URAQUEIN-COLOMBIA
Uchunguzi uliweza kufanyika kutambua chanzo cha kupotea kwa mawasiliano na chombo kilichokuwa kinapaa angani.
"Inaonekana ndege imeanguka mwisho wa msitu wa Amazon, tumeweza kupata sehemu alipo agent A1 ." Ilisikika sauti ya kiume iliyokuwa nzito
"Hakikisha mnatuma timu ya wokozi kwenda kuwaokoa." Wameweza kutoka vizuri toka rio de janeiro, nini kimewapata hapa kati kati mpaka chombo kupoteza mawasiliano? Alisema raisi kasmili
"Sawa mheshimiwa raisi Agent A1 hajawahi shindwa kazi. Tumemfunza toka akiwa na umri wa miaka saba anajua nini anapaswa kufanya katika suala hili. Amejaribu kuwasiliana na watu wetu waliopo mpakani na sasa wanaelekea kuwakoa." Ilijibu ile sauti nzito.
" hakikisha mnafanikisha kumleta hapa uraquein haraka iwezekanavyo tumeshapoteza masaa mengi kuwasubiri. Father appolo yupo sehemu ya kukutania ili aweze kumchukua mateo antonio." Alisema rais kasmili
"Ondoa Shaka mheshimiwa rais soon wanawafikia wametuma taarifa kwamba wamewakaribia." Alijibu B2
"A1 we are approaching you , remain where you're right now." Alisema B2 kwa lugha ya kiingereza.
Haikuwachukua muda mrefu kufika walpokuwa A1 , Alice na M107. Waliweza kuwachukua kwa usafiri wa helikopta iliyowapeleka moja kwa moja mpaka uwanja wa Ndege wa bogota.
BOGOTA INTERNATIONAL AIRPORT
Ni maneno yaliyokuwa yakisomeka juu ya jengo moja la ngorofa lililokuwa limeyengenezwa na vioo.
Baridi ilikuwa kali maan a bado jua halikufanikiwa kukutana na uso wa dunia.
Watu wanne walitoka nje ya helikopta iliyokuwa bado ikizunguka upanga wake. Ingekuwa ni bongo ambako vumbi hutawala wakti wote watu wote wagekuwa wameoga vumbi. Lakini ilikuwa tofauti sana katika nchi ya colombia kutokana na mvua baridi ndiyo iliyotawala katika eneo hilo.
Alice na A1 walijikunyata kutokana na baridi. M107 alivua koti lake alilokuwa amevalia na kumfunika alice.
"Asante Mateo " Ali jibu Alice kwa sauti yake nyororo na kumwangalia Mateo kwa jicho la shukrani.
"He saved you , you have to thank this man." Alisema A1 baada ya M107 kutangulia mbele.
"I will. It's not the time yet." Alijibu alice William
"I can see the way you look at him. Admit that you love him. He has eyes for you too I can tell." Alisema A1
"Don't tell me that , I already know. He is a nice man. Alijibu Alice
"I don't think that coat is enough. You need to cuddle up and get a natural heat." Alisema A1
Alice alitabasamu baada ya kusikia ushauri wa A1
"That's good for an advice, nadhani pia mnafundishwa Namna ya kuuteka moyo wa mwanaume. Alisema alice
"Are you talking to me? Aliuliza A1
"Yes I've just used my language. I thought you might understand.
"I can just use English that will make me comfortable around you.
"I can teach you , you know. Alishauri alice
"I've no time. But I will try learning a thing or two; I won't disappoint am a good learner. If you've time. A1 alisema
Mbele yao M107 alikuwa pamoja na yule mlinzi mmoja ya walioenda kuwafata katika mpaka wa colombia na brazil. alikuwa na asili ya afrika.
"Unajua kiswahili? Aliuliza M107
Yule mlinzi aligeuka sura yake ikionesha uchangamfu na kumwangalia kwa tabasamu.
"Ndiyo Mimi ni mzaliwa wa shinyanga, kiswahili Ndiyo lugha yangu. Nimetoka nyumbani toka nikiwa na miaka tisa, nilichukuliwa na shirika la kidini na sasa nafanya kazi katika kanisa la mtakatifu barbara mjini uraquein. Alijibu kwa kirefu na kukata maswali yakiyokuwa kichwani mwa mateo Antonio.
"Tunaelekea wapi sasa? Ilibid aulize mateo kuona wanazidi kusonga mbele
"Tunaenda kukutana na padre apollo, yupo mlango namba 24E. Tutaelekea moja kwa moja mji mdogo wa uraquein Haraka iwezekanavyo.
Dakika chache baadae walitokea kwenye mlango mkubwa wa vioo ulioandikwa 24E.
