Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 216 - NINAKUAHIDI

Chapter 216 - NINAKUAHIDI

Aretha akashtuka na kusimama ghafla, kabla ya kujibu simu ikakatika

"Hellow hellow Beruya!!" Aretha akajaribu kuita lakini simu ilikuwa imekatika.

Ed na Li wakamtazama kisha wakauliza kwa wakati mmoja

"Kuna nini?"

Wasi wasi ulikuwa usoni kwa Aretha kiasi cha kumfanya Ed amshike begani na wakaelekea mahali kulikuwa na viti, huku Li akibaki amesimama pembeni

"Rian, Beruya kanipigia simu inaonesha yuko hatarini na yule mchumba wake" Aretha akamwambia, ghafla akawa kama aliyeshtuka "Rian anahitaji tumsaidie, tafadhali tufanye hivyo"

"Retha hebu niambie kwanza vizuri" Ed akamsihi

Akashusha pumzi na kumwambia "Beruya amesema yuko mahali asipojua ambapo mchumba wake yule daktari amempeleka na hataki kumwachia anahitaji msaada wangu"

Edrian akamwangalia Aretha ambaye sura yake ilijaa mfadhaiko kwa taarifa ile, "tutamsaidia Retha, tafadhali usiwe na mashaka"

Alipomaliza maneno yale uso wa Aretha ukajaa matumaini, akainuka kama anataka kuondoka, lakini Ed akamshika mkono na kumrudisha aketi..

"Rian.." lakini kabla ya kumaliza

"Retha tunasafiri tafadhali usiikatishe hii safari" Ed akamsihi

Aretha akanyamaza na kumuangalia Li aliyeketi hatua chache kutoka walipo akiwa na mabegi yao...

"Kwa hiyo tunamsaidiaje Rian?" Akauliza Aretha huku wasi wasi ukirudi tena usoni kwake..

"Naomba uniamini. Nipe simu yako." Ed akamwambia huku akinyoosha mkono kumuelekea

Aretha akampatia simu, Ed akampa ishara abaki kisha akainuka na kumuelekea Li ambaye naye aliinuka, kwa pamoja wakaenda pembeni kidogo..

"Najua nakupa kazi ambayo si yako, ila nakuomba nisaidie brother!" Ed akamwambia Li

Li akamuangalia kaka yake akishangaa kwa namna alikuwa anamsihi na hakuzoea kabisa!

"Bro natakiwa kufanya nini?" Li akauliza huku akishika bega la Ed

Edrian akampa taarifa kama alivyoambiwa na Aretha.

"Sasa wasiliana na Captain, namtumia maelekezo ya kufanya kutoka kwenye hiyo namba. Atawahusisha 4D, ninataka wewe usimamie kila kitu. Na uhakikishe usalama wa Beruya ikibidi mpeleke kwa mama" akamaliza Ed

"Sawa brother, naomba niwaache nikafuatilie mapema. Nitaripoti taarifa kwako mapema." Li akamwambia, kisha wote wawili wakaelekea alipo Aretha ambaye aliinamisha uso wake kwenye magoti

"Retha, Li anakuaga!" Ed akamwambia huku akimgusa mgongoni..

"Ahha kaka Li asante" Aretha akamshukuru japo alikuwa na mashaka mengi usoni

Li akamwangalia Aretha halafu akageuka kumwambia kaka yake, "brother naomba dakika chache niongee naye"

Ed akashtuka lakini akapiga hatua kwenda pembeni ambapo aliendelea kuwasiliana na Captain.

"Aretha, nakuhakikishia Beruya atapatikana ila nihakikishie hutaondoa furaha ya hii safari kwake. Amepanga vitu vya kufanya najua hajakushirikisha ila shauku yake ni kuu sana" Li akamwambia Aretha mara tu alipoketi

"Aahhm na....na.." Aretha akashikwa na kigugumizi lakini kabla ya kuweka hiyo sentensi vyema Li akaendelea

"Mimi nakuahidi kumpata rafiki yako Beruya lakini ona kama hii ni biashara ya mabadilishano, Nakuahidi unaniahidi" Li akamwambia Aretha ambaye aligeuka na kumtazama Ed aliyekuwa akiongea na simu wakati huo..

"Sawa kaka Li." Aretha akaitika na kurudi kuangalia chini..

"Asante sana na ninaomba usimwambie bro" Li akainuka na kumpa mkono Aretha kisha akamwambia..

"Safari njema na ikumbuke ahadi yako"

"Sawa. Asante sana"

Edrian akawasogelea na kumgusa begani Li ambaye aliondoka kwa haraka kuelekea alipoegesha gari huku akipiga simu yake.

"Retha kila kitu kitakuwa sawa, tafadhali usiwe ma wasiwasi." Edrian akamgusa begani Aretha ambaye sasa aligeuka na kumtazama usoni, kisha akakubali huku akitikisa kichwa

"Namuamini sana Li kuwa atahakikisha Beruya atapatikana na atatujulisha mapema kila hatua inavyoenda"

"Rian, nimekuelewa. Naomba uniambie safari hii ni ya wapi?" Aretha akamuuliza huku akimtazama usoni

Edrian akatabasamu baada ya kuona uso wa Aretha ukirudi katika uchangamfu kama ulivyokuwa awali!

Akaingiza mkono kwenye moja ya mifuko iliyokuwa kwenye koti alilovaa akatoka na hati mbili za kusafiria. Akachukua moja na kumkabidhi Aretha

"Angalia mwenyewe"

Aretha akaichukua hati ile akamuangalia Ed..