Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

mpenzi wa mzimu

🇰🇪Kavita_Benjami
--
chs / week
--
NOT RATINGS
5.7k
Views
VIEW MORE

Chapter 1 - 1.Asili ya Jadi

Ni baada ya miaka kumi na mitano katika kijiji cha wasakatonge ambapo wazee na majagina wa jamii wameketi kitako, kujadili tatizo ambalo laekea kuingiza jamii nzima katika kisima chenye kina kirefu .Hawajui la kutenda na si kutenda tu bali ata pahali pa kuanzia wazee wenyewe hawapajui... ,Wazee wezangu, kwa heshima yenyu ,haya ni mauti yanatukondolea macho na bila shaka huenda yakaturamba sisi sote katika kijiji hiki,suluhu isipopatikana.

Bw. Wakalekye ,sisi sote twaijui suluhu ya janga hili ni nini, walakini pana moshi ufukao toka mlimani, na hapo ndio kizungumkuti kilipo.

Moshi mlimani ,maana yake ndio nini mzee mwezangu,Kithuku?.Bila shaka ,Wakalekye jibu la tatizo la jamii hii na suluhisho ya matatizo haya limo katikati yetu sisi sote.Mwanamwali sharti atolewe kafara katikati ya vilima vya ardhi hii ya mababu zetu na watakao shiriki katika kufanikisha kafara hiyo lazima miungu ya mababu wetu wawataje kwa jina zao .....

Na jina zao zatakiwa kuwa zishatambulika katika kipindi cha majuma matatu kuanzia leo ,Hao ndio watatueleza msichana bikira atatoka katika jamaa ipi miongoni Mwetu, Na wazazi wa binti atakaye changuliwa lazima walirithie hili pasipo pingamizi zozote ,la si hivyo basi kijiiji ...

Ni bayana kuwa ukoo wa Baa mwashetani ndio umekuwa ukitawala na kulishunghulikia maswala ya uongozi wa jamii hizi tangu jadi za hayati wazee wetu.Ni pendekezo langu kwenu wazee watukufu wezangu,Bw Wakalekye auridhi uongozi wa marehem baba yake.

Baada ya kutawazwa na kula kiapo cha kuilinda mila na tamanduni zetu basi ,atashirikiana na wezake kututafutia binti atakaye tolewa kama kafara ili kuiokoa jamii yetu,.... Na wazee wezangu hili lapaswa kufanyika kabla ya mwezi wa tisa kwani sote twafahamu kuwa kafara yaitajika kabla ya mwezi wa kumi na mbili ,kipindi ambacho mwezi utachomoza ... Farashee akasisitiza."Ayee hiyee avaoi syitu!!!! "kujiapa kwa jamii.nitaliwazia jambo hili la akumridhi maremu mzee Magwada ambaye na baba yangu ila kwa mashariti nitakayo wapa iwapo mtitimiza,...

Magwada alikuwa kiongozi mtukufu na aliyefanya nasaba yao kuheshimika zaidi katika janibu zake.Alijaliwa na maghulamu kumi na saba na mabinti ishirini na wanne ,kwa pamoja alikuwa na jeshi lake imara na stadi la kumwezesha kutekeleza jambo lolote alilolirithia nafsini mwake.Walio ona balaa bin belua ni wake wake waliokamilisha juma moja.Walimpenda na kumhenzi kwa nyoyo zao, kila mmoja akiwa na wajibu wa kupika siku tofauti na kuiadika meza iliyokuwa kwenye "Thome" kabla ya saa mbili unusu usiku na chakula chenyewe kiliitajika kuwa moto pamoja sharubati iliyotakiwa kuwa vuguvugu.

Kilicho wasumbua na kuwashangaza hawa wana wa 'jezebel' kama alivyozoea kuwaita wake zake,katika himaya hii vyakula vya uswahilini alomaarufu kama 'swahili dishes' vilikuwa marufuku hapa.Na si marufuku tu kwani viliogopwa ndovu aliye jifungulia katika shamba la mihindi. ' Natumai wajua matendo yake wakati zao lake nimekabiliwa na adui au ata kukaribiwa na adui '. Kadri jinsi walivyo mpenda ndivyo walivyo kutana na vikwanzo mbele yao ,Mke angepika chakula kitamu ,na kuandika meza ila angepigwa na bumbuwazi alipojaribu kujisitiri kwenye kochi ili ashiriki katika ule mlo ,Magwada angeita jina la mke aliyetaka kuwa naye usiku ule na kumshirikisha katika kula chanjio pamoja. kweli alifahamu kuwa ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona.