Walikutana na gari aina ya black SUV. Na njebya gari mwanaume aliyevalia vazi jeusi na kitambaa cheupe kilikuwa kwenye shingo yake.
"Hello my child, the angel of God are in your side. It's time to enter the church". Alisema father Apollo baaada tu ya kumwona kijana aliyemwona kwa picha siku iliyopita.
"Pole na safari." Alisema father Apollo kwa kiswahili cha kubabaisha.
"Asante father."
"It's father Apollo." Alijibu father Apollo kujitambulisha
"Am happy to know you, hope you know me." Alisema M107
"I know you." Alijibu kwa kifupi kisha kumsogea walipokuwa alice na A1
"A1 are you alright? Aliuliza father Apollo baada ya kumaliza mazungumzo na Mateo
"Am alright father. Thanks God we made it." Alisema A1
"And who are you my child? Aliuliza akimuangalia alice usoni
"My name is alice William. I came with him." Alijibu alice huku akionesha ishara kwa mkono wake wa kulia.
"Okay we don't have time, we need to hurry up so that his training can begin today." Alisema father Apollo na kuingia kwenye Gari aina ya black SUV. Huku akifatiwa na A1, alice ,M107 na yule mlinzi aliyejitambulisha kuwa katokea shinyanga Tanzania.
RUAHA -MOROGORO
Gari lilipita katika daraja moja kwa kasi huku likisindikizwa na sauti ya mziki uliokiwa ukipiga ndani ya Gari hilo.
Abiria wasiopingua 60 walikaa ndani ya Gari hilo huku baadhi wakiwa wanafurahia burudani iliyokuwa ikitolewa ndani ya Gari hilo. Na wengine kutokana na uchovu baadhi ya abiria walikuwa wamesinzia.
Katika siti namba 34 iliyokuwa kati kati ya Gari hilo kijana mmja aliyevalia kofia nyeusi na nguo nyeusi huku chini akiwa amevalia viatu vyeusi. Alikuwa akiangalia nje baada ya kukaribia maeneo ya kidodi. Alijua sehemu alipo baada ya kusikia muhudumu wa Gari hilo akitangaza abiria wanaoshuka kituo kinachofuata kujiandaa.
Ni generali mdogo aliyekabidhiwa jeshi na kupewa cheti hicho kikubwa na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ni safari ya Siri aliyokuwa akiifanya na alikuwa kama abiria katika gari hilo linaloelekea wilaya ya kilosa mkoani morogoro.
"Tushafika sehemu ya tukio afande". Ilisikika sauti kutoka kwenye kifaa cha mawasiliano kutoka kilichokuwa kwenye sikio la generali mtei.
"Hakikisha mnaangalia kama bado wapo kwenye hilo eneo". Alisema kisha kukata mawasiliano hayo.
Aliangalia saa yake ya mkononi na kisha kupiga simu upande wa pili.
Gari lilisimama katika kituo cha Basi ruaha .
"Ndiyo naelekea sehemu ile mheshimiwa nitakutaarifu kinachojili." Alituma ujumbe mfupi baada ya kukata simu aliyokuwa akiwasiliana.
Generali mtai alishuka katoka ndani ya basi na kufata uelekeo upande wa magharibi akielekea katika safu za milima ya udzungwa.
Kijani kilipamba safu hizo na huenda ndio chanzo cha kuvutia wageni katika milima hiyo.
"Kikosi Bravo..jiandaeni kwa ajili ya kuvamia maadui." Alitoa amri kupitia kifaa cha mawasiliano.
"Ninaona watu zaidi ya kumi wameshika silaha nzito na huenda ni moja ya kundi la magaidi wanaoisumbua nchi yetu." Alipeleka taarifa kwa kikundi bravo kikae tayari
"Tupo tayari kwa kazi afande. Toa amri yako tuwamalize Hawa magaidi."
Kikundi bravo ni moja ya kikosi kinachoongozwa na kipo chini ya generali mdogo mwenye miaka 38, generali mtai. Alikuwa kijana mrefu na mwenye sura nzuri ya kuvutia huenda aliingia kwenye kazi ya jeshi kimakosa lakini kazi yake ilionesha kwamba anafaa kwa kazi hiyo. Kazi yake ilikuwa sio mbovu kama magenerali waliopita, ambao waliishia kumaliza madaraka yao bila kukumbwa na maadui wengi kama generali huyu.
Umaarufu wake wa kuweza kuvamia maadui bila Adui kujua anaweza vamiwa vilienea nchi nzima na kikosi chake cha bravo kiliweza kufanikisha umaarufu wake uweze kuenea kwa kasi baada ya kufanya uperesheni zaidi ya kumi akiwa afisa kadeti na umri wa miaka 23.
