Chereads / PAINTED LOVE / Chapter 1 - Chapter 1: Home

PAINTED LOVE

its_cana
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 1.5k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - Chapter 1: Home

Majira ya mchana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere kijana mmoja mtanashati anaonekana akiangalia huku na huku baada ya kushuka katika ndege.

Baada ya kupepesa macho anamuona mtu aliyekuja kumpokea, anajongea mpaka kwa huyo mtu huku akiwa amevalia tabasamu usoni mwake "Haha Mr John Yani upo vilevile kama nilivyokuacha mara ya mwisho" aliongea huku akisalimiana nae kwa kushake mikono na huy Mr John ambae ni Mzee wa takriban miaka hamsini hivi, "Haha naona na wewe unazidi kuwa handsome zaidi ya mara ya mwisho kuonana na wewe" "Mzee wangu acha zako haha me mbona nipo kawaida kabisa" "I hope wazazi wako watakuwa more proud of you son" "They must be", baada ya salamu kumalizika, kwa pamoja wakaongozana mpaka kweny gari ambalo Mr John alikuja nalo hapo airport.

Safari haikuchukua muda mrefu sana na gari likaingia Ndani ya mjengo flani hivi wa kitajiri na hadhi ya juu wakatoka kwenye gari, mara baada ya huyo kijana kushuka kwenye akakimbiliwa na kurukiwa mbwa mmoja aina ya German Shepherd "Hahaha Zeus boy I missed you alot" na mbwa akaitikia "Woof woof" kana kwamba anasema miss you too Apollo huku akimlambalamba uso wake.

Ndipo mlango unafunguliwa na Kisha Mwamamke mmoja wa miaka kama 40 na ushee hivi mwenye muonekano wa mwanamke anayejitunza na umbile ambalo bado linawafanya vijana na wababa wavunje shingo kwa kumtazama akipita kiukwel alikuwa na uzuri wakipekee ingawa alikuwa mtu mzima "Eeh jaman mwanangu mpendwa huyo" aliongea kwa upendo huku akimkumbatia Apollo "Mama shikamoo I missed you alot" "Hakuna ambae hajakumiss Apollo wangu".

*********************************************

Kipindi kijana Apollo akiwa anapokelewa kwa furaha katika familia yake, upande wa mwingine Binti mmoja mrembo wa sura na umbo anaonekana akiwa akilumbana na mama yake juu ya maamuzi ambayo hajaafikiana nayo kabisa "Mayrah maamuzi yangu ni final unless unataka kusamehe Kila kitu kuhusiana na career yako" Aliongea mama ake huyo Binti "Lakini mama this is not fair kabisa like how can you do this to me" Alijibu Mayrah huku akitokwa na machozi kwasababu ya maamuzi yaliyotolewa na mama yake.

Kwa hasira akaelekea chumbani na kubamiza mlango kwa nguvu huku mama yake akimuangalia na kujisemea "Nisamehe sana Binti yangu lakini hii ndo njia pekee nayokutengenezea ili upate maisha mazuri badae"

Akiwa Ndani amejifungia Mayrah akawa analia bila ya kuwa na mtu wa kumfariji ndipo simu yake inaita anaiangalia mtu anayempigia na kuona ni mpenzi wake aliyemsave LOML❤️ yaani Love Of My Life anaitazama simu huku machozi yakiendelea kumtoka mpaka pale simu inapokata lakini mpigaji hakutaka kukata tamaa hivyo akajaribu kupiga tena na ndipo Mayrah baada ya kukusanya ujasiri wake na kujizuia kulia kwa muda anapokea simu "Hellow mchumba" sauti ya kijana wa kiume ilisikika kwenye simu "Yes my love mambo" Alijibu mrembo huyo "Pouwah kabisa mbona hukupokea simu mara ya kwanza nilivyokupigia?" "Simu ipo kwenye charge mpenzi alaf nilikuwa busy na some stuffs" "Ouwkey then check you back later nilikuwa nataka nisikie sauti ya malkia wangu kabla sijafanya mambo mengine" "Haha jamani, una hatari we kijana" "Mbona umechelewa kulitambua Hilo mama, anyway badae, nakupenda" "Hehehe sawa baba angu nakupenda zaidi" baada ya maongezi kuisha akakata simu Kisha akafungulia koki yake ya machozi iendelee kutiririka.

