Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 226 - MRS SIMUNGE

Chapter 226 - MRS SIMUNGE

"She is here with me." Ed akajibu huku akielekeza macho mahali Aretha alisimama

"Naweza kuongea nae?" Swali la Li likamfanya Ed ashtuke

"Kuna tatizo kwa Beruya?" Akauliza Ed

"Hapana bro, nafikiri aongee nae sbb yuko macho tayari" Li akamwambia huku akitabasamu kwa namna kaka yake alishtushwa

"Aah, good then!" Ed akageuka na kumuita Aretha ambaye alisogea japokuwa uso wake ulikuwa na maswali!

"Beruya ameamka" akamnong'oneza kisha akampatia simu

Aretha akategemea angemuona Beruya lakini sura ya Li ikiwa katika kioo cha simu

"Habari ya safari Aretha?" Akamsalimia

"Salama, Habari za huko?" Akauliza

"Huku, hatujambo, nimefanya kazi kama tulivyokubaliana. Naamini nawe hutaniangusha"

"Aaahmm... Asante sana" Aretha akashukuru,

Li sasa alifungua mlango na kutokea barazani ambapo Beruya aliketi na Annie

Akamkabidhi simu Beruya pasipo kuongea chochote. Aretha alifurahi mara alipomuona Beruya

Ed akasogea alipo Aretha mara aliposikia Beruya akiongea...

Wakamuuliza kuhusu maendeleo yake ya kiafya huku Aretha akimshauri amsikilize Li kwa kukubali kubaki hapo nyumbani kwa mama Simunge..

"Nakuomba usiondoke. Najua una onesho wiki mbili zijazo tafadhali hebu tumia muda huo kuchora tena picha zako" Aretha akamshauri wakati huo Ed akamtazama na kutabasamu

"Beruya, ukiwa hapo kwa mam utakuwa salama hadi tujue nini mwisho wa Damian" Ed akaongeza

Walipomaliza kuongea na Beruya, Li akachukua simu na kurudi ndani huku akiendelea na mazungumzo na Ed.

"Damian mmemalizana?" Akauliza Ed

"Captain amempeleka kwa mjomba wake!" Li akajibu

"Eeeh alijuaje?" Edrian akauliza kwa mshangao

"Unamjua Captain! Alimchukua akiwa hajitambui sababu dawa aliyojichoma imempa kiharusi kwa muda. Akampeleka asubuhi. Mjomba wake ameshukuru sana hakufunguliwa kesi baada ya kusimuliwa mkasa wote." Li akamuelezea.

"Hahahhaa namuelewa, hapendi ushahidi"

Walipomaliza kuongea, Edrian akamgeukia Aretha ambaye aliketi kwenye kochi akiangalia jarida la "The Sidney". Aliposikia Ed akikata simu akashusha jarida kisha akamwambia

"Asante Rian."

"Najisikia vyema kukuona mwenye furaha" Edrian akajibu huku akisogea alipo Aretha

"Tunaenda wote?" Akauliza Aretha

Edrian akatabasamu kisha akanyoosha mkono kumuelekea, Aretha akaweka jarida pembeni na akaupokea mkono wake naye akamuinua kisha akamvuta amsogelee. Akainama hata nyuso zao zikagusana

"Uko tayari nikutambulishe kuwa u mke wangu eeh?

"Ahmm" Aretha akashtuka na kujaribu kuinua uso wake lakini Edrian akambana kwenye paji la uso

"Mmmh uko tayari" akaongea kwa kunong'ona

"Ri. ..Rian..naa__" kabla ya kuendelea na kigugumizi kile Ed akamkumbatia Aretha na kumwambia taratibu sikioni kwake

"Nimekuandalia mahali pa kwenda muda huo. Utapapenda Mrs Simunge"

Akamwachia Aretha akibaki kwenye mshangao akapiga hatua hadi kwenye meza akamwambia

"Hakuna cha kuvutia kwenye ratiba ya leo Retha lakini kuna mahali nimetamani uende. Kwa masaa matano utatamani kuendelea kubaki ahaha!!. Britney, rafiki yangu na moja ya wakala wa SGC atakuwa mwenyeji wako kwa leo, nitajiunga nanyi baadae"

Edrian alipomaliza kusema hayo akamtazama Aretha

"Oooh nitaenda na huyo Britney?" Kulikuwa na wasi wasi kwenye sauti ya Aretha

"Retha, ni binti mchangamfu utamzoea hadi nahisi utanisahau kabisa mimi, usiwe na hofu, nitajiunga nanyi nikimaliza ratiba ya leo. Ipo siku nataka tuongozane wote!"

"Oooh basi sawa" Aretha akajibu kwa furaha

Simu ya mezani ikaita na mara alipopokea akajulishwa kuwa usafiri wake uko tayari.

"Twaweza kuondoka sasa. Umechukua mkoba?" Akauliza

"Uko hapo sebuleni" akajibu huku akiinuka

Wakatoka na kuelekea kwenye lifti, Aretha akapitisha mkono kwapani kwa Ed na kumfanya asimame na kumtazama usoni kisha akatabasamu

"That is so sweet Retha" akanong'ona

"Aaahm" Aretha akamezea.

*****

Li akatoa ile juisi kwenye jokofu, akabeba glasi mbili na kuelekea barazani, akamkuta Annie akiendelea na soga zake naye Beruya alionekana kufurahia kwa kucheka. Akasimama akiwatazama kupitia kwenye dirisha lililokuwa kwenye mlango wa kutokea.

"Hahaha Annie usichanganye mapenzi na kazi"