Aliweza kupanda madaraja kwa haraka na kasi isiyokuwa ya kawaida. Na hata wazee waliotangulia kazini walikuwa Hawana budi kusifu utendaji kazi wa kijana huyo. Na heshima ilibidi apewe kama mtu muhimu jeshini haikujalisha umri wake mdogo. Hata Mzee wa miaka 50 ilibidi ampe heshima yake.
Alipewa cheo na raisi Aloyce kasmili baada tu ya kupata nafasi hiyo. Alihitaji vijana wanayoipenda nchi yao na sifa za kijana huyo ziliweza kumfikia toka alipokuwa waziri mkuu miaka 15 iliyopita.
Alikuwa juu ya jiwe moja kubwa lililoko juu ya mlima huo na bondeni kulionekana mahema yaliyotengenezwa kama kambi ya kikundi hicho cha ugaidi.
Upande wa mashariki bendera nyeusi yenye maneno meupe ilikuwa ikipepea na kusambaza ujumbe wa maneno mawili tu yaliyokuwa yakisomeka "ISLAMIC STATE".
Aliweza kuona maneno hayo kwa kutumia kifaa cha kuona mbali yaani hadubini.
"Wako mita 80 toka nilipo mnaweza kuwafikia ndan ya dakika nane toka hapo mlipo. Mnaweza sogea taratibu sasa." Alitoa amri generali mtai.
"Wazi afande tunasogea." Ilisikika sauti ya kike upande wa pili wa kifaa cha mawasiliano.
Upande wa mashariki wa milima ya udzungwa watu wasiopungua kumi walikuwa wakisogea taratibu baada ya kupokea maelekezo toka kwa kiongozi wao mwanamke aliyekuwa mbele akitumia ishara ya mikono kuwagawa wawili wawili , na yeye kubaki na mmja wa mwanamke aliyevalia kombati ya kijeshi yenye rangi ya kijani na nyeupe.
Wote kumi walikuwa wameendana na mazingira yao hivyo iliwia vigumu kuwatambua kama ni watu hasa ukiwa umbali wa mita tano.
Majani ya miti na rangi nyeusi walizopaka nyuso zao ziliwaficha bara bara.
Wawili walishuka taratibu toka upande wa mashariki na kuweza ingia moja ya hema lililokuwa karibu na safu za mlima huo.
"Tumeweza ingia ndani ya hema mojawapo afande. Kuna masanduku mengi sana ndani ya hili hema . Na ni ajabu hatujakuta mtu akilinda hapa zaidi ya huyu mtu aliyelala humu ndani." Alisema mmja wa wanajeshi wale wawili na wote walikuwa wanawake.
"Hakikisha mnammaliza haraka iwezekanavyo nimewapa nafasi ya israeli mtoa roho yoyote aliye mbele yenu ni halali yenu." Yule mwanamke aliyekuwa akipewa maelekezo na generali mtai alitoa maelekezo ya mwisho.
"Sawa afande ". Alijibu na kisha kumsogelea yule mtu aliyekuwa amelala fofofo katika kitanda kilichokuwa kinaning'inia katika chumba hicho.
Alimpiga na kitako cha bunduki aina ya COLT REVOVLING RIFLE M1861 SPRING FIELD. Inayoweza kutoa risasi sita kwa mkito mmja endapo utagusa kifyatua risasi.
Baada ya kumzima huyo mtu waliweza kuona Nini kipo ndani ya masanduku yale.
Wote wawili walipatwa na mshuko kwa kuona kilichokuwepo ndani ya masanduku yale.
"Haiwezekani". Alisema mmja ya wanawake wale walioingia ndani ya hema hilo
"Hakuna kisichowezekana duniani, labda ushasahau ile operesheni yetu ya nchini congo.? Aliuliza mmja ya wanawake wale
"Nakumbuka lakini hawakuwa na silaha nzito kama hizi. Na haiwezekana kuwe na vichwa vya watu ndani ya masanduku. Hawa watu ni makatili kiasi hiki kuliko hata M23." Alijibu mwanamke mwengine
"Sasa nimepata sababu ya kuwaangamiza wote." Aliwaza mwanamke yule
"Irene ni Naomba niachie yoyote tutakaye kutana naye mbele yetu." Alisema mwanamke yule.
"Usijali maggie nipo nyuma yako. Kumbuka nimekuzidi idadi ya watu niliowaangamiza toka tumekuwa pamoja katika kikosi chetu.