Katika ufalme huu ilikuwa isha bainika wazi kuwa mzawa wa kwanza katika nasaba ya utawala ndiye angeridhi mamlaka kutoka kwa baba na hivyo kuutwa uongozi. mwana wa kwanza kati ya wana arobaini na mmoja ,alikuwa Binti kwa jina Lecho. Bibti huyu alihenziwa na babaye kwani yeye ndiye aliye mvusha kutoka kiwango cha "kivisi" hadi kiwango cha "mtumia".Lecho alikuwa idhibati tosha kuwa Magwada alikuwa mlengaji shabaha hodari na aliye fahamu kulitumia bunduki lake vilivyo na kumwanga risasi vipasavyo.

Kulingana na mitalatala ya uongozi,amali na utamaduni wa jamii ya wasakatonge ,Lecho ndiye mridhi aliye mfaa babake.Ni binti aliyezaliwa wakati baba yake alikuwa Ghulamu na kutokana na mchezo wake na binti ya mtu akamringa mimba na kisha kampewa mwana pamoja na mamake ,hivi Magwada akajitwaalia mke na mwana katika umri wa miaka kumi na sita.

Kando na mama yake lecho ' veronica' ,Magwada alikutana na binti wa kinyamwezi kutoka Zanzibar na kumuoa kama mke wa pili.mke huyu alijaliwa na mabinti sawia na mke wa kwanza , Hali hii ilileta mzozo kati yao na mume wao alitaka sana kuzaliwa mwana wa kiume ,Akaoa wake hadi wakalijaza juma, na hali ikawa vile vile ni mabinti tu hadi akawa na mabinti kumi na wawili..

Kwa kudura za Maulana au ukipenda miungu jinsi magwada alivyoita,Veronica kipindi hiki kiberiti kilikuwa kimetingizwa vilivyo ,vijiti vikapata joto na kuuwasha moto ,uliokuwa umejaribishwa kwa kipindi cha miaka na mikaka pasipo mafanikio.Magwada usiku ule yaonekana alikuwa amesoma jinsi ya kupiga mkiki wa penalty pasipo kukosa au kupiga inje kutoka kwa mkufunzi maaraufu PEP GUADIOLA.

Katika nasaba ya magwada hatimaye pakazaliwa mvulana, haialisi kuwa usiku ule miezi kumi na moja kabla ya ujio wa mwana huyu aliye pewa jina Wakalekye .baada ya kuandikiwa meza na mke wake wa tano ,alikuwa ameamua kushiriki kile chakula na Veronica, na ilivyokuwa ada yake mke aliyeshiriki meza naye ndiye angemsitiri usiku ule dhidi ya baridi...

Kitoto hiki kilifanyiwa viviga vya kawaida kulingana na mila na tamanduni za jamii ya wasakatoge na baadaye kukabidhiwa wa kwa baba yake ili kitakasishwe kwa miungu ya nchi hiyo kabla hakijaaacha kulia .

wakalekye ndilo jina lililopewa kijana huyu ambaye baba yake alimthamini kama boni ya jicho lake kwani alikuwa tunu kwa ile familia , Baaadaya ya viviga kukamilika wazee na bibi za mvulana yule walitawisha kwa kumpaka mate kwenye kipaji cha uso wake ,hili alikuwa ngeni katika jamii ya wasakatonge kwa kuwa walizoea kufanya hivi kwa kila mwana hasaa wa kiume ili kumuepushia jicho la hasidi kama walivyo amini.

Ujio wa wakalekye katika himaya ya mzee magwada ,ulibadilisha vitu vingi ,kuanzia kwa mrithi wa nafasi ya uongozi, kwani Lecho sasa alikuwa amepata mpinzani wa kiume . kijiji kizima kilitarajia Mfalme wao kubadilisha sheria za uongozi ili papatikane ndia ya kumfanya Wakalekye kutwaa nafasi ya babake yake badala ya Lecho,.

we nywele za koto waliingia katika mijadala isokoma na wenye nywele za singa , kila kikudi kitoa mwelekeo wake kujaribisha kuona kama Magwada atalidhia pendekezo lao .kwa Magwada hayo yalikuwa kama kelele za chura ambazo haziwezi kumtishia ng'ombe kunywa maji,

Magwada alikishilia mtanzamo wake na sheria alizo ridhi kutoka kwa baba yake ,kuwa mwana wa kwanza ndio mrithi na iwapo ni msichana akija kuolewa ,hapo ndio swala litabadilika na kuelekezwa kwa ghulamu wa kwanza.

Lecho na Wakalekye walikuwa dungu wa toka nitoke .... Baba yao aliwapenda watoto wake wote kwa upendo wa dhati ila kwa Lecho na Wakalekye alita pondo zaidi.