Chapter 228 - MBINAFSI

Jioni walipokuwa njiani wakirejea hotelini Aretha alikuwa akimsimulia Edrian kwa furaha namna ambavyo alifurahia matembezi ambayo walifanya na Britney kwa masaa matano.

"Am sorry princess, sikuweza kujiunga nawe mapema, kuna mabadiliko ya ratiba yalitokea tukatakiwa kubaki kwa muda" Edrian akamuomba msamaha

"Oooh it's okay Rian, lakini asante sana. Britney ni mtu mzuri kweli ukitaka kujua sehemu! Amenipeleka soko kubwa la utamaduni, huwezi amini nimekutana na watu wa kutokea kwetu nimefurahi sana" Aretha akamwambia Ed asiweze kuficha furaha yake

"Eeeeh nilikwambia utanisahau kabisa mimi!" Ed akalalamika

"Hahaaaa hapana, ni kusema tu nilikuwa naangalia vitu vingi vya sanaa pale sokoni, sikuwa hata na muda wa kuangalia simu. Hata hivyo nina zawadi nimekununulia naamini utaipenda"

"Eeeeh kweli! Iko wapi" Ed akanyoosha mkono ili kupokea

"Hahaha nitakupatia tukifika nyumbani. Ninataka kuiboresha kidogo."

"Ahhhm haya. Kitu gani kingine ulifurahia kufanya" Ed akamuuliza

Aretha akamshika mkono Ed na kumvuta amsikilize kwa karibu "Nimechora picha na nimeiuza papo kwa papo"

Edrian akashangaa "uliwezaje Retha?"

"Aaahhhh Britney ndio alikuwa dalali wangu mara nilipomaliza kuchora. Alinipeleka 'House of Art.. Rian ni pazuri sana!!" Aretha akamwambia huku akionesha kuvutiwa sana na mahali hapo

Edrian akazungusha mkono wake begani kwa Aretha akamvuta na kumbusu kwenye paji lake la uso, "Napenda ukiwa kwenye furaha wakati wote." Akamkumbatia " I love you Retha"

"Thank you Rian" Aretha akashukuru na kumkumbatia pia, lakini akakumbuka kiti ghafla na akajitoa kwenye mikono ya Ed

"Muda wote nimekuwa mbinafsi. Siku yako imeendaje?"

"Aaah sio ubinafsi Retha lakini nimefurahi kunisimulia jinsi ulivyojisikia" kisha Ed akamsimulia mambo aliyofanya hadi gari iliposimama kwenye hoteli wakashuka na kuelekea mapokezi ambapo walichukua kadi na kuelekea kwenye lifti

Kabla ya mlango wa lifti kufunga akaingia mwanamme na mwanamke ambao walionekana kuwa wapenzi. Wakawa wakibusiana na kucheka, Aretha ambaye alisimama karibu nao akainama akitazama simu yake. Ed akatabasamu na kisha akainama na kumwambia huku akijua kabisa wale watu hawataelewa

"Na mimi nifanye kama huyu jamaa!"

Macho ya Aretha yakang'aa kwa mshangao huku akiinua kichwa na kumtazama. Ed akatumia nafasi hiyo akamvuta karibu yake wakati huo lifti ikasimama kwenye sakafu waliyoshuka wale wapenzi, wakabaki wao pekee, kimya kikapita kati yao huku Ed akiendelea kumkamata begani Aretha.

Walipoingia kwenye chumba chao,

"Rian"

Aretha akamuita Ed mara alipomuachia na kuelekea kwenye tanuru ya kukolezea moto maana kulikuwa na baridi na hakutaka kutumia mashine ya kuleta joto. Akamwangalia lakini akatikisa kichwa kuonesha hakuwa na la kusema kwa wakati huo.

Akaendelea kukoleza moto kisha akasogea alipoketi Aretha ambaye alikuwa ametoa koti na kubaki na sweta jepesi

"Utakula nini princess?" Ed akamuuliza huku akichukua karatasi lenye orodha ya chakula juu ya meza kabla ya kujiunga pamoja nae kwenye kochi

Baada ya kuwajulisha jikoni chakula ambacho wangetumia usiku, wabaki kwenye kochi huku wakitazama runinga ambayo ilionesha matukio mbalimbali kwenye jiji hili la Sidney.

Ed akaamua kumpigia simu mama yake na Aretha ambapo waliongea nae kwa muda na baadae wakaongea na mama yake Ed. Wakati wakiendelea na mazungumzo huku wakisubiri chakula Aretha akakumbuka kitu akainuka na kuelekea chumbani kwake

"Rian nipe dakika tano nakuja"

Edrian akamtazama huku akitabasamu namna ambavyo aliruka kama mtu aliyeng'atwa na kitu tayari

Dakika tano zikapita, Ed akasubiri lakini Aretha hakuja, akaamua kuinuka lakini kabla ya kufika kwenye mlango wa chumba chake, mlango mkubwa ukagongwa

Akaelekea mlangoni alipofungua mhudumu akiwa na kitoroli kilichobeba chakula. Akakipokea na kumshukuru mhudumu na akakisukuma mpaka karibia na meza ya chakula. Akasimama akitazama mlango wa chumba cha Aretha

"Retha" akaita

"Nakuja Rian, dakika moja tu" sauti ya Aretha ikasikika kutokea ndani!

Ed akatabasamu kisha akaenda kuketi na kutazama simu yake, mlango ukafunguliwa..