maana inaonekana Nzagamba hayuko radhi kuzungumza,na yeye hataki kuishia mhanga wa hasira zake.

Anapiga hatua chache kuelekea chumbani lakini anashtushwa na sauti ya Nzagamba inayofanya miguu yake kupiga breki.

" unaenda wapi?" Sauti yake ni nzito na ikiwa bado ina hasira.

" ehh?!" Tulya anaitikia utadhani ameitwa anageuka na kumwangalia anamuona bado ameangalia ukutani,taratibu anageuka na macho Yao yanakutana.Tulya hamuoni vizuri kutokana na kivuli Cha Nzagamba kuziba upande wa mbele kwani alikuwa amesimama mbele ya taa na kufanya asionekane vizuri usoni.Lakini yeye anamuona vizuri Tulya,macho yake makubwa yakimwangalia kwa woga kidogo na wasiwasi.Kope zake zikiyaficha macho yake Kila baada ya sekunde wakati akipepesa macho yake.

" chumbani" anajibu baada ya kuona Nzagamba harudii tena swali lake.Macho yake yanatoka usoni kwake na kuangalia chini kitendo ambacho Nzagamba hakukipenda kwani anataka kuangalia macho hayo na kujua anafikiria nini.Kwa hatua mbili ndefu tayari alikuwa amesimama mbele yake, Tulya ananyanyua uso wake baada ya kuona anafunikwa na kivuli Cha Nzagamba na kumuona akiwa amesimama karibu kabisa na yeye.

" umevaa nini?" Nzagamba anajikuta anauliza swali alilosema hataliuliza.

" ehh?!" Tulya anaitika tena akijaribu kupata uhakika wa swali alilosikia kama ni sawa.

" kwa nini umevaa namna hiyo?" Nzagamba anauliza akiendelea kumkagua.

" k...kw..kwa sababu ya sherehe?" Tulya anamjibu kwa kigugumizi ndani yake akijaribu kuuliza swali kama jibu ni sawa.

" ndio uache miguu wazi namna hiyo?" Nzagamba anauliza tena macho yake yakiendelea kutazamana na ya Tulya yaliyojaa maswali kwani hajui ni nini kinaendelea.

" Niangalie na unijibu Tulya" anaongea baada ya kuona Tulya anaangalia chini sauti yake ikiwa juu na kumshtua,Tulya anaruka kidogo kwa woga.

" na kwa nini ulikuwa unacheza namna hiyo nakufanya wanaume wote wakutafune kwa macho eeeh?" anauliza kwa jazba akili yake ikirejea nyuma kwenye sherehe namna wanaume walivyokuwa wanamwangalia na aliowaona wengi waliokuwa wametuna katikati ya miguu Yao kitendo kinachomfanya damu kunuka puani.Watu wameanza kulala na mke wake kwa mawazo wakati yeye mwenyewe hajamgusa.

" nijibu Tulya?" anapandisha sauti juu zaidi,Tulya anashtuka na kushika kifua chake kuzuia moyo wake kutoroka mahali pake maana ulikuwa unaenda mbio kuliko kawaida.

Machozi yanamjaa kwenye macho yake,anainamisha kichwa chini lakini Nzagamba anamshika taya na kunyanyua uso wake.Tulya anafumba macho yake baada ya kuona hasira inayowaka machoni kwa Nzagamba.Machozi yanamtiririka kama mto wakati wa masika."Sikujua kama wewe ni mlevi wa kucheza namna hii,kiasi kwamba uko radhi kutembea uchi Ili tu kuonyesha kuwa wewe ni mcheza ngoma mzuri" Anaendelea kuongea uso wake ukiwa karibu zaidi na wa Tulya.

Hasira zime mjaa Nzagamba asijue anachoongea kwa sasa au hata kama Tulya analia,anachokiona yeye ni Tulya akicheza na wanaume wakimwangali utadhani ni kitu kigeni.Ndio sio kitu Cha kigeni kwa wanawake kushindana kucheza na watu kuwaangalia wengine kwa uchu na wengine kwa burudani.Ni kitendo Cha kawaida Cha Kila siku wakati wa sherehe. lakini kwa Tulya kwake ni kigeni kitendo anachotaka kisijirudie.Tulya ni mke wake,mke wake Nzagamba na anataka ibakie hivyo,wake nje na ndani.wazo tu la mwanaume mwingine kumfikiria mke wake kwa uchu na tamaa ya kutamani kumuweka kitandani kwake na kufanya vitu naye kinamuua Nzagamba.

Anatamani angekuwa na uwezo wa kufuta watu wote kumbukumbu za walichokiona Leo.Yeye ni mwanaume na anajua vizuri mwanaume mwenzake wanavyowaza,alipomuona Tulya akicheza wazo lililopita kichwani kwake ni kumchukua na kumuweka kitandani kwake na kumfanya akate vile viuno akiwa chini yake au juu yake akitoka sauti za miguno na yeye mwenyewe akihisi ni Raha gani atakayopata.Ni wazo ambalo anajua lilikuwa linapita na litaendelea kupita kichwani kwa Kila mwanaume aliyemuona Tulya Leo kitendo kinachomfanya mwili wote kufuka Moshi wa hasira kwani anajua hawezi kuzuia hilo.

" nimefanya nini Mimi?nilichokifanya ni kucheza tu,nilikuwa na furaha ndugu yangu kaolewa nikaamua kufurahia.Mimi sio kichaa kiasi hicho" Tulya nae anakuja juu baada ya kusikia maneno ya Nzagamba.Anamfikiria yeye ni WA chini kiasi Cha kuvua nguo Ili tu kucheza,anamfikiriaje, machozi yanamtiririka.

"Kwa sababu nakupemda na nililazimisha kuolewa na wewe usinione sijithamini kabisa,licha ya kutoa nusu ya heshima yangu kwako kumbuka bado ninayo nusu ambayo natembea nayo mtaani"

Nzagamba anarudi kidogo baada ya kusikia mlipuko wa Tulya.Anaupiga mkono wake uliokuwa umeshika taya zake,mkono wa Nzagamba unarudi kwake." Mimi sio malaya kiasi Cha kuvua nguo ngomani kutafuta wanaume,kama nikiwa malaya basi ni kwa mwanaume Mmoja tu ambaye ni wewe tafadhali usinishushe thamani" anaongea Tulya akifuta machozi anageuka kuelekea chumbani.

Nzagamba anakuwa kama kamwagiwa maji ya mtungi,haamini kama ameacha wivu na hasira vimtawale." Tulya unajua sijamaanisha hivyo" anaongea lakini Tulya tayari ameshaingia chumbani masikioni kwake anaisikia kwikwi yake ikimdhihirishia kuwa amerikoroga na mke wake analia.

"pumbavu..Tulya" anapiga hatua za haraka na kuingia chumbani anakomuona Tulya amelala kifudi fudi akilia.Anapeleka mkono wake kichwani na kusambaratisha nywele zake,mkono wake mwingine ukienda kiunoni.

" Tulya, Tulya" anaita na kwenda kuchuchumaa karibu kitandani.

" sikumaanisha hivyo,Tulya" anaongea akimshika bega,Tulya anaamka na kukaa.Mwanga hafifu unaotoka sebuleni ukiwaangazia." kumbe ulimaanisha nini Nzagamba?" anamuuliza akifuta machozi kitendo kinachompa maumivu moyoni Nzagamba kama kachomwa na mwiba.

" nisikilize ....."

" Nakupenda sana,tafadhali usiutumie upendo wangu kunisimanga unaj....."kabla hajamaliza Nzagamba anakutanisha midomo Yao akimbusu.