Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 199 - NAKUPENDA ZAIDI

Chapter 199 - NAKUPENDA ZAIDI

"Ninachokuomba princess usiruhusu chochote kiingilie hii safari." Kulikuwa na msisitizo mkubwa kwenye sauti ya Edrian kiasi cha kumfanya Aretha kusita kuendelea akamwangalia huku akitamani kumwambia BM alihusika lakini hakuweza.

"Ni hivyo tu ulitaka kuniambia Retha" Edrian akauliza huku akigeuka na kumtazama... akagundua wasi wasi uliokuwa usoni kwa Aretha

"Aaaamh hapana. Natamani kutumia fursa hii. Umeona fomu nilizojaza?" Aretha akajaribu kubadili mazungumzo baada ya kushindwa kumtaja BM

"Nimekwisha zituma na nitachukua kesho jioni." Akajibu Ed kisha akamuuliza huku akiinuka kuelekea kwenye meza aliyotumia kuchora

" Kwa hiyo huu mti uliouchora umebeba stori gani mpenzi?" Edrian akautazama mchoro ule kisha akamwangalia

"Angalia vizuri Rian" Akatabasamu Aretha

Edrian akarudisha macho kwenye picha akifuatilia mchirizi wa brashi, alichokiona kilimshangaza

"Retha ume___aaah, huyu ni mimi na wewe hapa ni wapi?"

Aretha akacheka alipoona picha imemteka Ed, akainuka na kusogea kisha akamuelekeza

"Huyu ni mimi na wewe, hapa ni bondeni tulipoketi siku ile tulitoka. Huu mti ni mahali ambapo nilikuona kwa mara ya kwanza. Picha mbili zipo ndani ya huu mti." Akamaliza kumwelekea

Edrian alikaza macho kwenye picha huku akishangaa uwezo wa Aretha kuziona picha mbili kwa urahisi wakati kwake ilichukua dakika kufuatilia mistari ya brashi.

:Oooooh nimeelewa....."Edrian akamgeukia Aretha

"Hii ni yangu eeeh" akauliza

"Ndio, ni asante yangu hahahha" akacheka Aretha kabla kicheko hakijaisha Edrian akamnyanyua juu huku miguu ya Aretha ikibaki inaning'inia. Sasa Aretha akimwangalia Edrian kutokea juu....

"Rian niweke chini hehehe" Aretha akamwambia huku akicheka

Edrian akatikisa kichwa akikataa, "Nataka unitazame wakati nakwambia haya maneno"

"Mhh" Aretha akaguna huku akiinua nyusi zake

"Nakupenda, halafu nakupenda zaidi." Edrian akamwambia kisha akaweka mdomo kutarajia busu lakini Aretha akamkumbatia

"Nakupenda pia Rian"

Giza lilianza kuchukua nafasi ya mwangaza hafifu uliobaki baada ya machweo ya jua. Wakiwa wamekaa mahali pale mwangaza wa taa uliwamulika Edrian aliketi kwenye kiti huku Aretha akiwa ameketi juu ya mapaja yake na kichwa chake akiwa amekilaza kifuani kwake.

"Retha, ninajua mama atakapoongea lazima tutasafiri. Nina shauku na hii safari kiasi kwamba natamani hata iwe kesho" Edrian akamwambia huku akichezea vidole vya Aretha.

"Mhhh tunaenda wapi kwani?" Aretha akauliza

"Hilo utajua mara nitakapokukabidhi tiketi yako princess" Edrian akaweka na tabasamu usoni akitafakari mambo atakayomshangaza nayo

"Rian, ulimwambia nini 'Dean' hadi akakubali nipumzike mwezi mzima?" Akauliza swali ambalo lilikuwa likimsumbua maana alijua isingekuwa rahisi. Alibakiza miezi michache kumaliza ruhusa kama hizo hazikukubalika.

"Hahaha unataka nikutobolee siri, hapana, labda unishawishi" Edrian akakataa

Aretha akataka kuinuka lakini Ed a kumrudisha, akamwangalia

"Nitakushawishi .....aaaaah" kabla hajamaliza Ed akamtekenya na Aretha akashtuka huku akicheka

"Nishawishi Retha" Ed akamtania tena

Aretha alipojaribu kuinuka Ed akamtekenya halafu akamrudisha mapajani kwake huku akishtuka na kucheka

"Rian please I...." kabla ya kumaliza Ed akamtekenya tena

Aretha alipoona amezidiwa akakubali atamshawishi. Edrian akamwacha kidogo huku akimwangalia alivyokuwa akihema. Aretha akataka kuinuka

"Hakuna kuinuka nishawishi hapa hapa" Edrian akamuwahi

"Rian....okay" Aretha akakubali kisha akavuta pumzi na kuishusha halafu kilichofuata kikamshangaza Edrian maana midomo ya Aretha ilimvamia ghafla tofauti na alivyotegemea busu la haraka kama ilivyo kawaida yake. Leo Aretha aliweka rekodi ambayo Edrian alitamani iendelea. Sasa yeye ndie alihitaji hewa maana Aretha alishavuta yake kabla ya kumshtua.

Mapigo ya moyo ya Edrian yalienda kasi lakini Aretha akaachia kisha akainuka ghafla asiweze kumwangalia usoni Rian akaenda kuchukua maji akanywa. Akachukua mengine na kumpa Ed ambaye sasa alisimama akiangalia mbele..

"Am sorry" Aretha akamwambia mara alipompatia maji.

Edrian akatabasamu kisha akafungua maji na kunywa