"Najua sasa niache nikulipe tuwe Sawa sawia sawa afande." Alisema magreth ambaye Irene alimuita maggie
"Nataman generali mtai aone ubora wangu kama alivouona ubora wa mkuu wetu wa kikosi...black Angela Aliwaza magreth na kutoka nje ya hema taratibu na kuzunguka hema lingine na kukuta kuna ulinzi mkali kuliko hema ya kwanza waliyoingia
"Walifyatua risasi zao kwa ustadi wa hali ya juu bila kumkosa aliyeelekezewa mdomo wa bunduki. Watu saba walianguka kwa pamoja na eneo hilo kuwa kimya kwa muda.
Viwamba sauti vilivyokuwa mbele ya midomo ya bunduki hizo aina ya M1860 SPRING FIELD. Viliweza kuzuia kusikika kwa sauti za risasi na kuwafanya waweze kuingia ndani ya hema la pili na kuangamiza wote waliokuwa ndani ya hema hilo.
Wanawake wengine waliweza vamia magaidi waliokuwa wakifanya dolia mlima hapo na kuweza kuangamiza hatari yoyote.
Wanawake nane walikutana katikati ya kambi hiyo na kushusha bendera nyeusi yenye maneno meusi na kuichoma moto.
"Black Angela sikuoni kati ya hao nane. Upo wapi Naomba ripoti ulipo." Generali mtai aliyekuwa juu ya jiwe akiangalia yaliyokuwa yanaendelea ndani ya kambi hiyo aliongea kwenye kifaa cha mawasiliano.
"Nipo upande wa kaskazini wa mlima . Kuna gari aina ya fuso lenye rangi ya kijani linapandisha uelekeo wa kambi hiyo." Aliripoti mwanamke yule ambaye jina lake aliitwa black angela
Jina hilo alipewa na generali mtai baada ya kuvutiwa na kasi ya mwanamke huyo ya kuweza kumvamia adui bila ya adui kujua kama amevamiwa. Alikuwa kama usiku wa giza ambapo vivuli vyote hukosa kujidai kama ilivyo mchana.
Alikuwa mwanamke jasiri na mwenye sura nzuri ya kuvutia na mwenye akili kubwa juu ya mapambano ya kivita. Alikuwa na urefu wa futi tano na mwenye shepu zuri la kuvutia lililokuwa limechoreka kwenye kombati ya kijeshi aliyovalia. Na kifua chake kilikuwa cha wastani na sio kama mithili ya bibi titi.
Wanajeshi wenzake waliochini ya amri yake walivutiwa na ukarimu wake wa kuongoza kikundi hicho na kutamani kuwa kama yeye.
Na huenda siku moja wakaja kuwa watu maarufu nchini kama ilivyo kwa generali mtai. Na uzuri aliokuwa nao ulimvutia generali mtai na kufanya kutengeneza kikosi hicho cha wanawake kinachoongozwa na mwanamke anayempenda.
"Nasogea hapo ulipo kukupa msaada, do not make a move kabla sijafika. Dakika tano ntakuwa hapo." Sawa afande alijibu black angela kwa sauti yake nyororo.
Aliweza kuliona Gari likipandisha mlima huku akiwa anatumia mawe makubwa kujificha .
"Black angela jiandae kuvamia sitoweza fika haraka ulipo inaonesha ameshtuka kuona ukimya katika kambi na ameongeza kasi ya Gari.
Phfuuu....
Mlio wa risasi ulisikika na gari liliweza poteza muelekeo na kuanguka upande wa pili wa maporomoko ya milima ya udzungwa.
Generali mtai alionesha ubora wake wa kutumia silaha za masafa marefu kumuangamiza dereva wa Gari hilo.
"Tunahitaji kujua nyuma ya gari hilo kuna nini. Nahitaji kikosi chote kije upande wa kaskazini". Alitoa amri kwa wote na kila mmja alisikia maelekezo katika kifaa cha mawasiliano
"Sawa afande". Walijibu kwa pamoja wale wanajeshi nane waliokuwa kambini wakiteketeza bendera na kumalizia kuwaua maadui hao waliokuwa wameziba nyuso zao kwa vitambaa vyeusi.
Black angela na mwenzake walisogea taratibu mpaka sehemu Gari lilipoangukia na waliweza kuona baadhi ya watu wakitoka huku wameshika silaha nzito.
Walianza kufyatua risasi kwa fujo na kuzua taharuki kwa watu waliokuwa chini ya mlima huo wakifanya shughuli zao. Watalii walizua taharuki na walitoka katika maporomoko hayo ambako Gari liliangukia.
Watu saba Wenye rangi nyeupe walikufa pale pale ndani ya maporomoko ya maji hayo. Baadhi ya waliokuwa wakipiga picha waliweza chukua picha za tukio hilo na waliokuwa wakitumia mitandao ya kijamii kujirekodi kama Instagram kwa kutumia insta live waliweza pata wafuasi wengi wenye mshtuko wa kile kinachoendelea.
