"Ulikutana na Simunge kisiri siri nisijue, unajaribu kunificha Renatha au unasahau jicho langu li mahali pote" Sauti ya TM ilikuwa imeshiba hasira
"Baba" Renatha ambaye alisimama hatua chache kutoka kwenye kochi alilokalia TM
"Nilikwambia katika kazi usijaribu kunirubuni na 'baba' thing, am not buying it!" TM akamwambia huku akichukua sigara kwenye droo iliyopo kwenye meza ndogo
Renatha akameza mate kisha akakunja ngumi "Bosi nilionana na Simunge ikiwa ni hatua ya kumshawishi kuniamini. Siwezi kuwa na ukaribu wa haraka sababu Simunge sio mtu mwepesi"
"Kwa hiyo akikuamini utamwambia wewe ni nani na unafanya hayo sababu unajaribu kumpata mama yako au sio?" Mtetemo wa ghadhabu ulikuwa kwenye sauti ya TM
Renatha akavuta pumzi ndefu kwa uchungu huku aking'ata meno "Bon"
"Ba.. ahm..Bosi, maneno yangu ni mtego nilioutega, ikiwa nataka Edrian aniamini lazima nimuoneshe kuwa nina siri ninayoficha kama yeye alivyo na siri. Sina sababu ya kusema nae ukweli wowote"
"Mhhhh Renatha, usifikiri unaweza kuwa na akili nyingi kupita za yeye alikuleta duniani!" TM akageuka na kumtazama huku moshi wa sigara ukifunika uso wake kisha akaendelea
"Nafikiri sasa muda wako unahesabika, wiki mbili zinatosha. Tafuta hiyo ramani. Don't try doublecrossing!"
Renatha akainama, "Asante TM" akashukuru.. lakini kabla ya kugeuka
"Baada ya hii kazi nitakuonesha mama yako alipo." TM akamwambia Renatha
"Asante bosi"
"Baba" TM akamrekebisha kisha akarudisha macho yake kwenye TV iliyokuwa pale sebuleni.
Renatha akapiga hatua kwa haraka akatoka mle ndani. Akiwa na fundo la uchungu alitembea kama simba aliyekosa mawindo anapojaribu kukamata chochote. Mwisho wa hatua zake zilimfikisha kwenye gereji iliyokuwa upande wa kushoto wa jumba hili la kifahari la TM. Kule gereji alielekea hadi kwenye gari moja iliyokuwa imefunguliwa 'bonet' kuonesha ilikuwa kwenye matengenezo, akasimama pembeni kisha akaita
"Bon"
Sauti ya tairi ikiburuza ilimdhihirishia Renatha kuwa Bon alikuwepo!
"Unataka nini Renee?" Bon akatokea chini ya gari akiwa amelala kwenye kitoroli. Hakuwa ndani ya mavazi aliyoonekana akiwa ameyavaa jioni ya leo bali alivaa suruali aina ya jeans na juu hakuwa amevaa shati akionesha alikuwa kwenye matengenezo ya gari!
"Ulikuwa na sababu yoyote ya kuingilia mazungumzo yangu?" Renatha akamuuliza huku akiweka mikono kiunoni
Bon akakunja mikono yake akakiegemeza kichwa chake huku akimwangalia na tabasamu la dhihaka likiwa wazi mdomoni mwake!
"Tangu lini unanikaripia ninapofanya kazi yangu?"
Renatha akashusha pumzi kisha akaendelea "unadhani sina haki ya kuwa na maisha yangu binafsi au nimeyauza maisha yangu kwako?"
"Hahahhaa hilo halinihusu, nadhani ni vizuri ukaongea hilo na bosi" Bon akamwambia huku akiendelea kulala kwenye kitoroli kile.
"Sikia ipo siku utajilaumu sana kufanya kazi unayofanya hata kama ndio inakupa maisha haya" Renatha akamwambia kwa hasira
Bon akamwangalia kama mtu aliyetafakari aliyosikia halafu akaachia kicheko "hahhaa nilijilaumu wakati ule sikujua maisha haya kuna mtu anafurahia wakati wewe unaumia. Hivyo hunitetemeshi kwa hilo. Anyway yule kijana mwingine anaweza kuwa mtu mzuri kwako" akainuka na kuketi
Renatha akamwangalia kisha akasonya na kuondoka
"He is a good boy Renee!!" Bon akamwambia huku akicheka na mara Renatha alipokuwa mbali na macho yake sura yake ikabadilika.
"Get that map Renee I want to live my life too"
Akavuta taulo iliyokuwa ukutani, akajifuta na kisha akachukua na kuelekea kwenye bafu iliyo ndani ya gereji ile
*******
"Haukuwa na sababu ya kwenda mwenyewe Retha, walau ungeweza kwenda na Frans. Usiamini mtu kirahisi. Vipi kama angekwambia kazi anayotaka iko chumbani" Edrian akamwambia Aretha ambaye aliketi huku miguu yake ikiweka mapajani kwake.. Walipomaliza kula wakiwa wameketi kwenye kochi, Aretha alimuomba msamaha Edrian na kujieleza kwa nini alifika pale peke yake!
Akatabasamu, "Rian unahisi hofu au unapata wivu" akauliza kwa sauti tulivu kabisa kiasi cha kumfanya Ed aangalie pembeni
"Napata vyote Retha"
Aretha akashusha miguu yake akainuka na kumsogelea Edrian