Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 240 - ALIKUSHIKA?

Chapter 240 - ALIKUSHIKA?

"Nitakwambia kwa nini umeniona kwenye kamera za Ashanti, lakini sitakwambia kwa nini nafanya hivyo" Renatha akamwambia Allan ambaye alimtazama kisha akashusha pumzi na kumtikisa kichwa kumuashiria aendelee sababu yeye hakuwa na kifaa cha kuongelea.

Renatha akampa tabasamu, "Sitaki unikatishe wala uniulize maswali kwa sasa ila taratibu utajua Allan"

"Niliondoka ofisini kama kawaida nikaelekea nyumbani kwangu, lakini nikiwa hapo simu yangu iliita, nami nilipopokea nilisikia sauti ya mtu ninayemfahamu akaniambia amepewa 'assignment' hapo Ashanti. Nikamwambia sio rahisi kuingia, lakini akaniambia ataingia. Nikajua akija kuna hatari ya kugongana na wewe sababu nilikuacha na haukuonesha kutaka kutoka mapema." Akapumzika kidogo akiendelea kumtazama Allan kuona kama hisia zake zilibadilika

"Namfahamu mtu huyo vizuri, angeweza kukudhuru iwapo ungeingilia mpango wake. Sikujua ni kazi gani hasa alitaka kuifanya hapo Ashanti. Nikatoka kwa haraka na kuja hapo ofisini.. ilinichukua muda kumuona nikaamua kumfuatilia lakini yeye alinipoteza. Nikaamua kutumia liftì ya kule VIP, nilipofika na yeye akawa ameshafika tayari, nikajaribu kumfuatilia, alipoingia ofisini kwako nikaingia ili kumuonya asifanye chochote lakini wakati tukibishana tukakusikia ukirudi. Kwa sababu yeye ni mzoefu alinivuta hadi chooni na tukapitia kwa juu ambapo aliparudisha vyema hata hukuona chochote. Tukatokea ofisini kwa Alphonse."

"Kuhusu kamera ni kwamba alizichezea kidogo ili kuwapoteza walinzi." Akawa kama aliyegundua kitu!

Akainuka na kuelekea kwenye vinywaji, akaagiza na kisha akasimama kusubiri. Wakati akisubiri mwanamume mmoja akamsogelea kisha akamsalimia

"Hello mrembo, unaonaje tukipata kinywaji pamoja mmh" akamwambia huku sauti yake ikionesha wazi alikuwa ameshalewa.

Renatha akamtazama kisha akarudisha uso wake kwa muuzaji ambaye alipomaliza kuchanganya vinywaji kama alivyoagizwa akamsogezea.

"Mrembo mzuri usinifanyie hivyo" akamwambia na mara akapeleka mkono na kumshika makalio kitendo ambacho kilisababisha Renatha kushtuka na ghafla akageuka na kumrushia usoni ule mchanganyiko wa vinywaji.

"Mfyuu unanishika kama nani wewe, ukome" Renatha akamwambia kisha akaondoka

Yule mwanamume akagugumia kwa maumivu huku akishika macho yake. Wakasogea wanaume wawili waliovalia mavazi yenye rangi nyeusi. Wakaelekea kwa yule mwanamume huku mmoja akichukua kitambaa na kutaka kumfuta

"Bosi pole sana, unataka tumfanye nini huyu mwanamke?"

Yule mwanamume akajaribu kufumbua macho lakini hakuweza sababu ya maumivu. ..

"Acheni ujinga kuniuliza mimi, hamjui mtu wa aina hii huwa tunamfanyaje?" Akawafokea

Wakageuka ili kumkamata Renatha, lakini alikuwa ameshaondoka. Wakaangaza lakini hawakumuona

"Bosi amekimbia" wakamwambia

"Nyie washenzi kweli, mtafuteni huyo mwanamke la sivyo mtajutia huo upuuzi mliofanya" akafoka kwa sauti huku akiketi baada ya mmojawapo kumsogeza mahali penye kiti apate kuketi

Wakaondoka kuanza kumtafuta Renatha..

"Allan tafadhali usimfuate" Renatha akamsihi Allan huku mkono wake mmoja ukishika ule wa Allan...

"Anakushikaje bila ridhaa yako eeh?" Allan akauliza kwa hasira. Wakati Renatha anaenda kuchukua vinywaji alisahau na kutoka na kile kifaa kwenye mkono wake. Allan alisikia yule mwanamume alivyokuwa alimsemesha na hata alipogugumia maumivu baada ya kumwagiwa kinywaji. Renatha alipofika alikutana na swali

"Hakuna shida Allan ni mwanamume mmoja mpuuzi alitaka kunishika kama ana_"

"Alitaka kukushika au alikushika?" Sauti ya Allan ikadhihirisha hasira

"Allan tafadhali sio muhimu" Renatha akajaribu kumsihi

"Sio muhimu??? Ina maana umezoea eeeh?"Allan akauliza kwa hasira na kusimama

"Simaanishi hivyo Allan nachotaka kuele__" kabla ya kumaliza Renatha akashikwa mkono wa nguvu

"Tumekupata we malaya!!" akaongea mmojawapo wa wanaume wale waliokuwa wakimtafuta

Kabla Renatha hajajibu chochote ngumi nzito ilirushwa usoni kwa yule mwanamume aliyeongea na kuwashtua

"Unamuita nani malaya mpuuzi wewe!" Allan akawa kama mbogo aliyejeruhiwa

Yule mwingine akageuka kupambana na Allan lakini Renatha akamshika mkono