Aretha akashusha miguu yake akainuka na kumsogelea Edrian aliyekuwa ameketi, akakaa mapajani mwake na kumwangalia usoni...
"Una haki ya kujisikia hivyo, sababu niko hapa kwenye moyo wako!!" Aretha akanyoosha mkono akigusa sehemu moyo wake!
Edrian akaukamata mkono wake akauweka vyema kifuani kwake kisha akamwangalia na kumwambia
"Kama unajua hivyo usifanye mambo yanaufanya udunde hata ukaribie kutoka"
Akacheka Aretha na kumwambia "Nakuahidi sitafanya hivyo tena" Edrian akambusu Aretha mdomoni busu jepesi,
"Utalala na mimi?" Akamtania
Aretha akainuka kwa haraka huku akitikisa kichwa kukataa
"Hahahaha unataka kwenda wapi, unaniacha mimi peke yangu!" Edrian akajifanya kusikitika
"Rian, nimeshamwambia Coletha nitalala kwake" Aretha akajibu
"Na mimi sitaki kulala peke yangu. Nataka nibembelezwe hadi nilale"
"Nikikusubiri ulale nani atanionesha chumbani kwa Coletha maana sipajui" Aretha akajitetea
"Basi ngoja nimpigie nimwambie utalala kwa__"
"No no no no...nakuomba Rian usifanye hivyo" Aretha akashusha pumzi kwa nguvu asijue cha kufanya!
Edrian akainuka na kumsogelea akamkumbatia huku akitabasamu "usingekubaliana na wifi yako kabla ya mumeo"
"Mhhhhh" akaguna Aretha
"Tufanye hivi, keti hapo kwenye kochi naenda kuangalia huyo wifi yako kama amekuandalia vyema halafu nakuruhusu ukalale huko. Sawa?" Edrian akamwambia huku akimpeleka kwenye kochi, akamketisha..
Aretha akamwangalia Ed akitoka mle chumbani!
***********
Coletha baada ya kuona Aretha bado hajatoka chumbani kwa kaka yake akamwambia Zena...
"Zena mie naenda chumbani, usiku umeenda, kama waendelea na huo mchezo kwenye runinga utachelewa kuamka kesho usisahau kaka yuko nyumbani na ana mgeni"
"Kaka Li na D hawarudi eeeh?" Akauliza Zena
"Nilikwambia toka unapika watakula kwa mama, na huenda wakalala huko kama unavyomjua mama!! Coletha akamjibu huku akipanda ngazi kisha akaendelea
"Kalale mapema, utaamshwa wakati hutaki"
"Namalizia hapa, naenda kulala"
Alipofika chumbani, Coletha akaangalia nguo za kulalia alizomuandalia Aretha akatabasamu "sijui utakuja au kaka ameshanizidi kete"
Mlango wa chumbani kwake ukagongwa, akainuka na kwenda kufungua, "Big brother"
Ed akatabasamu kisha akapiga hatua kuingia huku Coletha akimpisha
"Mgeni umemuandalia chumbani kwako, wakati nilikwambia mwandalie chumba chake eeh?" Ed akauliza huku akiangalia nguo ambazo Coletha aliziandaa
"Bro amechagua kulala na mimi.. au unaona wivu?" Coletha akamuuliza akimuangalia usoni
"Wivu kabisaa nauhisi. Basi mdogo wangu nimebadilisha mawazo" Ed akatabasamu alipoona nguo ambazo Coletha akimwangalia Aretha, akazichukua
"Hahaha bro, imekula kwako." Akacheka Coletha
"Basi sawa. Hizi nguo Nitaandika nazo ataoga kwangu atalala kwako!!" Ed akamwambia mdogo wake huku akitabasamu kwa utani ule
"H ahhaha mmmh Sawa." Coletha akakubali huku akijua kaka yake aliwaza nini
Ed akachukua zile nguo akainuka na kuanza kupiga hatua kutoka kisha akakumbuka
"Usimwambie mama sawa,baby sisy" huku akicheka Coletha naye akamjibu
"Sitamwambia kama atalala kwako, ila akilala kwangu namwambia"
Edrian akafungua mlango na kutoka mle ndani huku akicheka sentensi ya mwisho ya Coletha..
"If only she sleeps in my room!"
Akaingia chumbani kwake na kumkuta Aretha amelala kwenye kochi huku macho yake yakionesha wazi kuchoka
"Pole Retha..amka ukaoge, ubadilishe ukalale, kesho tuna mahali pa kwenda halafu tuna manunuzi ya kufanya"
Aretha akainuka kwa uchovu akachukua nguo na kuelekea bafuni. Edrian akauliza kwa utani
"Nije nikusaidie kuoga?"
"Hapana Rian" Aretha akatikisa kichwa kukataa akafunga mlango na kumuacha Ed akicheka.
"She is amazing!"
***********
Aretha alipoingia kwenye bafu la Edrian ghafla usingizi wote aliouhisi ukatoweka, macho yake yakavutia na kile alichokiona.
"Mungu wangu hili bafu au nini hiki" akasema mwenyewe huku akipiga hatua kuweka nguo alizoshika mkononi kwenye eneo la kuning'iniza nguo. Akaangalia sehemu ya kwanza ilikuwa na mlango wa kuvuta wa kioo, akachungulia akaona sinki la choo cha kukaa, pazia la plastic likionesha upande wa pili ni bafu.