Chereads / KIZAZI DHALIMU / Chapter 10 - SURA YA KUMI

Chapter 10 - SURA YA KUMI

Asubuhi na mapema, mjumbe alifika katika boma la Bi. Tabitha kumpa Tumaini ujumbe kwamba anaitwa na Bw. Mazoea. Tumaini alikataa wito wa chifu wa kisiwa kwa kumwambia aliyeleta ujumbe kwamba hatafika.

"Nenda mwanangu," bibiye alimsihi baada ya kuona msimamo wake, "ndiyo, najua alikutenda maudhi lakini huna budi kumsamehe. Lazima kuna taarifa njema anataka kukupasha."

"Taarifa njema! Hakuna mema yoyote ikiwa amesusia kufuatilia chanzo cha vifo vya wale vijana wawili na kupagawa kwa kijana mmoja."

"Hapana mwanangu."

"Siku ya kwanza ujenzi wa klabu hiyo ulipoanza nilimpa maonyo, lakini akayafumbia mato na kuziba maskio kama sikio la kufa lisilosikia dawa."

"Ajali haina kinga."

"Hapana mama," Tumaini alimpinga, "haya yalikuwa na kinga, pasingejengwa klabu hapa kisiwani maafa hayo yasingetokea."

"Yaliyopita tuyapishe, basi nitaandamana nawe. Kuwa mwepesi wa kusamehe," Bi. Tabitha aliingia ndani akachukua khanga tayari kumfuata kuelekea kwa chifu wao.

Tumaini alikubali kuelekea kwa Bw. Mazoea shingo upande. Waliandamana unyo unyo na Bi. Tabitha kila mmoja akiwa kimya. Walipofika katika boma la chifu, hakuhitaji tena kuambiwa kwa kinywa alichoitiwa. Alimuona mumewe ameketi kando ya mwenyeji wake, kwa ghafla machozi yalimtoka akafuta lakini yakaendelea bila kikomo.

Bw. Mazoea alipogeuka na kumuona, alimgusa mwenzake kuashiria uwepo wa mkewe, Mziwanda naye alipogeuka na kumuona Tumaini, alisimama.

Tumaini alimuondokea Bi. Tabitha akaenda na kumkumbatia mumewe akitokwa na machozi ya uchungu. Wote kutoka walipoonana, hakuna aliyekuwa amesema chochote, wote waliongea lugha ya machozi. Pengo la umbali wao wa mwezi mmoja lilikuwa limezibwa.

Mziwanda aliridhia alipomuona mkewe bila jeraha lolote akalia machozi ya furaha, ila kwa mwenzake mambo yalikuwa kinyume, alilia kwa sababu ya kuwa mbali na mpenziwe kwa muda mrefu, akahisi donda lake la moyoni likipona, alihisi yuko katika mikono salama tena.

Walikumbatiana kwa sekunde ishirini hivi, Tumaini akakumbuka siku zake za utotoni katika shule ya chekechea, angetendwa maudhi na yeyote, papo hapo angetoka darasani hata pakiwa na mwalimu na kuelekea katika darasa la Mziwanda kumshitaki, alikuwa mwanzo na mwisho wa maisha yake.

Yale yalipompita akilini, alimuachia mwenzake akaenda mpaka mahali ambapo Bw. Mazoea na Bi. Tabitha walikuwa wakiwa angalia.

"Asante bwana wangu," Tumaini alitoa shukrani, "huyu ni mume wangu."

"Ndiyo, ameshanieleza kila kitu mpaka kilichotokea ukajikuta huku."

Walikaa pale kwa dakika chache wakizungumza kisha baada ya kufahamiana, Tumaini alimchukua mumewe kuelekea alikoishi.

***

Waliketi juu ya jabali wakiangalia angani;

"Hebu basi nambie, maisha hapa kisiwani yamekuwa vipi?" Mziwanda alimuuliza.

"Maisha ni salama. Ila kwa mwezi mmoja nimekuwa mpweke nikitazamia siku utakayofika kunitua kama mkeo kwa mara nyingine."

"Nami vivyo hivyo, nimekuwa pekee yangu. Kuondoka kwako kuliacha pengo moyoni mwangu lisiloweza kuzibwa na yeyote. Nilikosa amani na furaha nikahisi maisha hayana maana tena."

"Wanaume siku zote ni umbea," Tumaini alimchokoza katikati ya kicheko, "najua kwa sasa umekuwa na Shata mpaka ukachoshwa naye."

