RIO DE JANEIRO - BRASIL.
Baada ya ndege kukatiza kati kati ya bahari ya atlantiki , mnamo saa sita na dakika ishirini ilitua katika uwanja wa ndege wa rio de janeiro, nchini brasil. Vijana wawili walionekana kutoka nje ya ndege na kuelekea sehemu iliyoandikwa "arrivals" neno lenye maan wanaowasili.
Mmja wa wale vijana alikuwa ni kijana mwenye umbile la kawaida lakini Mwili wake ulikuwa mkakamavu kuliko kawaida.
"Mateo Antonio"
liliandikwa bango kubwa upande wa mapokezi ya wanaotoka kwenye ndege. Alice aliyekuwa karibu na mateo Antonio alimuonesha mateo kufata uelekeo wa mtu aliyeshika hilo bango.
Mateo Alienda moja kwa moja na kusimama karibu na mwanamke yule aliyeshika lile bango lenye jina lake.
"You're mateo antonio? Iliuliza sauti ya kike ambayo ilikuwa ni mzuri masikioni kwa yeyote atakayeisikia.
"Am mateo antonio". Alijibu mateo kwa kifupi na kumwangalia Alice aliyekuwa nyuma yake kuashilia kwamba wapo pamoja.
Alice hakuhitaji kuongea sana alitoa ishara moja tu ya kuwa yeye ndiye aliyekabidhiwa huyu mtu na inatakiwa kumkabidhisha kwake.
"Am Alice William " Alisema kisha kukaa kimya.
"Follow me please". Alisema yule mwanamke bila ya kujitambulisha jina lake.
"Is this how Brazilian behaves? They asks others names without telling their names too.! " alijisemesha mateo kisha kumfata yule mwanamke Alice akiwa nyuma yake.
Waliingia kwenye Gari jeusi aina ya black SUV , Gari lilikata kona kutoka airport na kukunja kulia kufata uelekeo wa bara bara iliyokuwa inawaka taa za kila aina katika majengo Marefu yaliyolipamba jiji hili la rio de jenairo. Dakika chache baadae walifata uelekeo wa jengo moja kubwa lililokuwa limeandikwa "RIO DE PARADISE". Na yule mwanamke alisimamisha Gari hilo aina ya black SUV na kuwaomba wageni wake wamfate.
"Follow me". Aliongea maneno mawili tu kuashiria kwamba wamfate.
"Alice hivi huyu mwanamke ni roboti? Aliuliza mateo antonio
"Hey haijalishi namna gani anabehave tambua kuwa we need to follow her yeye ndio mwenyeji wetu...kama hutaki kufata baki ndani ya Gari. Aliongea Alice huku akitoka nje na kubamiza mlango wa Gari lile.
Waliingia ndani ya jengo hilo la rio de paradise na kupanda lift iliyowapeleka moja kwa moja katika ghorofa ya themanini. Mlango wa lift ukafunguka na yule mwanamke bila kusema neno alitoka nje ya lift hiyo kuashiria kwamba hapo ndio mwisho wa safari yao. Alifungua mlango uliokuwa umeandikwa "RESTRICTED AREA DO NOT OPEN".
Bila kujali maana ya maneno yale walitokea upande wa pili wa mlango ule na kukuta ndege aina ya helikopta yenye rangi ya chatu ikiwasubiri mbele yao , ikiwa imekalia neno moja lililokuwa likisomeka kama H.
Upepo ulianza kuvuma taratibu kuashiria ndege ipo tayari kuondoka.
"Get in". Alisema yule mwanamke na kisha kuvaa kifaa cha mawasiliano kilichopo ndani ya ndege hiyo. Huku akiwa ana
Alice na mateo walifanya kama walivoambiwa. Walijikuta wanashindwa kuvumilia kuburidisha macho yao kutokana na uzuri wa jiji hilo la rio de jenairo.
Sauti ya yule mwanamke ikawatoa katika mshangao huo na kupanda kwenye helikopta hiyo na kuvalia kifaa cha kupunguza sauti na pia hutumika kuwasiliana wawapo angani.
"This city is so beautiful I wish I could start my life here one day". Alisema mateo Antonio na kufanya Alice kugeuka kumwangalia mateo kwa mshangao.
"Your wish won't come true , ouch sorry for that..! This ain't your destination." Alisema yule mwanamke huku akielekea upande wa kaskazini kwa kasi ya ajabu.
"Where is our destination ? Aliuliza Alice ambaye nayeye alikuwa hajui ni wapi wanaelekea.
"We're going in the borderlands of brasil and colombia". Alijibu kifupi kisha kubonyeza kitufe kilichokuwa mbele yake.
"Your destination is colombia in the city of uraquein" aliongeza kusema yule mwanamke na kisha kukaa kimya.
