Baada ya siku chache,kulitokea tatizo na si tatizo tu bali lilikuwa janga na janga kuu katika ka kijiji hichi ambacho kilikuwa ni himaya ya Mfale Magwada.Kulitokea jambo la kushangaza kwani watoto wa kiume walianza kupatwa na tauni ya ngozi , Ikawa ni kujikuna kila dakika baada ya ingine,kujikuna huku kuliandamana na kutokwa na vipele vilivyo kuwa nikitoa unga unga unaofanana na jivu.
Mukutano wa dhararu ulikusanywa kwa haraka haraka ili kutafuta suluhu la tatizo hilo.Kama ilivyo ada ,wazee iliwalazimu kukuna kichwa kwa muda mrefu ili kujaribu kupata suluhu.walitia na kutoa mawazo hapa na pale Magwada aliwaita washauri wake na kuwaambia watafute suluhu kwa haraka ili waokoe jahazi ambalo lilikuwa linakwama,
Wakalekye kipindi hiki alikuwa ameduwaa mwisho wa kuduwaa ,yeye alikuwa kijana wa kwanza kwa aila ile hakuwa na Bundi ila kutafuta suluhu tena ya haraka kwani ata baadhi ya watoto wa watoto wake walikuwa wamenza kuhadhirika,Mgaga alitafutwa kwa jino na ukucha na pindi alipowasili pale kiamboni kwa hayati Magwada ,ujio wake ulileta matumaini ,Wenyeji wakatabasamu na kuonesha magego,Kipindi hichi chote Wakalekye ambaye ndiye aliyeirithi fimbo ya hayata baba yake alikuwa kashika tama ,ungemuuliza moja mara mbili labda anagekuabia ni kumi na moja kutokana na hali iliyokuwa imemzingira, upande huu wazee wanazungumza naye kujaribu kuleta suluhu ,upande ule mwingine kina mama na watoto wote wanalia kutokana na maradhi yaliyowakondolea macho tayari kufungua vinywa yavyo ili kuwameza.
" Mfalme na wazee watukufu wenzangu,kuendelea kuukizana maswali hapa na pale ,swali baada ya jingine,hakujaleta mwafaka kwetu ,ingalikuwa vyema iwapo tutasikiliza Daktari wetu hapa aliye wasili. Labda wakuu wa miungu wamezungumza naye na wakamuelekeza ,jamani naomba tumsikilize kile atatueleza kisha tushirikiane kuleta suluhu"Makezi alisikika akihimiza .Kimya kilitanda kwa dakika kama ishirini hivi, hakuna aliye dhubutu kuzungumza , kila kiumbe ata nzi waliokuwa pale ,walitii masharti ya miungu ata kabla hayajatolewa.kipindi hiki chote Wakalekye alikuwa kimya, walimsihi azungumze si kwa kumuita na kumuuliza maswali ili kumchochea, ila kwake halikutoka hata neno moja ! .Wazee wakiongozwa na Makenzi walizidi kumuita wakalekye mmoja baada ya mwingine , walijawa na wasiwasi wakajawa na maswali chungu nzima ,wanaemtengemea kutoa mwelekeo au ata pendekezo la suluhu ya mtafaruku wao ,aliyekuwa akiwaeleza sasa hasemi lolote ila tu kuwakondolea macho kondokondo.
kumukumu! kokoko! Ndugu zangu na wazee waheshimiwa sikizeni na tena kwa makini ..... huu ndio mwaka wa kutoa kafara kwa miungu ya mababu zenyu na haya majanga yanayo wapata kwa sasa ni ishara ya kuwa bado hatujajitayarisha ili kufanikisha kafara yenyewe. Mumechelewa sana katika kufanya maamuzi ya uteuzi wa bikira atakaye tumika kama kafara na bila shaka mwakosea! wangwana wenzangu ,Kumbukeni janga likifika na likianza halina dawa bali itawa gharama mara ndufu . Itatugharimu! itatigharimu tena sana wazee wetu.kila mmoja anajua kuwa tunaitaji mwanamwali ili kutekeleza jukumu hili...
"Kimya ... kimya kila mtu na atulie!." kyalo alikatiza usemi wa mganga .kwa sauti kuu na enye wasiwasi ulioandamana na hofu ambayo ilishamiri katika uso wake.Maneno yako daktari ni kweli kabisa, ni wajibu wetu wazee tulio hapa kupendekeza maono yuliyo pewa na Miung, kuhusiana na jamii inayaopaswa kumtoa binti kwa shughuli za kafara ! tunavyojua ni kuwa muda haupo upande wetu tumechelewa tena sana .Angalieni ata sasa tanzameni mrithi wa mfalme wetu hasemi lolote wala kufanya lolote .Daktari tuangalilie kiongozi wetu amepatwa na nini cha dharura. Tusilichukulie jambo hili la kawaida huenda likatimbuka usaa na tukaja kujutia utepetevu wetu.