Mziwanda alimwangalia kwa jicho la kukati, alijua mwenzake anamtafuta kusikia aliyokuwa amemficha.

"Vipi niwe na Shata, siku zote nimekuwa nikikuwaza wewe," alikwepa mtego wake, "hebu basi nambie ulichoniandalia."

Pasi na neno jingine, Tumaini alifikia mfuko wa suruali yake ndefu akatoa kijikaratasi kilichokuwa na shairi la mishororo mitano akamkabidhi, "hiyo ndo zawadi yangu kwako ewe mapenzi."

Ewe wangu mahabuba, mboni mwangu machoni.

Machoni wewe dhahabu, nafasiyo hatatwaliwa yeyote.

Yeyote tamkana kwangu, kwa sababu yako labibu.

Siku zote uwepo wako hufanya siku yangu kung'a zaidi ya nyota angani.

Baada ya kupitia shairi lile, alimwangalia mwenzake.

"Wakati mwingine maisha hukosa maana kwangu kabisa. Utazamapo nyanja zote katika maisha utaona kasoro moja au nyingine."

"Kwa nini ukasema hayo?" Tumaini alimuuliza akionekana aliyeudhika, "nilifikiri ukifika utaniambia unavyonipenda."

"Usinikarikie lazizi, ila ni kuwa mkweli. Baada ya uvumbuzi na maendeleo katika nyanja za kisayansi, watu kanakwamba wamefanywa watumwa na maendeleo haya. Kwa sasa watu hawaamini tena hekima waliyopewa na Muumba kufanya uamuzi, ila kwa sasa kila kitu kinafanywa mtandaoni."

"Why are you always against technology?!"

"Si kwamba siku zote mimi hupinga teknolojia, ila matumizi mabaya ya utandawazi. Mabaya mangapi yanaenea mitandaoni kwa sasa. Filamu zilizojaa umwagaji wa damu, vita, ngono, matumizi ya dawa za kulevya, sheria nyingine zinaenda hata kinyume na mapenzi ya Mungu."

Tumaini alimsikiliza kwa makini akaona umuhimu wa kile alikuwa anaambiwa.

"Mwanadamu ameumbwa kwamba kile aonacho hukishika akilini kushinda anachosikia au anachosoma, ndo maana hupenda kuangalia filamu."

"Kujiburudisha."

"Hamna burudani katika filamu za sasa zinasheheni sehemu nyingi za mauaji, nguvu za kishirikina. Hayo yote yakiwa na nia ya kujaza fikra zetu wale tuangaliao ufedhuli, tusijue njia maadamu za kusuluhisha migogoro yetu ila kwa kutendana unyama."

"Nimekuelewa mwanamikakati," Tumaini alimwambia katikati ya kicheko, "una yapi ya kusema kuhusu kuabudu kwetu."

"Yapo madhehebu mengine yanayowaelekeza wafuasi wake visivyo," Mziwanda alimueleza baada ya dhehebu moja kupita akilini mwake, "tukaishia kuabudu sanamu tukiambiwa ni ishara ya Kristo msalabani, watu wasiotoa zaka au fungu la kumi wasitambulike tena na kanisa lao, hata wakiwa katika shida wasisaidiwe kwa sababu kanisa haliwatambui, kisha tukaishia kuimba nyimbo za Zaburi kuwa sala zetu mbele ya Mungu. Kwangu, maombi ni kile mtu asemacho kutoka moyoni mbele ya Mungu.Tukatumia jina "wakristo" kuficha maovu yetu."

"Siku moja ukweli wako utakuweka matatani. Kwa muoga huenda kicheko, kwa shujaa kilio,"Tumaini alimwambia akiinuka tayari kuondoka.

"Shujaa hufa mara moja ila muoga hufa mara elfu moja," Mziwanda naye alimpinga, "and sometimes to know who you truly are, you have to stand against all odds."

***

Shata ukumbini alipoketi hakuwa na amani baada ya babake kumtimua katika kasri lake baada ya kumpotezea kampani lake. Mamlaka yote alikuwa amevuliwa akapewa masaa sita kuondoka nyumbani kwao. Alimkumbuka Rehema rafikiye aliyepatana naye chuoni, lakini akakumbuka maasi aliyomtenda mpaka kupoteza kazi.