"Colombia !!! Wote walishtushwa kutokana na taarifa waliyoipata walipokuwa bado jijini dar es salaam. Asubuhi ya siku hiyo ulitokea mlipuko mkubwa katika jiji hilo likidhaniwa kuwa lililenga kumuangamiza raisi Aloyce kasmili
"You're taking us to our death." Aliongea mateo Antonio huku Alice akionesha kuwa na wasi wasi pia.
"You're going to meet your president he has some work for you there in uraquein".
"We've been following you around since we met, who are you by the way? Alice aliamua kuuliza
"I am A1" alisema yule mwanamke.
"You call that a name?. Aliuliza mateo
"You'll understand one day". Alijibu na kisha kukaa kimya .
Safari yao iliambatana na ukimya wa masaa manne walikuwa wakipita katikati ya msitu wa amazoni na kuona jinsi msitu huo ulivyokuwa unatisha wakati huo wa usiku.
"We're crossing the amazon forest...brace your self for what has to come". Alisema A1
Ilikuwa majira ya saa kumi na nusu ya alfajiri , mvua kubwa ilianza kunyesha katika anga za msitu huo wa amazoni. Helikopta iliingia katikati ya wingu jeusi liloambatana na rangi zilizosababisha msiguano kati ya hewa na mawingu...hivyo kusababisha mgurumo mkubwa usio kawaida.
"I can't see the front" Alisema A1 kuonesha kuwa alikuwa na wasi wasi .
Alice aliweza kuona wasi wasi Aliokuwa nao A1 lakini alishindwa kufanya chochote.
"Trust your self we can get out of here if you ain't wavered by this storm". Aliongea kwa sauti mateo kumtia moyo na kutoa wasi wasi aliokuwa nao mwanamke yule ambaye jinalake alijitambulisha kama A1.
Upepo mkali uliweza kuwaharibia mawasiliano kati yao na walijikuta wanapita kati kati ya radi kali zilizosababisha ndege kushindwa kusoma uelekeo.
"The radar isn't working". Alisema A1 kisha kuwaangalia mateo na Alice .
"Give me that bag and wear them as well...we are about to read the end of the forest..s..so we need to jump or else we're going to die from the clash." Alisema A1 na Alice alifanya maamuzi ya haraka kuchukua begi lililokuwa nyuma ya siti waliyokuwa wamekaa na kumpa A1 na moja kumpa mateo.
" the is only two bags." Alisema Alice
"That doesn't matter you will jump together with him." Alisema A1 na kumfanya Alice kumwangalia mateo kwa wasi wasi.
"Mateo maisha yangu yapo juu yako, of I die know that nitakufata mpaka kuzimu kuhakikisha nina kumaliza." Alisema Alice huku akimvisha begi lile mateo.
A1 hakujua wanaongea Nini ila alidhani kwamba Alice alikuwa anamuaga mateo na kufanya maombi yake ya mwisho.
"You have to jump first or you'll die...I will try controlling it for the time being." Alisema A1 kwa sauti ya juu.
Alice alimkumbatia mateo kwa mikono yake na miguu yake kwa nguvu , kuonesha kwamba yupo tayari kukabiliana na kifo chake. Kwa kasi ya ajabu waliporomoka kutoka juu na kuanza kushuka chini, upepo mkali uliwapeleka kushoto na kulia mpaka pale mateo alipoweza kuendana na kasi ya mwelekeo wa upepo. Aliachilia mikono yake na kumfanya aelee angani.
Kelele za Alice aliyekuwa kamkumbatia kwenye tumbo lake zikamkumbusha mateo kuwa inatakiwa kufyatua kifaa cha kuachilia parachuti. Haraka bila Kupoteza muda alifyatua kifaa hicho na parachuti kubwa lilitokea kutoka ndani ya begi alilovaa mgongoni mwake na wote wawili wakaanza kuelea angani.
Kelele za Alice zilitulia baada ya kuona sas hawashuki kwa kasi kama waliyokuwa wakitumia mwanzo.
Mlipuko mkubwa ulisikika baada ya A1 kutoka ndani ya helikopta ile. Aliweza kuliongoza parachuti lake mpaka upande walipo mateo na alice.
"Follow me this is the direction of the borderland." Alisema A1 baada ya kuwa karibu nao na mateo Alifanya kama alivoagizwa.
Walitua katika sehemu iliyokuwa na majani marefu yaliyostawi kutokana na uwepo wa mvua nyingi.
Alice alipoteza fahamu kutokana na kutua kwa kishindo na wasi wasi.
"Is she okay." Aliuliza A1 baada ya dakika chache za kutoa kamba zilizokuwa mabegani mwake zilizoshikilia parachuti.
"She is okay, she has just fainted." Alijibu mateo aliye mshikilia alice kwenye mikono yake. Aliweza kuona uzuri wa Alice alipokuwa kapoteza fahamu.
"A woman is a woman she can't be man." alijisemea mateo na kisha kumbeba Alice mgongoni mwake.
"Where are we going now? Aliuliza mateo
"I've tried to make communication with others , they've seen my position so they will be here soon." Alijibu A1