Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 218 - HII NI MPYA

Chapter 218 - HII NI MPYA

Joselyn alikuwa kama mwenye wazimu mara baba yake Martinez alipomuonesha picha kwenye simu iliyomuonesha Edrian na Aretha wakiwa uwanja wa ndege, wakiwa wameketi kwenye eneo la kusubiri kuingia ndegeni.

"Baba huyu mwanamke ni mchawi na tena akirudi ataniel____" akakatishwa na baba yake

"Eeishshhh utamfanya nini? Hayo uliyofanya yamezalisha nini zaidi ya kuvuruga mipango yangu" sauti ya Martinez ilikuwa ya ukali huku akimwangalia Joselyn kabla ya kuchukua glasi ya mvinyo na kunywa

"Baba naweza kuwa nimeshindwa mara moja au ya pili lakini mara hii akirudi atajua mimi ni mtoto wa Kussa" Joselyn akakunja ngumi kwa hasira

"Hahahaha wewe ni binti yangu!!" Akauliza kwa dhihaka, kisha akaendelea "unachotakiwa kufanya ni kusikiliza au hicho nacho ni kigumu kufanya Joselyn Kussah" akamuuliza na kuinuka huku akiweka glasi iliyoisha mvinyo kwenye meza

Joselyn akanyamaza kimya huku akimtazama baba yake

"Simunge si mjinga Joselyn, ukitaka umpate tumia akili ambayo ni muda sasa tangu umeiacha ilale!"

"Mmmmmhh, sawa baba. Lakini niruhusu sasa nitoke walau ni__"

"Utatoka wakati ambao mimi nitakwambia. Kwa sasa fikiri kwa kina kama binti yangu na si kama mwanamke mtumwa wa mapenzi" Martinez akapiga hatua na kuondoka akimuacha Joselyn ambaye alijitupia kwenye kochi

"Aaaargh" akalalama

"Utalipa maumivu haya Aretha, I swear you'll pay"

********************

Li alikuwa barabarani akiwa na Captain, wakifuatilia gari ambayo iliendeshwa na Damian baada ya kufanikiwa kuwatoroka walipofika eneo ambapo Beruya alimpigia Aretha simu. Wakakumbuka walipishana na gari wakati wakiingia eneo hilo ambalo ilikuwa nje kidogo ya mji huu wa A. Wakafanikiwa kupata namba ya gari baada ya Captain kutumia utaalamu wake hata kuingia kwenye CCTV.

Li akiwa kwenye usukani, alikuwa katika mwendo mkali kuhakikisha wanasogelea gari alilokuwa akiendesha Damian. Walitumia dakika ishirini kuweza kulifikia gari hiyo ndogo.

Akajaribu kugusa kidogo ile gari ndogo kwa nyuma kumshtua Damian asimame lakini hakufanya hivyo. Usiku huo barabarani kulikuwa na gari chache na hivyo Li alijaribu kuwa mwangalifu ili kuhakikisha usalama wa Beruya. Akaongeza mwendo kujaribu kuipita gari lakini Damian akamzuia

"Comrade tumalize mchezo naona anataka kutusumbua" Captain akamwambia Li akatoa kifaa kama bastola kisha akashusha kioo akakielekeza kwenye tairi za gari ya Damian. Akabonyeza kikatoka kitu mfano wa wavu mdogo sana ukaenda hadi kwenye tairi la nyuma upande wa kushoto...

Li akamuangalia mara moja Captain kisha akatabasamu, "hii ni mpya eeeh"

"Hahaha ya muda kidogo" Captain akajibu na ghafla kukasikika mkwaruzo ya tairi kwenye gari ya Damian, ikayumba kulia na kushoto, akajaribu kuendelea lakini tairi la nyuma halikuzunguka. Wakati akihangaika kuendelea kuendesha, gari ya Li ikaingia kwa mbele yake na kisha likasimama mbele yao ghafla Damian akalazimika kushika breki gari ikateleza na kujigonga kwenye ukingo wa barabara kisha kusimama.

Li na Captain tayari walikuwa nje ya gari na wakasogea kwa uangalifu kwenye ile gari ya Damian. Lakini kabla hawajafungua mlango Damian akatoka, kwa msaada wa taa za barabarani, damu zilimchuruzika kwenye sehemu ya juu ya jicho. Walipomtazama kama alikuwa na silaha wakaona mkononi ameshika bomba la sindano. Akafungua mlango wa nyuma akavuta mkono wa Beruya na kuelekeza sindano karibu na ngozi yake..

"Mkinisogelea nachoma hii sindano" Damian aliongea kwa sauti ambayo ilidhihirisha hasira

Li na Captain wakasimama wasipige hatua yoyote lakini Captain akatabasamu kisha akamwambia "Damian unajua una vingi vya kupoteza ukiamua kufanya hivyo eeeh"

"Najua sana lakini Beruya ni mali yangu na hakuna mwingine wa kumchukua. Mkijaribu kumsogelea mtampoteza!"

"Hahaha, Damian nakupa uchaguzi, mwache Beruya tukuache uendelee na safari yako au ukamatwe na polisi ufunguliwe mashtaka ya utekaji, unaelewa" Captain akamwambia

Damian akageuka huku akiuachia mkono wa Beruya ambaye alionekana kutokuwa fahamu zake.

"Usinitishe wewe, utafanya kile mimi ninataka" Damian akakasirika zaidi

"Hahaha wewe hujui unachotaka"