Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 229 - IT'S TOO LATE

Chapter 229 - IT'S TOO LATE

Ed akatabasamu kisha akaenda kuketi na kutazama simu yake, mlango ukafunguliwa..

Aretha akatokea akiwa amevaa gauni ambalo lilitengenezwa kwa mtindo wa 'cinderella' lakini tofauti ni kwamba hili lilikuwa fupi. Kitambaa kilichotumika kilinakishiwa kwa rangi tatu tofauti; njano, kijani na nyekundu, mapambo ya asili yaliongezwa eneo la shingo kushuka chini karibu na kifua, kulipambwa kwa shanga za rangi ya dhahabu. Eneo la tumbo kulikuwa na mfano wa mkanda ambao nao ulijazwa shanga za rangi ya dhahabu ambazo zilizishuka kwa mstari hadi usawa wa mwisho wa gauni

Kichwani kulikuwa na urembo uliotengenezwa mfano wa taji dogo lililozunguka nusu ya kichwa chake na kumfanya aonekane kama binti wa chifu. Mkononi alibeba boksi dogo.

Pasipo kujua nini kilitokea Ed akasimama akimtazama Aretha ambaye alitabasamu kisha akanyoosha mkono uliobeba boksi kumuelekea

"Hii ni kwa ajili yako Rian, niliipenda nilipoiona lakini Britney alinishawishi nichukue na yangu."

"Mhmmmm" Ed akapokea lile boksi akaanza kufungua huku moyo wake ukiwa na shauku ya kujua nini kimo ndani. Ndani ya boksi juu kulikuwa na kadi ndogo yenye picha ya vipepeo wawili kwenye mti mkavu. Akainua macho na kumtazama Aretha ambaye aliinama na tabasamu likionekana usoni

"Soma" akamwambia

Ed akaweka lile boksi mezani akafungua kadi ile na kuisoma taratibu kwa sauti ya chini

"Umeleta uhai kwenye maisha yangu,

Umenisongeza penye ndoto zangu,

Umeupatia ushujaa moyo wangu,

Edrian wewe ni chaguo langu"

Ed alipomaliza kusoma aliinua macho na kumtazama Aretha ambaye macho yake yalilowana machozi. Akapiga hatua na kumkumbatia huku akifuta machozi yake

"Nakupenda sana Retha" akasema

Akamsogeza mbele "umependeza sana" kisha akamkumbatia tena. Akamuachia na akamshika mkono hadi kwenye meza akamkatisha

"Mbona hujaangalia zawadi yako?" Aretha akamuuliza mara alipomuona akiweka sahani tayari kwa chakula

"Nitaangalia princess, maneno haya ni zawadi nzuri sana. Kukuona na furaha ni kitu kikubwa kwangu. Ngoja tule kisha nitaitazama." Akainama na kumbusu kwenye paji la uso..

Wakala chakula kwa furaha, mara walipomaliza Ed akainuka na kuchukua box ili kuangalia zawadi yake

Pochi ya kiume iliyotengenezwa kwa urembo wa shanga zile zilizokuwa kwenye gauni ya Aretha. Haikuishia hapo kulikuwa na "off shirt" ambayo ilitengenezwa kwa rangi kama zilizokuwa kwenye gauni ya Aretha haikuwa na vifungo.

"Retha mpenzi asante sana" akamwambia kabla ya midomo yao kukutana na kuzama kwenye busu zito.

Tamaa ya miili yao sasa ilimeza uwezo wao wa kufikiri, busu likaendelea na sasa walikuwa chumbani kwa Ed. Japokuwa alisita kufungua zipu ya gauni la Aretha lakini alipomtazama pale kitandani alipomuweka na jinsi alivyomtazama kwa uhitaji wa kuwa mikononi mwake ni kama zimwi liliamshwa mwilini mwake. Akainama na kumbusu taratibu sasa akianzia shingoni kwake na kushuka taratibu kitendo kilichomfanya Aretha kugugumia kwa raha.

Mikono yake ikapita kwa chini na kuvuta taratibu zipu ya gauni huku midomo yake ikimbusu taratibu kwenye shingo yake.

"Aaahh" sauti ya Aretha ilidhihirisha kwa kiasi gani kila mguso wa Ed uliathiri mwili wake na kutamani tamaa yake ikidhiwe

Zipu ilipofika mwisho, akalishusha gauni mwenyewe huku Aretha akifumba macho kwa aibu. Edrian alipofanikiwa kulitoa gauni lote kwa uangalifu macho yake yalimtazama Aretha kiasi cha kumpa picha ya fisi mwenye njaa kali ambaye mate humtoka kwa kuona kipande cha nyama.

Akameza mate kwa nguvu hata koromeo lake likapanda na kushuka. Akavua shati aliyovaa kwa haraka na kuitupia pembeni, akashusha mkono kwenye mkanda akaufungua kwa haraka akauvuta na kushusha suruali akaitupa chini..

Sasa Ed alibaki na bukta, hakuna kilichowazuia kutimiza tamaa zao. Akainama na kuendelea kumbusu lakini japo alisikia raha na kutaka kuendelea lakini kulikuwa na sauti ya upole ikimzuia.

"She is yours why are you in hurry?"

" Stop now before it's too late"

Ghafla akamkumbuka Joselyn na kile alichomfanyia kwenye usiku wa harusi ya Brian.

Akajitupia pembeni ya kitanda huku akihema kwa nguvu na kumshtua Aretha ambaye alifumba macho muda wote kwa raha.

"Rian" akaita