Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 223 - SAFARI NDEFU

Chapter 223 - SAFARI NDEFU

"Are you sure?" Akamuuliza

Tabasamu la uchokozi likatokeza usoni kwa Ed akapiga hatua kumsogelea Aretha ambaye macho yake aliyaelekeza kwingine akikwepa kumtazama

Ed alipomkaribia akainama hadi usoni kwake akamshika kidevu chake akakiinu kumuelekea..

Akatabasamu alipogundua mkwamo wa pumzi uliokuwa kwa Aretha,

"Retha" akamuita kwa sauti ya chini

"Ahmmm" akaitika Aretha huku macho akiyakwepesha asimtazame Ed

"Niangalie"

Aretha akayarudisha macho yake usoni kisha akalamba mdomo wake akimfanya Ed amtazame zaidi kwenye midomo yake.

"Ni kweli huniogopi mmmh?" Akauliza kwa sauti ya chini lakini ilifanya mwili wa Aretha usisimke.

Akatikisa kichwa akikataa kuwa hamuogopi Ed, kitendo kilichomfanya Ed ashushe midomo yake ikakutana na ya Aretha, mkono ule alimshika kidevu akaushusha hadi kiunoni kumpa wepesi wa kubaki ameketi na asianguke kwenye kitanda.

Busu lilikuwa la dhati naye Ed hakumpa nafasi apumue, Aretha akakamata mikono ya Ed akifurahia muunganiko wao.

"Ahmm" sauti ya mguno kutoka kwa Aretha ni kama uliwasha moto, Ed akamuinua huku akitenganisha midomo yao.. akamsimamisha alionekana kuwa kama mtu asiyetaka kupoteza hata sekunde moja..

Akamwangalia Aretha akiwa mwenye kuonesha uhitaji wa kupata busu jingine...

"Huniogopi?" Ed akauliza taratibu huku macho yake yakitazama yale ya Aretha

Akatikisa kichwa kisha kwa mara ya kwanza Ed akaona tabasamu la kichokozi kwa Aretha na kilichofuata alivutwa kwa busu jingine ambalo hakika akakubali kuwa Aretha sasa hamuogopi!

Uzito wa busu hili ukafanya mwili wa Ed sasa uwake kutaka kutimiza tamaa yake. Akamnyanyua pasipo kukatisha muunganiko wa ndimi zao, mikono ya Aretha ikiwa shingoni kwa Ed. Akamlaza kitandani kama mtu aliyebeba kitu chenye kuvunjika huku mkono wake ukiegemea kwenye kiwiko.

Walipopeana nafasi ya kupumua, macho yao yakatazamana tamaa yao ikawa wazi, Edrian akameza funda kubwa la mate mara Aretha alipomshika kifuani na kuanza kufungua vifungo vya shati... akilini kulikuwa na sauti ya mjomba ikimkumbusha ahadi ya yake. Akajaribu kushindana nayo japokuwa ilizidi kufifia ndani yake kila mara Aretha alipomgusa. .

"Rian" sauti dhaifu ikamshtua Ed kwenye mawazo yaliyomjia ghafla, akatazama mikono ya Aretha ambayo ilitoka kufungua hadi kifungo cha mwisho

"Ahmm" akaitika akiwa ameathiriwa na mazingira yale na kufanya mikwaruzo isikike kwenye sauti yake..

"Naa. ...naomba...ninywe maji" akainama tena

Edrian akatoka juu yake na kushuka taratibu, akafungua mlango na kutoka huku akirejea na chupa ya maji. Akampa Aretha ambaye macho yake yalimtazama kifuani ambako hakuwa na shati. Akanywa maji kisha akaweka chupa kwenye meza pembeni mwa kitanda. Wakaangaliana huku macho yao yakizungumza tofauti na kile akili zao zilinena. Ed akasogea na kupiga goti moja juu ya kitanda kisha akamshika kidevu na kuinua uso wake

"Sawa Retha nimekubali huniogopi, nenda kaoge upumzike nitakuamsha baada ya masaa manne" alipomaliza akambusu, akavuta shati yake na kuelekea mlangoni..

"Rian" sauti ikamfanya Ed asimame akageuka na kumtazama

"I love you" akamwambia kwa tabasamu huku akilamba midomo yake

Edrian akasimama huku akimtazama, miguu ilitamani kurudi alipo Aretha lakini akili ikagoma.

"I love you Retha" akameza mate kisha akafungua mlango na kutoka nje akielekea chumba cha pili.

Mara alipoingia ndani ya chumba chake, akaelekea bafuni, akaruhusu maji ya uvuguvugu yammwagikie kwa muda, japokuwa hayakuwa na msaada wa haraka katika kushusha joto la tamaa kwenye mwili wake. Baada ya nusu saa akatoka na kujiweka vyema, akavalia pajama zake na kisha akajitupia kitandani

"Ngoja nimuache apumzike" Ed akazuia mkono wake kwenda kwenye simu iliyokuwa mezani ili ampigie.

Akalala huku akikumbuka kile kilichojiri muda mchache nyuma, akacheka kicheko chepesi

"Wiki mbili, itakuwa safari ndefu tofauti na nilivyodhani"

Akapitiwa na usingizi, hawakuhitaji chakula kwa usiku ule kwa kuwa walikula masaa manne kabla ya kuwasili Sidney.

Aretha hakuweza kulala alipomaliza kuoga aliketi kitandani akisikiliza masomo ambayo yalisomwa na wenzake darasani, akitabasamu kila mara alipomkumbuka Ed