Video ya majibizano ya risasi ilisambaa kwa kasi baada ya watu kutumiana kwa kila namna ya mawasiliano. Nchi ilijaa taharuki na vyombo vya habari vya Tanzania viliweza ripoti tukio hilo.
"AYO TV ILIWEZA RIPOTI KWA KINA TUKIO HILO BAADA YA KUTUMA TIMU YAKE YA WAANDISHI WA HABARI AKIWEMO MWANZILISHI WA CHOMBO HICHO AMINIKA KILICHOANZISHWA MIAKA YA 2014.Chombo hiki kiliaminika na nchi nzima kutokana na umahili wa kazi zake na ukweli wa taarifa zake. Hivyo wengi walikuwa wakisuburi taarifa toka chombo hicho.
Waandishi wa habari walifika kwa usafiri wa helikopta iliyoandikwa AYO TV na kutua katika eneo la tukio. Waandishi wa habari ni moja wa watu waliothaminiwa katika uwanja wa vita.
Huenda ndio ilikuwa sababu ya generali Mtai na kikosi chake kuwapa ulinzi huku wakiwa wnachukua majibizano ya risasi yaliyokuwa yakitokea chini ya mlima huo ambako magaidi wale waliweza kutumia silaha zilizokuwa ndani ya Gari hilo kujibu mashambulizi.
"Ainesta , Magreth, Abigail , na Irene Naomba mbaki huko huko juu kuweka ulinzi. Usiruhusu Polisi yeyote ashuke huku chini huu sio uwanja wao wa vita siitaji kupata Majeruhi yoyote kutoka upande wetu." Alitoa amri huku akifyatua risasi toka kwenye silaha yake ya masafa marefu.
Magaidi waliotoka na kuanza majibizano ya risasi walikuwa zaidi ya kumi na kupitia camera zinazoitwa drone ziliweza chukua tukio zima mubashara na kuonesha watanzania kinachoendelea.
"Nilijua tu nchi yetu haipo Salama toka ile siku walipotaka kumuua raisi wetu mpemdw kasmili siku ya kampeni ". Ali andika mmoja ya wananchi anayefatilia mubashara kwa mtandao wa YouTube.
"Umeona wale wazungu nje ya maporomoko ya maji?
"Ni wazima kwan mbna kama wamekufa" alijibu mmja wa wafatiliaji wa taarifa hiyo
"Ndio maana walitaka kumuuua raisi wetu ugenini.
Watu waliendelea kuandika maoni yao na kusababisha chombo ya habri hicho kupata wafuasi wapya waliotaka fatilia tukio hilo.
Vyombo vikubwa duniani viliweza tumia video za chombo hicho cha AYO tv kuripoti tukio hilo linalohusiana na tukio la mlipuko uliotokea nchini colombia katika mji Mdgo wa uraquein.
"SHOOTING IS HAPPENING RIGHT NOW AT UDZUNGWA MOUNTAIN IN MOROGORO TANZANIA. A MILITARY TEAM SEEMS TO TAKE CONTROL OF THE TERRORISTS TERRITORY. THE BURNT FLAG OF ISLAMIC STATE HAS BEEN FOUND ON THE PREMISES. Kililipoti chombo kikubwa duniani BBC.
Dunia nzima iliweza ona tukio hilo la majibizano ya risasi na kikosi cha ulinzi wa nchi kilifika eneo la tukio kuzuia watu wasisogee karibu na eneo kwa tukio. Na waziri wa mambo ya ndani alikuwepo wakati huo akishuhudia kinachoendelea.
"WANAJESHI SITA WANAWAKE NDIO WANAOPAMBANA NA KIKOSI HICHO WAKIONGOZWA NA GENERALI MDOGO KUWAI KUTEULIWA NA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA... GENERALI MTAI." Kililipoti chombo cha AYO tv na kuonesha ukakamavu wa wanawake hao waliokuwa wakitumia silaha kwa ustadi wa hali ya juu.
Black angela nikinge nataka niingie ndani ya Gari tumeweza wasogeza mbali na gari lililobeba silaha." Alisema generali mtai.
"Sawa afande". Alijibu black angela kwa sauti ya juu na drone iliyokuwa inachukua matukio iliweza chukua sura ya mwanamke huyo. Aliyekuwa na shabaha kali.
"Jamani naona kama maigizo". Aliandika mmoja ya watazamaji wa AYO tv
"Yangekuwa maigizo hapo sidhani kama ungeona hao wazungu waliokufa hapo nyuma ya gari ".
