Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 220 - NI SHWARI

Chapter 220 - NI SHWARI

Li hakuweza kulala usiku kucha toka muda ule aliomfikisha Beruya nyumbani kwa mama yake. Chumba alicholala kilikuwa ni chumba kilichotumiwa na Li wakati wote walipoishi kwenye nyumba hii. Alimtazama Beruya ambaye alilala pasipo kuwa na ufahamu wowote juu ya mambo yaliendelea barabarani.

"Mhhhhh" akashusha pumzi mara aliporejea na beseni lenye maji na kitambaa safi laini akamfuta jasho ambalo lilianza kuonekana usoni kwa Beruya..

Huku akiwa na wasi wasi akachukua simu na kumpigia Dokta Brianna akamueleza hali ilivyo, kwa sasa lakini Dokta akamuondoa shaka

"Li hiyo dawa niliyoichoma ndani ya dripu inapambana na ile ambayo alichomwa mwanzo hilo joto litakaa vyema. Fanya kama nilivyokuagiza, tumia maji na kitambaa kumfuta taratibu mwili wake utarejea"

Li akamshukuru kisha akakata simu, "hili zoezi sikujua kama lingekuwa gumu, namuombea apone haraka la sivyo itakuwa shida" akawaza kwa sauti.

Mara alipofika nyumbani na kumtaarifu mama yake juu ya ujio wa Beruya na hali aliyokuwa nayo, mama yake alimshauri amtafute daktari waweze kuangalia hali yake. Walifanya hivi baada ya kujaribu kumuamsha Beruya lakini hawakufanikiwa, hawakujua msaada wa kumpa.

Dokta Brianna alipofika alifanya uchunguzi wa haraka na akagundua kuwa Beruya alichomwa dawa ambayo inafanya awe katika hali ya kupoteza fahamu kwa masaa mengi. Ili kumrudisha alihitaji kumwekea dawa nyingine ambayo itapunguza taratibu utendaji kazi wa ile ya kwanza. Akamwekea dripu la maji na kisha akachoma dawa mpya ndani yake. Dripu ile ilitona taratibu kuingia mwilini kwa Beruya..

Li aliendelea kumfuta taratibu, alitamani angekuwepo Coletha angempa ile kazi lakini hakuwa nyumbani ambako aliishi nao. Hapa palikuwa kwa mama yake na muda ambao alitumia kumsaidia mara alipofika hakutaka kumsumbua tena, japokuwa mama alimwambia amuashe ikiwa angehitaji msaada zaidi.

Wakati akimfuta taratibu kwa kile kitambaa laini aliona akikunja nyusi kama mtu aliyekuwa kwenye ndoto ya kutisha na kila mara alipofanya hivyo alitoka kijasho kwenye paji lake la uso!

"Nini kinaendelea Beruya" akamuuliza huku akiwa na hakika hatoweza kupewa majibu yoyote. Akamwangalia namna alivyolala akasikia funda zito limemkaba kooni. Huruma ikamshika huku akitafakari mambo mazito ambayo ameyapitia mara alipochomwa sindano ile. Hasira zikamshika alipomfikiria Damian

"Unakuwaje daktari na ukatili wa namna you?"

Ghafla mikono ya Beruya ikarushwa hewani kama mtu aliyekuwa akijitetea asiumizwe, beseni ambalo Li alilishika likaanguka pembeni. Li akamuwahi na kumshika mkono ule ambao sindano ya dripu iliwekwa. Akamshika vyema huku akiinuka na kuketi kitandani akamshika mikono yote miwili.

Machozi yakatiririka pembeni ya macho ya Beruya, Li akatamani angesikia nini kinachomfanya atoe machozi yale walau amfariji lakini asingeweza kwani Beruya alikuwa katika usingizi ambao bado ulikuwa na jinamizi likimuwinda!

Akanyoosha mkono kuchukua kitambaa laini kwenye boksi lililokuwa pembeni ya kitanda. Akamfuta machozi yale "Ni shwari Beruya usiendelee kulia." Kama vile Beruya alisikia maneno ya Li, machozi yakaacha kutiririka.

"Thank you" Li akajikuta akisema maneno yale, sauti ya mtetemo wa simu yake ikiita ikamshtua akaivuta kutoka kwenye meza iliyokuwa pembeni

Alipoangalia kioo cha simu yake, Edrian kaka yake akipiga simu ile, akapokea ambayo ilipigwa kwa mfumo wa video

"Brother" akaitika Li

"Uko na Beruya?" Ed akauliza mara alipomuona kwenye kile chumba ambacho alikifahamu

"Ndio bro, yuko hapa japokuwa hali yake sio njema ila Dokta Brianna amesema ndani ya siku mbili itarejea vyema" Li akajibu huku akiiweka vyema kamera

Kimya cha sekunde kilipita kisha Ed akaendelea "ilikuwaje, nambie?"

Li akamsimulia kwa ufupi jinsi ilivyokuwa na namna ambavyo akimuacha Captain kumalizia yaliyosalia huku yeye akiwahi kumsaidia Beruya..

"Asante sana brother!" Akashukuru Ed kisha akaongeza, "Mwache akae hapo mpaka nitakaporejea na kama atasisitiza kuondoka usimzuie, isijekuwa tunalazimisha mtu pasipo kujali maamuzi yake"

"Sawa brother. Mmefika Kuala Lumpur?" Akauliza Li huku akitazama kwenye kioo cha simu yake