*********************************************

Upande wa Apollo, baada ya kukaribishwa Ndani kwa bashasha na Kila mwanafamilia akaenda zake mpaka chumbani kwake aoge ili kuondoa uchovu wa safari yake iliyomtoa kutoka America mpaka kufika Tanzania.

Baada ya kumaliza kuoga akatoka bafuni huku akiwa amejifunga taulo kiunoni, akachukua simu yako na kumpigia mtu, haikuchukua mda mrefu sana simu ikapokelewa na sauti flani hivi tamu ya kike ilisikika kwenye speaker "Hi Darlin' I hope ushafika Tz maana umenpigia kwa normal call " "Yes Mamie nipo home right now" "Aww jamouwni, badae I'll have to meet with you I can't wait tomorrow ni mbali sana ety.." Aliongea mdada huyo kwa madeko "Well I'm afraid we can't meet kwa Leo labda siku nyingine" "Bhana kwanini tushindwe kumeeet Leo au una plans zako na hao wanawake wako wengine" "Nope, najua unajua jinsi navyokupenda mchumba Sasa kwanini niwe na side chick wakati Kila kitu napata kutoka kwako hapa ni some family matters ndo yananifanya nishindwe kuonana na wewe Leo" "Sawa kwa Leo ntafanya kama nakuelewa but kesho if we don't link ntajua kama unanipenda kweli au la" "Usijal mwanamke wangu everything will be alright" "Ouwkie chwirrie lemmi get busy sasa my mubebe" "Sawa babe lovin' you" "Way more my love"

Baada ya kuongea na simu akavaa nguo zake Kisha kushuka downstairs kujumuika na family yake katika chakula Cha usiku.

Kufika mezani anawakuta wote wameshaketi katika meza hiyo mama yake akiwa amevaa pembeni ya mwanaume mmoja ambae ndiye alikuwa baba Yao na pembeni akiwepo mdog wake wa kike aitwae Vera hivyo kujumuisha watu wanne akiwemo na Apollo.

Meza ilijawa na vinono mbalimbali vya kuufanya mdomo ujae mate, Apollo baada ya kukaa na kusalimiana na Wana familia akakata paja la Bata mzinga na kuongezea na vimbogamboga vya majani nakumalzia na pilipili Kisha kuanza kufurahisha mdomo kwa utamu huo wa chakula huku akiendelea kupiga story mbili tatu na nduguze.

*********************************************

Nyumbani kwa kina Mayrah, mama yake aonekana akiwa anaongea na simu lakin kwa mwonekano ni maongezi flani hivi ambayo kwa namna yoyote Ile hakutaka Mayrah asikie hayo maongezi "Tell me this plan of yours is going to work smoothly" Aliongea mama huyo kwa sura yenye u serious mwingi "Mona my Mona tangia lini umeanza kuwa na mashaka na maamuzi yangu, ni kwamba huniamini kama ntafanya Kila kitu kiwe sawa" "Kumbuka tunachezea hisia za Binti yetu hapa, Mimi kama mama yake sikutaka kabisa hiki kitu mpaka najutia kwanini nilimwambia ona Sasa mwanang mpendwa amejifungia Ndani na hataki hata kuniona, whatever you are doing whether it's for the better of our daughter or your own sake pray that it goes smoothly" Alimaliza kuongea Kisha akakata simu huku chozi likifanikiwa kumporonyoka kutoka machoni mwake, akalifuta kwa kitambaa chake na kuelekea chumbani kwa Mayrah ili kuangalia anaendeleaje mwanae.

"Mayrah" aliita mara baada ya kufika mlangoni lakini hakupata jibu lolote lile zaidi ya ukimya tu akaita Tena lakini ilikuwa vilevile tu "Mayrah mwanang najua maamuzi niliyoyafanya yamekuumiza na hujayapenda lakini Binti yangu naomba please try to consider ni kwanini nameamua hili jambo, Mimi kama mama yako naelewa unachopitia saivi kwaio naomba unisamehe sana" alinyamaza kusikilizia kama atapata jibu lolote kutoka upande wa pili lakini halikutoka jibu lolote "Anyway please have something to eat usilale njaa mama yako pia naumia" alipomaliza kuongea akaondoka na kuelekea chumbani kwake huku sura ikiwa imemshuka .