"Wanawake kumbe tunaweza. Natamani kuwa kama huyo dada aliyesema sawa afande". Aliandika ujumbe mwanamke mmoja anayejiita kim wajah na kusababisha watu wengi kupenda ujumbe wake.
"Cleopatra sogea hapa haraka uondoe miili ya Hawa watalii. Dunia nzima inaangalia tumeshapoteza uaminifu mpaka sasa wa Amani kwa watalii wetu." Alisema generali Mtai na kusogea mbele kufata uelekeo wa magaidi watatu waliosalia.
"Tuna dakika kumi za kumaliza operesheni hii . Imetuchukulia muda mwingi sana kuimaliza. Nifateni." Alitoa maelekezo na wanawake wanne walimfata akiwemo black angela.
Waliweza kusogea kwa kasi kuwafikia huku virile vyao vya shahada vikiwa katika kifyatua risasi tayari kwa kuangamiza maadui.
Wale magaidi watatu walikuwa wakikimbilia upande kusini mwa safu za milima ya udzungwa. Waliweza kuingia kwenye miamba iliyochongwa kwa mkono wa mwanadamu. Lakini mmoja wao alibaki akijibizana risasi na kikosi cha bravo kilicho chini ya kamanda generali Mtai.
Generali mtai aliweza kuona kuwa kuna baadhi wameweza jificha ndani ya pango hilo.
"Mbio za sakafuni huishia ukingoni, mwisho wenu umefika". Alisema generali mtai na kisha kuchukua silaha inayorusha kombora masafa marefu na kuangalia kwenye kilengeo.
Na baada ya dakika chache makombora mawili yalitoka kwa kasi ya ajabu na kuacha moshi ukimfunika generali mtai. Mwili wake uliweza kumsaidia kusimama wima baada ya kufyatua kombora hilo.
"Aaah Allah wakbal".
Ilisikika sauti ya watu waliokuwa ndani ya pango hilo na ukimya ulitawala baada ya moshi ukiochanganikana na vumbi kufunika mdomo wa pango hilo.
Kamera aina ya drone iliweza sogea karibu na pango lile na kuonesha muonekano wa pango hilo baada ya kupigwa kwa bomu hilo.
Mdomo wa pango hilo ulikuwa hauonekani , mawe makubwa yaliyoporomoka kutokana na mlipuko yaliweza zuia mdomo wa pango hilo.
"Nadhani wameshaangamizwa wote". Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa kijamii wa instalive alitoa maoni yake baada ya kuona watu wapo kimya kusubiri kinachojili.
"Bora wafe tu hao magaidi, wanatishia amani yetu nchini." Ujumbe mwengine ulisomeka hivyo na kusababisha watu wote kuwa na mawazo ya aina moja ambayo ni kuangamizwa kwa magaidi hao.
"Aurelia kahakikishe kama wameangamizwa wote " alitoa amri na mwanamke mmoja aliyekuwa ameshika silaha yake kikakamavu alisogea taratibu na kwenda kuhakiki kama adui wote wameteketezwa.
"Afande kwa jinsi ilivyo itabidi tutoe mawe yanayozuia mlango wa pango hili."
"Lakini huyu wa mwisho amefariki.". Alijibu Aurelia baada ya kuona mkono ukiwa peke ake na kichwa kikiwa mbali na mwili.
"Njia uliyotumia sidhani kama itapendezwa mbele ya macho ya magaidi. Umeweza kuongeza Hasira juu ya nchi yetu. Hawatalifumbia macho shambulizi letu la leo." Alisema black angela huku akisogea taratibu na kumsaidia aurelia kusogeza jiwe kubwa lililokuwa mlangoni mwa pango hilo.
"Haijalishi black angela kinachohitajika kwa sasa nikuwaonesha kuwa hatutolifumbia macho kundi lolote la kigaidi litalotishia Amani nchi yetu. Nitahakikisha kikosi chetu cha bravo kinatekeleza hilo hata kama tutatumia njia hatari za kivita.' Alisema generali mtai
"Afande hakuna masalia ya mtu yeyote humu ndani." Alijibu Christina baada ya kuingia ndani kuangalia mabaki ya magaidi hao.
"Haiwezekani hakuna tone hata moja la damu. Inawezekanaje? Aliuliza generali mtai na kumtazama black angela.
"Afande this is war. Kuna mengi sana yanaonekana kwenye uwanja wa vita huwezi jua wametumia njia gani mpaka tusiweze ona masalia yao au hata ya bunduki walizokuwa wakijibia mashambulizi." Alisema Christina mmja ya mwanamke mwanajeshi mweusi mwenye midomo myembamba na macho makubwa.
