Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 196 - UNGEWEZANA NAYE

Chapter 196 - UNGEWEZANA NAYE

"Rian, umeandaa kabisa?" Aretha akauliza baada ya kuona mazingira safi yaliyoandaliwa.

Edrian akatabasamu na kisha akamshika mkono kumuelekeza kwenye meza iliyozungukwa na viti viwili, akamketisha kisha akafungua jokofu dogo lililokuwa pembeni akatoa boksi lenye juisi akamimina kwenye glasi iliyokuwa mezani akamsogezea Aretha.

"Rian unatak__" Edrian akainama na kumbusu mdomoni kisha akamuinua kidevu hata wakaangaliana machoni

"Retha, pumzika hapa, hiyo meza nyingine unaweza kuitumia kwa kazi yako. Wakati mwingine nitakuboreshea mazingira ya kazi yako." Akashusha busu jingine jepesi kwenye paji la uso akageuka na kuchukua tufaa moja akang'ata na kuondoka.

Aretha akabaki katika mshangao, kisha akainua kidole chake akagusa pale alipombusu Edrian na kufumba macho,

"I love you Rian" akasema kwa sauti ya chini

"I love you too" sauti ya Ed ikamshtua Aretha hata kidogo amwage juisi iliyokuwa mezani ambayo aliiwahi..

"Rian umenishtua" akasema Aretha huku akiweka mkono kwenye kifua chake

Edrian akasogea hadi alipoketi akaweka mkono wake juu ya ule uliokuwa kifuani kwa Aretha

"Am sorry princess" akamuomba msamaha..

Nilisahau simu yangu, akanyoosha mkono kuchukua simu iliyokuwa juu ya meza.

"Aaahhhh umenishtua ningeanguka ujue" Aretha akalalamika

"Sitakushtua tena" Edrian akamwambia na kupiga hatua akimuacha Aretha papa yake

"Rian" Aretha akaita huku akiinuka kumfuata

Edrian akasimama na kugeuka nyuma wakiwa hatua chache kukutana, Aretha akamshukuru,

"Asante kwa haya yote"

"Asante pia kwa kuja" Edrian akamjibu

Aretha akasogea akainamisha kichwa chini kabla ya kuinuka na kumkumbatia Ed ambaye alipitisha mikono kwenye kiuno chake na kumkumbatia pia.

"Umenipendelea sana Rian" Aretha akasema, sauti yake ikisikika kutoka kifuani kwa Edrian.

"Nimefaulu kukuteka hisia zako. Natakiwa kupata pongezi au sio?" Akauliza kwa sauti ya kunong'ona kwenye sikio la Aretha na kusafirisha mawimbi yaliyoleta msisimko katika mwili wa Aretha

"Mmh" Aretha akaguna asijue nini Edrian alimaanisha

Akamsogeza nyuma kidogo na wakabaki wakiangaliana, "Haudhani kuwa nahitaji kupewa pongezi na mpenzi wangu kwa kum_"

Kabla ya kumaliza maneno yale, Aretha alimbusu kwenye midomo yake mara moja kabla ya kujichomoa kwenye mikono ya Ed na kurudi kwenye kiti alichoketi mara ya kwanza..

"Hahahhaa hilo halijaisha princess na hata sio zawadi ya mtu aliyekufurahisha, nitahakikisha unalilipa hivi karibuni" akageuka na kumwambia

"Naenda, ukinihitaji niko ofisini mpenzi" akamwambia Aretha ambaye muda huu alishika simu yake akiangalia..

"Asante" Aretha akamjibu Edrian na kumuacha aelekee ofisini hakutaka kuwa sababu ya kumtoa katika majukumu yake.

Edrian akaelekea panapo lifti, akashuka ghorofa ya kumi na tatu. Lifti ulipofunguka akapiga hatua kuelekea ofisini kwake ambapo alikutana na Bwana Ganeteu ambaye ni mwanasheria wa SGC.

Baada ya kusalimiana naye akaelekea ofisini huku akijua lazima kuna jambo la muhimu lililomfanya mwanasheria huyu kuingia ofisini kwake mida hiyo.

"Kaka nimefanya kila nililoweza kuhakikisha lile ombi linakubaliwa. Hivyo Inspekta kwa shingo upande imebidi akubaliane na mkubwa wake. Hivyo mmeruhusiwa kuwa nje ya nchi japokuwa ndani ya hizi siku chache mtatakiwa kuwa tayari iwapo Sunday atawahitaji." Bwana Ganeteu akamwambia Edrian

"Asante kwa hilo rafiki yangu, angekataa bado nisingeweza kusimamisha safari" Edrian akamjibu huku tabasamu likiwa usoni

"Hahahha ungewezana naye nakujua?" Ganeteu akacheka kisha akaendelea

"Hilo sio hasa lililonileta"

"Nakujua, niambie" Edrian akaegama kwenye kiti

"Nina ushauri kidogo tu kuhusu kesi hii ambayo umeniomba niisimamie. Kwa kuwa hili suala la Aretha bado halijafunguliwa kesi nilikuwa nashauri mwenye kufungua kesi awe yule kijana." Bwana Ganeteu akameza mate kisha akaendelea kwa kuwa alimfahamu vyema Edrian kuwa si mtu wa kuongea kwa haraka, hapa alisubiri ampe sababu

"Kwa namna nilivyoongea na Sunday naonelea ikiwa Aretha atafungua kesi, utalazimika kuonekana mara nyingi kortini. Sio kitu salama sana hata kama utayaweka mahusiano yenu wazi."