Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 227 - NI MGONJWA

Chapter 227 - NI MGONJWA

Weeeh dada Beruya, anaweza kuwa anazingua__"

Mlango ukafunguliwa na Annie akanyamaza asiendelee kuzungumza, akainuka alipomuona Li akiwa na glasi...

"Niletee barafu ziko juu" Li akamwambia baada kumuona ameinuka tayari kuingia ndani.

Akamimina juisi kwenye glasi mbili huku moja iliyojaa akimsogezea Beruya ambaye sasa alimtazama na kumshukuru,

"Hii itakusaidia kupunguza athari za ile dawa " Li akamwambia huku akiketi na mara hiyo Annie akaleta bakuli lililokuwa na vipande vya barafu akaweka mezani na kutoka

Dakika kadhaa zikapita kukiwa na ukimya kati yao huku wakinywa taratibu juisi

"Samahani, uliniokota au kuna mahali mlikuja kunisaidia?" Akauliza Beruya akimshtua Li ambaye mawazo yake yakirejea mambo yaliyotokea usiku wa juzi.

"Mmmh!" Akaguna kisha akamuangalia Beruya na akaona uhitaji mkuu kwenye macho yake kujua nini kilimpata,

"Unataka nikusimulie kilichotokea?" Akamuuliza

Beruya akatikisa kichwa akikubali, akachukua juisi na kunywa.

"Nini kilitokea Beruya?" Li akauliza taratibu akimtazama kwa makini usoni

Beruya akamtazama kisha akaelekeza uso wake kutazama kwenye bustani nzuri ya maua iliyokuwa mbele yake kisha akaanza kumsimulia,

"Damian aliniambia nimsindikize kuna mgonjwa anahitaji kumfanyia matibabu Eastern Zone. Mwanzoni nilikataa sababu hatukuwa kwenye hali nzuri kimahusiano, hata ujio wake kwangu haukuwa rasmi." Akashusha pumzi na kunywa juisi kisha akaendelea

"Akaniambia huyo mgonjwa ni mwanamke na hatoweza kwenda peke yake, nikamwambia awasiliane na nesi, lakini akaniambia kuwa huyo ni mgonjwa wake binafsi. Baada ya kunishawishi na simu yake kuita mara kwa mara, nikaamua kwenda pamoja nae. Wakati tukienda nikaona muelekeo wa gari unaenda nyumbani kwake nikashangaa na kumuuliza, lakini aliniambia kuna dawa akazipitie kwake. Tulipofika nikakataa kuingia ndani, wakati namsubiri akanipigia simu akiniomba niende nikamsaidie kuchukua kasha la sindano. Nikaenda. Nilipoingia ndani hakuwepo sebuleni, akaniita akiwa jikoni, nikaenda nilipofungua mlango alikuwa ameshika kasha linalobeba dawa za sindano, nilipolipokea nikachomwa na kitu kwenye mkono, nikaachia lile kasha maana mikono yangu ilikufa ganzi ghafla nikasikia baridi. Nikarudi nyuma na wakati huo macho yangu yakapata giza japokuwa nilihisi Damian akinidaka, kisha sikujua nini kiliendelea" macho ya Beruya sasa yalikuwa na unyevu unyevu wa machozi, Li akatoa kitambaa chake mfukoni na kumpatia

"Asante" akashukuru kisha akafuta pua na kupangusa machozi kisha akaendelea

"Nilipozinduka nilikuwa nimelala kwenye godoro lililokuwa chini kwenye chumba ambacho alikitumia kama stoo, lakini karibia kila kitu kilikuwa kimeondolewa na kukabaki makabati. Nilipojaribu kuinuka sikuweza kabisa japokuwa kilikuwa katika ufahamu wangu. Baada ya muda kupita akaingia na kuniketisha kisha akanipa chakula. Taratibu nguvu nikaanza kusikia nguvu kwenye mwili wangu. Akaendelea kufanya hivyo kwa siku mbili"

Li akamuuliza "Hakukwambia kwa nini alifanya hivyo?"

Beruya akavuta pumzi na kuishusha kwa nguvu, akapangusa tena mafua mepesi yaliyotokana na kujaribu kuzuia machozi

"Damian ni mgonjwa! Nimeamini sasa mara kadhaa Yassin aliniambia nikae mbali nae!!" Akasema huku akionesha mfadhaiko usoni

"Lakini ni daktari yule!, lazima asingeendelea na kazi Beruya" Li akauliza kwa mshangao

Beruya akaangalia glasi ya juisi kabla ya kunywa funda moja kisha akaendelea

"Nahisi kuna dawa anazitumia ambazo hataki mtu azifahamu maana kuna wakati nilikuta boksi za dawa na nilipomuuliza akasema ni za mteja wake. Nilipomuuliza akasema anapitia changamoto za kiakili, siku moja niliona ndani ya begi lake zile zile dawa zikiwa kwenye chupa ndogo ambayo imeandikwa "supplement"

"Beruya pengine sio zake kama alivyosema. Hebu tuishie hapa tutaendelea wakati mwingine, si vyema kuwa na mfadhaiko wowote kwa sasa. Nitakusimulia baadae, nadhani kapumzike." Li akamwambia kwa sauti ya upole..

Beruya akakubaliana naye sababu alihisi uchungu moyoni, akamalizia juisi

"Asante kwa juisi nzuri"

Li akainama kichwa kupokea shukrani zile, akajibu

"Asante kushukuru"