Wakati akina Edrian wakimaliza chakula cha jioni kwa furaha na kuelekea kwenye nyumba ambayo waliikodi kwa kutumia gari maalumu lenye kupita kwenye theluji, upande mwingine ulikuwa ni wakati wa aidha kuziweka wazi mbichi zilizovundikwa. Yaani ulikuwa wakati wa kuyaleta marefu kwenye ncha yake...
Allan aliendesha gari mwendo wa saa moja na robo baada ya kumpitia Renatha eneo ambalo bado lilimchanganya. Hakujua aamini kipi kwa sababu eneo ambalo alimwambia amfuate lilikuwa nje kidogo ya mji.
"Kwa nini uko huku Renatha?" Allan akamuuliza mara alipoingia kwenye gari..
Renatha akatabasamu "sababu sipendi watu fulani hivi wanifuatilie. Hivyo nimewachanganya na sasa hawajui nilipo"
Allan akashusha pumzi akasogeza kiti nyuma akitaka kumpumzika kwa kuegama lakini maneno yaliyofuata kutoka kwa Renatha yakamshtua..
Ulijaza mafuta kama nilivyokwambia?maana tuna nusu saa tena barabarani!"
"Renatha ni michezo gani hii unacheza maana ni___" kabla Allan hajamaliza maneno yake Renatha akamvamia na kumbusu kisha akamwambia
"Endesha gari kurudi mjini ila utaingia "Dream Club" tutaongelea hapo" kisha akaketi vizuri na kufunga mkanda akimuacha Allan kwenye mshangao!
Akarudisha kiti mbele huku akitikisa kichwa na kutabasamu asielewe huu mchezo utaishaje "Sawa Renatha ninaomba tu usijaribu kunirubuni na haya mabusu yako ambayo sijui yanamaanisha nini"
"Hahaha hujui kweli Mr Nubri?" Akauliza Renatha huku akicheka
"Ndio sijui. Nilikwambia niite___ " Akamjibu huku akiendesha gari kurudi upande wa pili wa barabara ili kurejea mjini
"Allan.. Je haupendi nifanye hivyo?" Renatha akauliza kwa sauti ya chini huku akisogea sikioni kwa Allan
"Aah.. mghhh... Renee tafadhali tuko barabarani" Allan sasa akakunja vidole vyake kwa nguvu kwenye usukani wa gari maana pumzi iliyotoka mdomoni kwa Renatha ilimpuliza kwenye sikio lake na kusafirisha hisia za tofauti mwilini mwake
"Hahahhah Allan, haupendi nikubusu sawa tutaona huko mbeleni" Renatha akacheka na kurudi kuegama kwenye kiti chake akitazama nje kisha akamwambia kwa huzuni
"Najua umeniona kwenye kamera, unataka nikwambie ukweli"
"Ndio Renatha, asubuhi nilikuuliza ukakataa kabisa ukasema sina ushahidi. Sasa nina ushahidi. Unaweza kuniambia nini kinaendelea" Allan akamwambia huku akiibia kumtazama lakini Renatha aliendelea kutazama nje...
"Kwa nini hukuupeleka huo ushahidi polisi Allan?" Akauliza Renatha
"Eeeeh!!" Allan akashtuka
"Kwa nini unakaa na ushahidi wa mtu aliyevamia ofisi yako? Ungeweza kuwaita poli__" kabla ya Renatha kumaliza Allan akamkatisha
"Sikia Renee... nilitaka kukupa nafasi ya kujisafisha mwenyewe pasipo kuhusisha polisi."
"Kwa nini nijisafishe kwako aaahm?" Akamgeukia Allan
"Aaaah. ..aah sababu ni ofisi yangu ndio iliyovamiwa... hata hivyo hatuhitaji kuongea hayo...nataka nijue ukweli na yule mtu mwingine ni nani"
"Mhhhhmm" Renatha akaguna na kisha akasema, "Sawa nitakwambia"
"Kwa nini usiniambie sasa Renatha?"
"Uwe na subira Allan, unaweza kusubiri tufike napotaka kuongea nawe"
Allan akashusha pumzi na kunyamaza hakutaka kuendelea na mazungumzo tena ili asionekane anamlazimisha..
Baada ya nusu saa walikuwa 'Dream Club & Casino'. Wakaketi kwenye meza iliyokuwa karibu na eneo la vinywaji. Kulikuwa na kelele za watu na muziki. Muda ulikuwa wa usiku wa saa nne watu walikuwa wengi mle ndani
"Tutasikilizanaje hapa Renatha?" Allan akamuuliza kwa sauti
"Utanisikia wala usihofu" akamjibu kwa sauti na yeye huku akichukua mchanganyiko wa kinywaji chake na kunywa. Akaingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake akatoa kifaa kilichoonesha kuwa ni cha kuvaa masikioni akakiwasha na kuviachanisha kisha akampa Allan vikiwa vinawaka taa ya bluu..
"Vaa hii masikioni"
Allan akachukua na kuvaa huku akishangaa ni nini kiliendelea
Renatha akatoa kifaa kingine ambacho kilikuwa muundo kama pipi, akakibonyeza halafu akakiweka karibu na mdomo wake akapuliza
Allan akashtuka baada ya kupuliza kule kusikika kwenye kile kifaa na sasa hakusikia tena kelele za ndani zaidi ya Renatha
"Sasa naweza kukwambia nini kilitokea" Renatha akamwambia huku akitabasamu