Edrian alishtuka masaa matatu baadae akajinyoosha kitandani huku akitamani aendelee kupumzika alihisi uchovu lakini alihitajika kwenye siku ya kwanza ya ufunguzi wa kongamano.
Akashuka kitandani na kuelekea bafuni, akaoga na kisha akajiweka sawa kwa kuvalia suti ya rangi ya kijivu shati nyeusi ndani. Akachukua kitambaa kizito (scarf) akakizungusha vyema shingoni ili kujikinga na baridi. Alipojihakikisha kuwa muonekano ule ulimfaa vyema huku kila hatua aliyopiga ikinena "mimi ni Edrian Simunge", jasiri kama simba.
Akafungua mlango ili aelekee chumbani kwa Aretha apate kumuamsha kwa ajili ya kujiandaa, lakini akashangazwa na kumuona Aretha akiwa amesimama kwenye mlango wake.
"Retha uko macho tayari ulikosa usingizi!!!"
"Mmh ... nadhani nililala sana kwenye ndege, umeamkaje?" Aretha akamsalimia huku macho yake yakivutiwa na muonekano wake
Edrian akafungua mlango na kumruhusu aingie chumbani kwake. Aretha akaingia huku macho yake yakitazama mwonekano wa chumba kile ambao aligundua kilikaribia kufanana na chake isipokuwa pembeni kulikuwa na meza ya kiofisi na kiti na pembeni kulikuwa na kochi la watu wawili. Kitanda kilikuwa upande mwingine wa chumba na kilikuwa cha ukubwa wa wastani tofauti na kile cha chumbani kwake Aretha.
Edrian alimtazama Aretha, moyoni akakubali kuwa alipendeza sana asubuhi hii. Alivaa suruali na juu koti lenye manyoya ya sufi ilionekana kwa juu huku china akivaa viatu vilivyofunika karibia na kwenye goti. Nywele zake zilifungwa pamoja na kusababisha uso wake kuonekana vyema.
Aretha akasimama akimtazama Ed ambaye alielekea moja kwa moja kwenye meza akachukua begi la kiofisi akaangalia vitu vyake
"Rian, tunaenda wote?" Akauliza Arerha
Edrian akaacha kuangalia kwenye begi, akageuka na kumtazama Aretha huku macho yake yakimkagua kama aliuliza akimaanisha anatamani kwenda naye au la! Akaona furaha kwenye lile swali!
"Unataka twende wote?" Akauliza
Aretha akatikisa kichwa kukubali na tabasamu likaonekana..
"Sawa nipe dakika chache nimtaarifu mratibu saba__"
Simu ya Ed ikaita naye akaangalia alikuwa Linus alimpigia kabla ya kupokea akamgeukia Aretha
"Umeshaongea na mama?" Akauliza
"Hapana, nitampigia kabla hatujaondoka"
Akapokea simu ya Li
************
Usiku wote uliisha, hata mawio ya jua yakaangaza nje, Li aliketi chumbani kwake akimtazama Beruya mpaka alipohakikisha joto la mwili wake limeshuka na hali yake kuimarika. Pamoja na hayo bado Beruya hakuwa ameamka.
Li akainuka na kujinyoosha, sauti ya mtu aliyegonga mlangoni ikamshtua lakini kabla hajaitikia mlango ulifunguliwa na mama yake akaingia
"Li hukulala eeeh?" Mama akamuuliza mara tu alipomatazama usoni
Akatikisa kichwa kumuonesha kuwa hakulala,
"Eishhh umekesha pasipo kuniamsha! Ungemwamsha hata Annie, duh!"
"Mama ni__"
"Shhhshh, hebu kaoge, kanywe supu na ulale na ulijaribu kunibishia" mama akamwambia huku akisogea alipolala Beruya
"Sawa mama, lakini natakiwa kwenda kaz__"
"Aiii una msaidizi, mpigie asimamie hadi utakapoamka" mama akatoa maelekezo huku akiketi kwenye kiti pembeni ya kitanda. Beruya alionesha kila matumaini ya kuamka kuanzia utulivu katika kupumua tofauti na ule usiku ambao Li alilazimika kukaa pembeni yake akimsaidia. Hakuwa tena na dripu na alionesha kusafishwa vyema na nywele zake zilifungwa pamoja tofauti na alivyokuja..
"Bado umesimama! Hauamini niko kumsaidia?" Mama akamuuliza kwa utani Li
"Hahaha hapana mama" Li akajibu kisha akageuka na kuelekea mlangoni
"Mwambie Annie aje huku mara moja"
Li akatoka akimuacha mama ambaye alimtazama Beruya kwa huruma
"Sijui kwa nini unapitia maumivu haya wakati bado wewe ni binti mdogo sana" mama akawaza kwa sauti kisha akaangalia kitambaa na beseni dogo vilivyokuwa tupu mezani..
"Huyu mvulana wangu amejitoa hivi kwako aaaah una bahati sana dada. Natamani ukiamka utambue mchango wake katika kuokoa maisha yako" mama akatabasamu kabla ya kusikia mlango ukingongwa.
"Ingia"
Annie akaingia ndani akiwa ameshika beseni dogo na kitambaa safi
Li kakuambia uje na hivyo? Akauliza mama
"Ndio"
Akaweka kwenye meza akasimama na kumsikiliza mama