Muda wote mama yake alipokuwa Akiongea, Mayrah alikuwa amekaa chini amejiinamia huku akiwa ameegemea mlango mama yake alivyoondoka akasubiri kama nusu saa hivi ndipo akafungua mlango na kwenda jikoni kupakua chakula kimtoshacho na kurudi nacho chumbani kwake upesi akijua mama yake ameshalala kumbe mama yake alikuwa anamwangalia kupitia mlangoni huku akijua kuwa kama atajionesha basi atamfanya bintie ashindwe kufanya alichokuwa anafanya na baada ya Mayrah kuingia Ndani na kufunga mlango wake nae akafunga mlango wake na kujilaza Kitandani akiwa na mawazo.

*********************************************

Katika restaurant flani hivi Ndani ya Masaki kijana mmoja mwenye muonekano wakitanashati anaingia Ndani ya restaurant hiyo na kwenda direct kweny meza mojawapo iliyopo empty anatoa laptop yake kwenye begi lake na kuiwasha, mda si mrefu anakuja waitress mmoja na kufika mpak kwenye meza yake "Welcome to Mamboz sir what would you like to order please" aliongea waitress huyo kiutaalam zaidi na kwakuwa restaurant hiyo watu wengi wa mataifa tofaut tofaut walikuwa wanafika pale hivyo lugha kuu iongelewayo na wahudumu ni English, huyo kijana akamuangalia huyo mdada mbele yake Kisha akatabasamu "Naomba unletee sekela with pineapple juice" "Okay sir order yako itakamilika muda si mrefu" "Alaf while nasbiria naomba unletee some appetizers" "Which type specifically, sir?" "Ummh... I'd like spring rolls with shredded chicken and then skip the formality call me Aidan" "..." Mdada alikaa akimuangalia mshkaji then "Okay Aidan basi subiri kidog order zako soon nakuletea" "Okay ..." Alijibu huku akiwa kama anasubiri kuambiwa kitu "Raquel (Rakel)" Alijibu waitress huyo baada ya kuelew anachosubiri mteja wake huyo.

Baada ya kumalizana na Aidan akarudi chap mpaka kitchen kuwapa order Kisha akachukua appetizers kama alizoagizwa na mteja huyo na kumpelekea pindi muda huo jamaa akiwa anaangalia progress ya mapato yake ya cryptocurrency akapokea order yake Kisha akawa anakula mdog mdog huku akiwa anasubiri sekela yake.

Soon akaletewa order yake ya kwanza, alipoiona tu akaweka laptop yake pembeni ainjoy mlo wake bila shida yoyote "I could use your company here" alimwambia Raquel ambae ndo alimletea order yake "I'm sorry but I can't, you see hapa nipo kazini kwaio nikisema tu nikae it will cost my job" "Okay nmekuelewa mrembo thanks anyway" "You're welcome" akaondoka na kuendelea na kazi akimwacha Aidan mwenyewe "Such a nice name, Raquel" Alimuangalia kwa mbali Kisha akendelea na mlo wake.

Alipomaliza, Raquel akafika Tena,mshkaji hakuwa Tena na sababu ya kubaki hapo akalipa bill alafu akatoka zake nje na kupanda Ndani ya gari lake na kusepa huku Raquel akimwangalia akiondoka "Raquel" sauti ilimuita kwa nyuma akageuka na kumuona mfanyakazi mwenzake "Tell me amekuomba namba" Aliongea rafiki yake huyo "Haha we nae" "Mmh nambie basi na wewe mama sio kwa kuangaliana hivyo" "Haha Jane bhana, me hajaniomba namba ye kalipa bill then akaniaga na kuondoka" "Mmh jamaani Yani Mimi handsome kama yule nisingekubali aondoke bila yeye kuchukua namba yangu, anyway let's get back to work manager asije akafoka badae" wakarudi kuendelea na majukumu Yao ya Kila siku.