Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 217 - KAKUZIDI AKILI

Chapter 217 - KAKUZIDI AKILI

"Sydney!!!!" Macho ya Aretha yalimtoka kwa mshangao, hakuamini kile alichokiona

"Nione 'passport' yako" akanyoosha mkono kumuelekea Ed huku akimwangalia kama kulikuwa na dalili za kumtania

Ed akatabasamu na kumkabidhi hati yake huku akitabasamu kwa furaha kuona mshangao wa Aretha, "Are you that much suprised aaah!"

Akamuuliza pasipo kujali macho ya baadhi ya watu waliokuwa karibu nao,

"Rian oooh my God, siamini hadi nipaone" shauku na furaha ilijaa usoni kwa Aretha

Edrian alifurahi kuona uchaguzi wa kuongozana na Aretha kuelekea Sydney ulikuwa sahihi.

Sydney ni mji mkubwa na wenye kuvutia katika nchi ambayo ni bara, Australia. Mji wenye vivutio na maeneo mazuri ya mapumziko.

"Jiandae bado nina 'suprise' nimekuandalia tufikapo" Ed akamwambia huku akiweka mkono juu ya mkono wake. Aretha alimtazama aliposema maneno yale

"Aaahm...Asante" akashukuru.

Waliketi kwa saa moja pale wakisubiri kupita katika ukaguzi kabla ya kuingia kwenye ndege. Mambo mengi yalikuwa mageni kwa Aretha na ilikuwa kazi ya Ed kumuelekeza kwa furaha na upendo mwingi. Mara zote Aretha alijiona yuko huru kumuuliza Edrian hata muda ulipofika wa kuingia kwenye ndege.

Mhudumu wa ndege alipoangalia tiketi zao akawapokea na wakaelekea sehemu ambapo waliketi abiria wa daraja la kwanza (first class).

Edrian akashtushwa na mkono ambao ulimshika, alikuwa Aretha ambaye alihisi kushindwa kuzuia mshangao na furaha ya kuona mandhari ile ya kuvutia iliyokuwa machoni pake. Alimshikilia Ed kama alitegemea mkono kama kitu pekee cha kumfanya asimame vyema..

"Rian" akaita kwa sauti laini na ya kunong'ona

Ed akamuangalia, mhudumu akasimama mara tu alipofika mahali ambapo viti vyao vilikuwepo, akawafungulia 'cabin' kisha akachukua mzigo mdogo aliokuwa amebeba Ed na kuuweka. Alipomaliza akawageukia

"Karibu sana Bwana na bibi Simunge, tafadhali kwa huduma yoyote kuna kitufe cha kijani hapo pembeni ya kiti waweza tumia kumuita mhudumu" akawakaribisha na kisha akawaacha.

Edrian akampisha Aretha akaketi kwenye kiti chake, naye akaketi.

"Rian, hii ndio 'first class!" Aretha akanong'ona huku akiangalia kwenye meza ambayo ilitengenezwa ikiunganishwa na sehemu ya kiti ambapo kulikuwa na 'smart screen' na pembeni kukiwa na 'ear pods'. Bado kulikuwa na sehemu ya kuwekea chakula na vinywaji. Blanketi safi na mito viliwekwa pembeni.

"Retha, unastahili kupata vitu vizuri ikiwa vimo katika uwezo wangu. I love you princess" Ed akamwambia huku akimsogelea na kuinama kisha akambusu kwenye paji la uso.

Baada ya kurudi na kuketi, "Tuna masaa sita ya kuwa angani kabla ya kubadilisha ndege kwa masaa nane tena. Nataka ufurahie kila dakika. Ukichoka niambie" Ed akamwambia

"Masaa yote hayo angani Rian!" Aretha akahamaki

"Aaaahm usiwe na shaka sababu nimejiandaa kuyafanya haya masaa yawe na kumbukumbu nzuri kiasi usitake yaishe" Edrian alimwambia huku tabasamu lake likithibitisha uhakika wa kile alikisema

Aretha akashusha pumzi na kukubali kwa kichwa, Edrian akaanza kumuelekeza namna ya kutumia ile skrini iliyokuwa mbele yake.

**************

"Baba siwezi kuendelea kukaa ndani, si umesema tarehe ya kesi inapangwa wiki ijayo" Lyn alimlalamikia baba yake ambaye aliingia nyumbani usiku

Martinez hakuongea chochote zaidi yakuendelea kunywa mvinyo akiwa ameegama kwenye kochi macho yake yakitazama kioo cha simu yake!

"Baba kwa nini hunisikilizi? " sauti ya Lyn ilikuwa ya kubembeleza sasa huku akipiga magoti na kuegemea kwenye miguu ya baba yake, akaendelea

"Nakuahidi baba, mara hii sitafanya ujinga wo___"

"Shshshhhhh" Martinez akaweka kidole kwenye mdomo wake na kumpa ishara Joselyn anyamaze

"Hakuna nafasi ya mara mbili, huyu kakuzidi akili" akageuza simu yake kumuelekea Joselyn akimuonesha picha

Macho ya Lyn yaonesha hamaki, "hii ya lini baba?" Akauliza huku akisimama

"Nisikilize binti yangu, umeshindwa kufanya kazi yako vyema..sasa tulia tutumie njia nyingine" Martinez akamwambia

"Baba hiyo picha ni ya lini, najua hapo ni 'Airport'....Tafadhali niambie baba yangu" akiwa amesimama hivyo

Martinez akainuka sasa, akasimama kumuelekea Joselyn,"nimesema acha kabisa"