Mali aliyokuwa na tamaa ya kumiliki ilikuwa imeota mbawa ikatoweka isimfaidi yeyote, baba na mwana sawia.

"Hakuna rafiki mwingine nimthaminiye kama Rehema," alijisemea akiinuka kochini tayari kuondoka kuelekea kwa rafikiye.

Alipakia nguo zake katika begi mbili akatoka na kufunga mlango nyuma yake, alianza safari lakini alipofika langoni na kuangalia nyuma machozi yalimtoka baada ya fikra kumpitia kwamba hataishi tena nyumbani kwao.

"Nakupa masaa ishirini, nirudipo kutoka Kenya uwe umeondoka. Mwana afriti, anayemuwazia babake mabaya. Lipi sijafanya kwa akili yako mwanangu, nimepoteza, lakini nawe umepoteza vyote ambayo ungerithi kutoka kwangu," aliyakumbuka maneno ya babake kabla hajaondoka,"nani atakubali kuozwa kwa mwanawe baada ya kudhihirisha unyama na ujinga wako wazi. Nimekukinga na kila baya, sasa nimekuachia, 'nenda kapambane na ulimwengu."

Alitoka langoni akalifunga nyuma yake, alikuwa ametia msumari moto kwenye kidonda na ulikuwa umefika wakati wa kuvumilia maumivu. Yalikuwa masaa ya adhuhuri, aliburura mabegi yake kwa shida, akahisi ulimwengu umewekwa mabegani mwake, tena akahisi kila aliyekutana naye barabarani akimwangalia kwa macho ya kumulaana kwa vitendo vyake.

Jua lilifanya akaroa kwa jasho, mtu aliyekuwa hajazoea safari za miguu ilimuwia vigumu lakini hakuwa na budi kuvumilia yote. Maisha yake alipojiunga na chuo mpaka kuhitimu yalimpita akilini.

Baada ya kujiunga na chuo, kwa haraka aliingiwa na "ustaarabu" wa huko kwa sababu ya tabia zake. Alianza kuona mambo aliyokuwa akiona kwa filamu. Wasichana wa chuo waliobadili taaluma zao usiku na kuwa mashangingi.

"Unafanya nini mahali hapa," Mziwanda alimuuliza siku moja baada ya kumkuta nje ya danguro.

"Yanakuhusu nini!" Alimuuliza naye kwa dharau akigeuka na kuangalia upande mwingine.

"Hufai kuwa hapa kabisa," Mziwanda alimshauri, "you are too beautiful to be in such a place, and your dad is richer to take care of all your needs."

"Niache, kwani hawa wengine ni vinyago au...wao pia ni watu kama mimi, kisha kama mimi ni mrembo unavyonisemea kwa nini usimuache huyo mtu wa kijijini unijie, mishe!"

"Usitawaliwe na roho ya uasherati."

Kwa maneno ya mwenzake, alimtupia jicho la kuchukiza kisha akaondoka.

Pale barabarani aliona ukweli wa maneno ya Mziwanda, wala hakujiona pekee yake aliyeingiwa na roho mbaya ya uasherati bali dunia nzima. Watu walienda vitendo kama wanyama, alipokumbuka hata barabarani walipokuwa wakijipanga, wengi wa "wafadhili" wao walikuwa waume wa watu, kuanzia kwa wavulana wa chuoni, wahadhiri, watu wa afisi tofautitofauti mpaka watu wa serikalini.

"Advancement indeed," alijisemea akitikisa kichwa, "the more we advance technologically, the more our thoughts are becoming futile. We cannot control our own emotions, like unreasoning animals, we do things blindly without thinking of consequences or our attitude towards God. All we do saying it's freedom, but freedom which has no limit is not freedom at all but slavery."

***

Alipofika nyumbani kwa Rehema akamuona, alihisi uoga kumsongea. Rehema alipomuona mwenzake, aliinuka akaenda kumlaki, alipofika karibu yake, aliona alama ya machozi usoni.

"Nisamehe," Shata alimwambia akitupa mabegi yake chini na kupiga magoti mbele ya mwenzake.

"Inuka," Rehema alimwambia akimuinua na kumkumbatia, "dunia ni duara. Hujui kesho yako, hakuna haja ya kumtenda yeyote mbaya."

Baada ya maneno yale Rehema alimsindikiza mwenzake mpaka katika nyumba yake, walipiga soga kwa masaa kadha wakisimuliana kila lililotokea wakati walipokuwa