Chereads / KIZAZI DHALIMU / Chapter 8 - SURA YA NANE

Chapter 8 - SURA YA NANE

Mziwanda alipofika nyumbani kwa rafikiye alishanga karibishwa na Rehema kitu ambacho hakikuwa kawaida kupatikana pale masaa hayo.

"Karibu ndani," Rehema alimkaribisha mwenzake japo si kwa furaha.

"Asante," Mziwanda aliitikia kukaribishwa kwa sauti isiyo imara, "kwa nini haupo kazini?!"

"Aah! Hujapata taarifa kwamba niliachishwa kazi!"

"Kisa na maana!"

"Mie mwenzako sijui."

"Lakini nimemkuta...nina hamu ya kumuona mke wangu."

"Ndiyo amelekea mtaani kupatana na dereva wa lori la kubeba mizigo kuzungumza naye."

Wakiwa wanazungumza, Ali alisimama mlangoni akionekana mtu ambaye hajaridhia, kwa haraka, Mziwanda aliinuka mitini akaelekea alipokuwa.

"Umefanikiwa!"

"Ndiyo. Nimezungumza naye lakini ikaniwia vigumu kumshawishi akubali ombi langu," Ali alimwambia kwa huzuni.

"Kama umefikia maridhiano naye, kipi cha kutua furaha yako..."

"Nauli yake ni ghali mno...anasema atandamana nawe ikiwa utatoa elfu hamsini."

"Hapana...,"Mziwanda alimpinga," hiyo ni akiba yangu ya miezi mitano. Nitatoa vipi hela hizo...anyway, lazima nimuone mke wangu."

Ali na Rehema waliangaliana kwa mshangao baada ya mwenzao kukubali kutoa pesa kiasi kile.

"Una wazimu au..."Ali alimuuliza kwa hasira,"tutasubiri gari jingine litakalofika baada ya majuma mawili, nauli ya kawaida ni elfu tatu, asituone wahi..."

"Hapana, hakuna anayetawala kwa kiti cha wakati," Mziwanda alimkatiza, "sina lolote la kufanya mjini kwa sasa. Shata na wafanyakazi wa babake wanapanga mapinduzi juu ya mkurugenzi wao. Nitasalia nikifanya nini! Heri niende kwa mke wangu."

Ali na Rehema walishanga kwa taarifa ya mwenzao;

'Everybody wants a fool for a friend but not a daughter,' Rehema alifikiri.

"Rehema, nakuaga. Nafika kijijini kuwajuza wazazi wangu kisha nijiandae kwa safari ya kesho."

"Nakutakia kila la heri."

Mziwanda aliitikia kwa kichwa kisha akaondoka na sahibu yake.

Rehema alipoona wanaondoka, kumbukizi walivyokuwa chuoni zilimrejea walivyokuwa wakizunguka katika mazingira ya chuoni kabla mpenziwe hajatalikiwa mwaka mmoja baadae.

Talaka iliyotokea wakati ambao kampeni za chuoni zilikuwa zimekita mizizi. Ali alikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao walikuwa wamegombea nyadhfa za juu pale chuoni. Ali alikuwa amewania kiti cha kuwa kiongozi wa wanafunzi na kumchukua Mziwanda kama naibu wake.

Siku ya kutoa manifesto na ajenda ilipofika, kila mwanafunzi pale chuoni miguu ilielekea uwanjani kusikiliza ambayo yangesemwa na viongozi watarajiwa.

Wanafunzi waliotaka kuwa viongozi, kila mmoja alisimama na kusema ambacho angewatendea wanafunzi baada ya kuchaguliwa.

Ali aliposimama na kuhutubu mbele ya wenzake, alisoma manifesto iliyotetemesha viongozi wa pale chuoni kuanzia kwa mwenyekiti wa chuo. Ajenda yake haikulenga tu wanafunzi, bali pia wanafanyakazi na jamii nzima iliyozunguka chuo kile kwa jumla.

Baada ya hotuba yake, wanafunzi wote waliinuka wakapiga makofi kitu ambacho hata hawakumtendea mwenyekiti wa chuoni. Rehema alipokuwa ameketi, alimuona akimnong'ononezea naibu wake.

"Ni siki miongoni mwa wanafunzi, lazima aondoke," wanaume wasiojua kunong'ona walizungumza mpaka sauti ikamfikia.

"Vuka mto na watu wengi using'atwe na mamba," Rehema alimuonya walipokuwa wanaondoka baada ya hafla kutimia.

"Tutakumbatia uongo mpaka lini..."Ali alimuuliza akisimama mbele yake,"ukweli hung'aa zaidi na huchukiwa na wengi kwa sababu ya uovu wao."

Rehema alikaa kimya kwa sababu alijua Ali na tabia zake za ubabedume, lakini uoga ulikuwa umemfika baada ya maneno ya wakuu wa chuoni kutua kwa maskio yake.

Siku hazikukawia kabla Ali hajatalikiwa na chuo kwa madai kwamba alipatikana usiku wa manane katika bweni la wasichana akipanga jinsi ya kuanda mgomo wa kuchochea kutolewa kwa mwenyekiti wa chuoni, pia ilitokea kwamba alikuwa akiuza dawa za kulevya chuoni.

Hivyo ndivyo chuo kilivyomtema, akalishwa kalenda kwa miezi miwili na alipotoka akaanza kung'ang'ania kazi za mitaani, hapo napo ndipo Rehema alipata fursa ya kumfahamu Mziwanda zaidi.