"Afande njoo ujionee mwenyewe." Alisema christina huku akiwa ameinama chini akishika unga unga wenye rangi nyeusi.
"Ninajua wengi wenu hamuwezi jua maana ya unga unga huu. Ila kuna Siri kubwa iliyopo juu ya kupotea kwa watu Hawa bila kuacha hata tone la damu wala silaha walizokuwa wakitumia."
"Huo unga unga ni nini? Aliuliza black angela Huku aurelia akimkazia macho christina aliyesimama kujielezea.
"Moja ya maadui tuliopigana nao mwaka jana katika msitu mmoja kule kongo, alikuwa na unga unga wa namna hii."
"Aliweza jipaka katika paji lake la uso. Na kwenye mikono yake, baada ya dakika chache alipotea mbele yangu kama upepo. Nilidhani naota lakini nadhan ndicho kilichotokea hapa siku ya leo." Alisema christina huku akiwa na tabasamu.
"Afande kuna kitu kimepelea kwenye kundi letu. Tunahitaji tuwe na mbinu mbadala. Tukiendelea hivi hivi basi hatuwezi shinda hii vita." Alishauri christina
"Nimeanza kukuelewa christina". Alisema aurelia huku akimwangalia black angela aliyekuwa ametulia akiushika shika ule unga unga wenye rangi nyeusi.
"Nadhani nimepata suluhisho la tatizo hili". Alisema black angela baada ya ukimya mrefu
"Kuna mtu anaweza kutusaidia katika hili." Aliongea black angela huku akimuangalia generali mtai.
"Ni nani huyo anayeweza kutusaidia? Aliuliza generali mtai na kuwafanya wote watano waliokuwepo kumtazama black angela.
"Nitakutaarifu generali tukiondoka katika eneo hili. Ila kwa kifupi kwakuwa tumewapoteza siku ya leo, kuna Mzee mmoja maarufu jijini dar es salaam ataweza kutusaidia katika hili." Alisema black Angela huku akiiweka silaha yake begani tayari kwa kutoka nje
"Mzee mpitekule". Alisema jina na kumfanya christina kushtuka na kumuangalia black angela kwa udadisi.
"Unamfahamu Mzee mpitekule? Aliuliza christina kwa shauku
"Ni nani asiyemfahamu Mzee mpitekule wa mizimu ya ndindile. Hata watoto wadogo wanajua kazi ya huyu Mzee hajawahi feli.
"Japo kutokana na ubora wake wa kazi na kuhutaji pesa za kujikimu watu mbali mbali na hatari huenda kwake kuomba msaada hasa waharifu.
"Na kwakuwa anahitaji pesa na pesa Ndiyo kitu pekee cha kuweza kumshawishi Mzee huyu Basi ataweza tusaidia katika hili." Alisema black angela
"Nadhani sasa tunapambana na watu zaidi ya watu. Itabidi tuwe kama wao ili tuweze mshinda adui wa aina hii." Alisema generali mtai aliyekuwa ameinama chini akichukua taarifa anazopewa na mwanajeshi aliye chini yake. Na alishikwa na butwaa kuwa black Angela anaujua ulimwengu wa miujiza kama kiganja chake cha mkono.
"Pia Naomba tuongee zaidi juu ya hilo jambo." Alisema generali mtai na kuwafanya wanawake wanne kumwangalia black angela kwamba una la kujieleza kwa taarifa ulizotoa.
"Sawa afande." Alijibu black Angela bila kuwa na wasi wasi kama wanajeshi wenzake walivojawa na wingu la woga
Kamera aina ya drone iliwachukua watu hao sita waliokuwa wakitoka ndani ya pango lililokuwa limefunguliwa kwa wakati huo.
"KIWILI WILI CHA MMoJA WA MAGAIDI KIMEPATIKANA KATIKA ENEO LA TUKIO HUKU BAADHI YA SEHEMU ZAKE ZA MWILI IKIWEMO MIKONO NA MIGUU NA KICHWA KIKIWA MBALI NA KIWILI WILI. HAIJULIKANI WENGINE WAWILI WAMEENDA WAPI KWAKUWA HAUKUPATIKA HATA UNYWELE WA KICHWA CHAO. Alilipoti mwandishi maarufu wa AYO tv na kusababisha watu kuzua taharuki na kushtushwa na taarifa hizo.
Polisi wa dolia waliweza safisha eneo la tukio kwa kuondoa miili ya magaidi na kuhakikisha haribaki hata ganda moja la risasi zilizotumika katika uwanja huo Mdogo wa mapambano.
