Edrian alikuwa akihema huku macho amefumba, kichwani kwake kulikuwa na ghasia na picha ile ikijirudia kwa namna ya kumfanya ajisikie vibaya.
"Retha samahani nafikiri tusiendelee zaidi" Ed akamwambia Aretha
Aretha akashtuka na kuvuta shuka iliyokuwa imekunjwa akashuka na kujifunika kisha akazunguka upande ambao Ed alilala.
"Rian uko salama?" Aretha akamuuliza
Ed aliposikia swali lile akafumbua macho na kumtazama Aretha
"Retha naomba nikwambie ukweli" Ed akameza mate kisha akaendelea kwa sauti ya mkwaruzo
"Nataka kuvumilia hadi nitakapoipata ridhaa ya mama, sababu nilimuahidi japokuwa natamani nikufurahie sasa, you are beautful and it's so hard to resist!" Akainua mkono na kumshika kwenye shavu Aretha
"Unanielewa Retha!"
Aretha akatikisa kichwa kukubali. Akainama hadi usawa wa uso wa Ed kisha akamwambia
"Rian kama huwezi, bado tuna nafasi ya kufanya maamuzi kwa kukubaliana sisi wawili! Hili halihusiani na mama!"
Ed hakutegemea kusikia kauli hii kwa Aretha akamtazama huku midomo yake ambayo ilikuwa karibu sana na ile yake
"Retha una_" Kabla ya kumaliza Aretha aliyakatisha maneno yake
"Rian I want to kiss you more" akanong'ona huku midomo yake ikimbusu Ed
"Retha..I .." Ed hakuweza kuendelea sababu Aretha alimbusu kwa dhati
Alipomtazama Aretha akaona alivyofumba macho akimbusu akafumbua midomo yake na kumpokea
Kama kimbunga akamgeuza kwa haraka na sasa Aretha alikuwa chini na yeye akiwa juu
"Retha, tuna uhuru wa kufanya tunavyotaka, lakini kama siwezi kutunza ahadi kwa mama sitakuwa na uwezo wa kutunza ahadi. Huyu sio mimi sitakuwa Edrian. Please help me" Edrian akamwambia Aretha huku macho yake yakimtazama kwenye kifua chake kilichovaa sidiria pekee
Aretha akatabasamu "Sawa Rian. I will help. Am sorry"
Ed akambusu na kisha akashuka kitandani na kuelekea kwenye mlango ulioingia kwenye sehemu ya bafu. Akavuta "bathrobe" akampelekea Aretha aliyekuwa bado kitandani akifikiri namna ya kupata nguo.
************
Kesho yake walipoamua kunywa chai kwenye mgahawa uliopo ndani ya hoteli, kulikuwa na kimya cha mara kadhaa kati yao. Edrian alihisi kumuingiza Aretha kwenye jambo ambalo hakuwa tayari nalo. Akawaza labda hakupenda lakini akajitupia wazi hilo mbali kwa kujikumbusha maneno aliyosema.....
Wakati akiwaza hayo Aretha yeye alimtazama Ed huku akihisi huenda ni yeye ambaye anayachukua mambo kwa wepesi
"Sijui ananifikiriaje, I hope he doesn't take my simplicity as being cheap" Akawaza
Walipomaliza, Ed akaamua kuondoa ile hali ya ukimya kati yao akaangalia saa yake kisha akamtazama Aretha
"Retha" akauchukua mkono wa kushoto wa Aretha uliokuwa mezani na kuushika macho yake yakimtazama vyema
"Ahmm" akaitika Aretha
Akashusha pumzi "naomba tuwe kama tulivyokuwa, jambo lililopita lisiibe furaha yetu"
Aretha akatabasamu na kumtazama Ed, "Asante Rian, nilidhani umenikasirikia!"
"Ooh noo Retha, siwezi kukasirika kwa sababu...ah mimi nilihisi umejisikia vibaya" Edrian akamwambia huku akimtazama machoni kwa upendo
"Hapana Rian, kuna mambo hata mama huwa simruhusu ayaingilie sababu naamini yako kwenye utashi wangu" Aretha akainama akiangalia mkono wa Ed uliokuwa juu ya viganja vyake
"Retha, nakubaliana nawe lakini kama nilivyoahidi nitaheshimu ahadi yangu kwa kuwa nilimuahidi yule anayemtunza mke wangu" aliposema akambonyeza mkono kwa juu, naye Aretha alipomtazama akamkonyeza
"Hhhhaaa ooohkay" akacheka Aretha, kisha akaendelea, "sawa nimekuelewa Ŕian"
*******
Beruya aliamka mapema sana baada ya kulala kwa muda mrefu, akaamua kutoka chumbani kwake walau mwili uchangamke. Akaelekea jikoni ambapo alitafuta nini afanye, baada ya kuona hakuna vyombo cha kuosha na mazingira yalikuwa safi, akaamua kutengeneza chapati.
Akahangaika kutafuta vitu vya kuandaa kila mahali ambapo alimuona Annie akivihifadhi jana yake. Hakujua chumba cha Annie kilipo walau angemuamsha amuulize. Akaamua kuanza maandalizi vichache alivyopata. Lakini kabla ya kuendelea sana Annie naye akaamka, akamtafutia vingine vilivyobaki kisha akaelekea kwenye usafi wa mabanda ya kuku.
Wakati akiendelea na mapishi mlango wa jikoni ukafunguliwa.