Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 219 - UVUNE ULICHOTAKA

Chapter 219 - UVUNE ULICHOTAKA

"Hahaha wewe hujui unachotaka" Captain akacheka kwa dhihaka

"Ungejua unachotaka ungemuacha huyo mwanamke asiharibu maisha yako, ona ulivyokuwa usi__"

"Shut up!!" Akahamaki Damian na kupiga hatua kusogea alipokuwa Captain

"Unaambiwa ukweli Dr, utapoteza vitu ambavyo umevihangaikia takribani miaka 10 ya maisha yako" Li akaongeza

"Unayo mengi ya kupoteza Damian, kubali umuache huyo mwanamke na sisi hatutamwambia yeyote kuhusu wewe na__"

Damian sasa alikuwa anatetemeka kwa hasira, lakini ghafla kulikuwa na gari nyingine ikipita upande wa pili wa barabara, ikasimama na dereva akatoa kichwa kuuliza kama kulikuwa na tatizo..

Captain akachukua fursa ile kumkimbilia Damian huku Li akielekea kwa kwenye gari kumtoa Beruya. Yule mwenye gari alipoona hivyo akaondoa gari kwa haraka.

Damian akajaribu kurudi alipokuwa Beruya lakini Captain akamkamata na kumvuta kwa nyuma. Damian akajaribu kumchoma ile sindano Captain lakini mkono wake ulishikwa vyema.

"Niache...usimchukue Ber" akalalama Damian lakini Captain alimzidi nguvu.

"Sasa ngoja uvune ulichotaka" Captain akamwambia kisha akaubana mkono na kugeuza lile bomba la sindano kumuelekea Damian..

Damian macho yakamtoka akiangalia ile sindano iliyomwelekea, hakuamini mpaka aliposikia ikiangia kwenye sehemu ya paja lake na ghafla ulimwengu wake ukaanza kuingiliwa na giza kisha viungo vyake vikakosa nguvu.

Captain akamuachia Damian ambaye alianguka chini. Li alisimama pembeni huku Beruya akiwa mabegani mwake.

Captain akafungua mlango naye Li akamuweka Beruya kiti cha nyuma. Captain akafungua mlango na akatoa begi lake kisha akamwambia Li, "tangulia, ngoja nishugulikie hili na huyu bwana asaidiwe"

"Sawa, thanks comrade" Li akashukuru na kingia kwenye gari kisha akaondoka, akiamini Captain atahakikisha hakuna sehemu watahusishwa.

****************

"Rian" Aretha akaita kwa sauti ya kunong'ona huku mkono wake ukimgusa begani Ed

"Mmhh" Edrian akaitika kwa sauti ya mikwaruzo huku macho yake yakiwa yamefumbwa kwa usingizi uliomnyemelea..

Masaa matatu yalipita wakiangalia filamu pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali hata wakaanza kuzungumza uwezekano wa kufunga ndoa watakaporejea. Ed alifurahi mara alipomuona Aretha akiunga mkono wazo lake huku shauku yake ikiwa kubwa usoni.

Muda huu Aretha alikuwa akitumia kompyuta mpakato kufanya kazi za chuo ambazo alitumiwa na Charles! Ed alikuwa amechoka na mwenye usingizi akaamua kupumzika akimwacha Aretha akiendelea na kazi zake za chuo. Mara akamsikia akimuita kwa kunong'ona, alipoitika akajaribu kufumbua macho lakini alikuwa amechoka

Akasikia Aretha akiinama karibu na uso wake kisha akambusu taratibu mdomoni mwake

"I love you Rian. Tafadhali pumzika mpenzi nitakwambia ukiamka"

Edrian akajaribu kufumbua macho lakini macho yake hayakufumbuka lakini akajaribu kusema "I love you so.... " hakuweza kumalizia

Aretha akatabasamu na kumbusu tena kwenye paji la uso, akavuta blanketi na kumfunika vyema. Akarudi kwenye kompyuta yake kuendelea na kazi aliyokuwa akiifanya.

Haikuchukua muda naye akamaliza na mara mhudumu akapita na kuuliza kama walihitaji kitu kingine, lakini Aretha akamjulisha kuwa hana chochote alichohitaji.

Akajilaza kwenye kochi huku akiwasha taa ili kusoma kitabu cha simulizi cha "True Lies" mpaka alipopitiwa na usingizi.

Sauti ya mhudumu wa ndege ikiwataarifu muda mchache watashuka katika uwanja wa kimataifa wa Kuala Lumpur..

Ed akafumbua macho, akamuona Aretha akiwa usingizini akatamani asimwamshe lakini walitakiwa kubadilisha ndege ili kuelekea Sydney. Akavuta dirisha mwanga wa rangi ya dhahabu ukamulika ndani, jua lilikuwa katika machweo yake, akainuka na kumshtua Aretha taratibu

"Aaaaahh" Aretha akapiga miayo na kuangalia mwanga ulipotokea akashtuka alipomuona Ed, akajifunika uso na kumfanya Ed acheke

"Unaona aibu ya nini Retha"

Akajifunua "yaani nimesahau kama tuko kwenye ndege"

"Tunashuka sasa hivi jiandae__"

Sauti ya mhudumu wa ndege ilisikika ikiwataarifu kukaa tayari ndege sasa ilikuwa ikijiandaa kushuka.

"Retha hapa ni Kuala Lumpur, tutapumzika hapa kwa saa moja kabla ya kuingia kwenye ndege kwa masaa manane tena"