Helikopta ya kijeshi iliweza karibia katika kambi ya magaidi na mmoja wa mwanajeshi aliyekuwa ndani ya ndege hiyo alidondosha Kamba nene iliyokuwa imefungwa kwenye upande mmja wa chuma cha helikopta hiyo.
"Ni muda wa kurudi katika kambi yetu ya kijeshi iliyopo dar es salaam." Alisema generali mtai huku akishikilia Kamba hiyo na kukwea kwa kasi ya ajabu mpaka ndani ya helikopta hiyo akifwatiwa na kikosi chake cha wanawake 10 waliobobea katika kazi hiyo.
Black angela aliyekuwa wa mwisho kuning'inia katika kamba hiyo, aliweza toa bendera yenye rangi nne yaani blue ,nyeusi, njano na kijani na kuiacha ipepe huku wakiondoka taratibu katika eneo la tukio.
Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali waliweza chukua tukio hilo na kuwafanya wananchi kulisifu jeshi la nchi yao ya Tanzania.
"Baka Baka hawanaga kazi mbovu." Alituma ujumbe mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Makubi Madilisha katika mtandao wa kijamii wa YouTube.
"Wamekunywa maji ya bendera hao wako tayari kufa kwa ajili ya nchi yetu. Natamani na mimi nife kwa ajili ya kupambania Amani ya nchi yangu. Naipenda Tanzania." Aliandika mtumiaji mwengine wa mtandao wa kijamii wa YouTube na kusababisha watu wengi kumuunga mkono.
Alionekana raisi Aloyce kasmili aliyekuwa ndani ya ndege aina ya BOEING MILLITARY 458 iliyokuwa ikipasua anga na kupita katika bahari ya pacific kuliacha bara la amerika kusini na kuelekea katika bara lililokuwa kwa teknolojia kama ilivyo kwa Mabara mengine. Bara la Asia . aliweka simu aina ya kishikwambi huku akitazama mawazo ya wananchi kupitia mtandao wa YouTube.
"Tunahitaji kukutana na raisi wa china Hedaejin siku ya leo. Kwa sasa Amani ya nchi haiko shwari nahitaji watu watakao nisaidia katika kutatua shida hii." Alisema rais kasmili akionesha kuwa alikuwa anaongea na mtu kupitia mawasiliano ya njia ya video ya Skype.
"Hakuna Shaka mheshimiwa raisi nitahakikisha nchi inakuwa salama." Alisikika sauti ya mwanamke upande wa pili na kuonesha kuwa atafanya kazi kama inavotakiwa.
"Nakutakia utendaji mzuri wa kazi mheshimiwa makamu." Alisema raisi Aloyce kasmili na kukatiza mazungumzo hayo ya njia ya video.
"Tunakatiza katika anga la nchi ya Syria mheshimiwa raisi." Ilisikika sauti ya rubani na kumfanya raisi aangalie nje kupitia dirisha dogo la ndege hiyo.
Pipipiipi
Ulisikika mlio wa radar iliyokuwepo kwenye ndege hiyo.
Raisi Aloyce kasmili alishtushwa kwa alichokiona na kumfanya afumbe macho na kufanya maombi yake ya mwisho.
Je ni nini kilimfanya raisi kasmili afanye maombi yake ya mwisho.
Je atapita salama katika anga la nchi ya Syria?
MWISHO WA SEASON 1.
KUHUSU MWANDISHI
Felix Michael Menda ni mwandishi wa vitabu mbali mbali vya kazi ya fasihi kwa lugha ya kiingereza na kiswahili katika Nyanja mbali mbali zikiwemo riwaya , simulizi fupi na mashairi mbali mbali kwa lugha ya kiingereza na kiswahili. Mpaka sasaunaweza kupata nakala yako ya simulizi ya kiingereza inayoshika namba moja katika website ya www.freeebooks.com (NO ONE LOVES GUSTAV) Kwa muda wa miezi sita mpaka sasa. Na MZALENDO Ni kitabu chake cha kwanza cha Kiswahili kinachohusu siasa ya baadae miaka ya 2070 kutoka sasa 2023 chenye visa vya kimapenzi na mauaji ya kutisha.
ONYO
Hairuhusiwi kunakili kazi hii bila idhini ya muandishi, na kazi hii ni kazi ya kufikilika. Majina na sehemu zilizotumika ni ubunifu wa kazi ya fasihi hivyo haihusiani na mtu yeyote yule hai ama amefariki, wala haihusiani na shirika lolote lile.
MAWASILIANO
NAMBA YA SIMU WHATSAPP NA KAWAIDA +255627096853
BARUA PEPE: mendafelix06@gmail.com
Links for My English stories: www.freeebooks.com(NO ONE LOVES GUSTAV) Written by FELIX MENDA