"Haya tulieni basi wazee ,nipeni muda wa dakiki kama nusu saa hivi na ninawasihi mniachie faragha na huyu mrithi wa mfalme wetu kabla haijawa too late .Kumbukeni ni kipindi kirefu tangu alipo nyamaza .Hapa labda pana dharura na inatuitaji tumakinike zaidi ili tuwai msaanda kabla hakijaturamba wagwana wa hichi kijiji na himaya hii. Pasiwe na shaka mfalme wetu yumo salama ila tunaitaji kumfanyia gangaganga za hapa na pale kabla ya hatari.Sasa nipeni muda naye.
"Wameenda! Wameenda"? Wakalekye aliuliza kwa sauti ya chini zaidi punde tu baada ya wazee na wawakilishi wa vijiji vya himaya ya Magwada.Kuondoka.Naam washatoka wamo mle nje .Haya nieleze kile kinaendelea Baba !.Dakitari sikiliza na usikilize vizuri .,mimi sio mgonjwa wala sina dwele lolote. Hali hii nimejitwisha mwenyewe masaa machache yaliopita kutokana na shinikizo lililo mbele yangu kama mrithi wa mfalme wa himaya hii.Wajua fika kuwa ni miezi mitano tu! Tangu kufanya matambiko ya kimpumzisha Hayati babayangu na mfalme wa himaya hii . Sijapumzika ata nikarudisha akili zangu pamoja .Natumahi kipindi cha mazishi ulikuwa hapa ,uliona jinsi Dada na ndugu zangu walivyokuwa na maneno mengi na ni dhahiri kuwa ukiona mashinzi basi kuwa kulikuwa na kuni zilizokuwa zawaka na lazima pana jivu pia mahali.
Uliona kuwa kuna baadhi ya mama zangu ,ikiwa inahafiki mimi na dada yangu Lecho kuwaita mama.hawakuwepo na mimi kama mfalme mtarajiwa sikupata habari kutoka kwao ya kutohudhuria mazishi ya Mume wao, ilihali hao ni wake halisi wa baba ! Mahari ilikuwa imetolewa kwa wakwe wa Baba ,pasipo kusaza ata tone wala peni yoyote ile , nilipigwa na Butwaaa kutowaona baadhi ya kina mama ikihalisi kuwaita mama.Kipindi hichi chote ni Lecho tu amekuwa akiwapokea wangeni na ata kushughulikia mambo ya kimsingi ambayo yamekuwa yakitendeka hapa nyumbani.
Jambo hili limechora picha isiyoeleweka vyema katika himaya hii na bila kukuficha lolote ni dhahiri kuwa kuna hatari mbele yetu kama ufalme .Sisi wana wa Magwada tulifaa kusema kwa sauti moja bali ni nini kilifanyika!.Kuna mambo ambayo Marehemu baba yangu kabla hajaanga dunia alikuwa amenielekeza yafanyike kwani ata yeye aliyaachiwa na baba yake , asaa babu yangu. Dosari lilitokea kwani kulikuwa na masharti yaliyo itajika kitimizwa katika shughuli ile. Na kama ujuavyo mashariti ya miungu ni makali na jambo hilo linanitia kiwewe sana .Kando na hilo unajua kuna dwele ambalo limeanza kukita mizizi katika hichi kijiji.
Ilianza kwa watoto wa kike sasa limeanza kusabaa ata kwa vijulanga vya kiume.Sasa nakuomba wew ujaribu kututafutia suluhisho la dwele hili haraka iwezekanavyo.Na kuhusa afya yangu sema nimeungua maradhi hatari ambayo huenda yakautwaa uai wangu baada ya miezi miwili, Dawa ni kuandaliwa kwa safari ya kwenda kule kwenye vilima vya Mumoni mle juu ya kilima cha nne kuna mti uitwao " mtiliku ".Wafunge safari wakalete mzizi wa mti ule ili niitokote kwenye chungu ninyweshe na Dada yangu Jully .Nipate kutakasika mwili na hata kijiji kipate kutakasika kwa ndwele hili kwa muda tukizidi kutafuta jamii ya kutafuta jamii ya kutupea kafara! .Watakao endea mzizi ule ni watu saba mmoja mmoja kutoka kwa watoto wa wake za hayati Magwada saba...