Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 197 - NIFIKIRIE KWANZA

Chapter 197 - NIFIKIRIE KWANZA

Aretha alitulia akitazama mandhari safi iliyovutia kutoka kwenye baraza la juu la jengo hili la Ashanti. Akiwa mawazoni juu ya picha aliyokusudia kuipiga simu yake ikaita alipotazama haikuwa namba anayoifahamu, akasita kupokea huku akiiacha iite kwa muda hadi ikakata. Lakini simu iliita tena ķwa ile namba, na mara hii akaamua kupokea,

"Hellow" akaita

"Aretha, unaendeleaje?" Sauti ya mwanaume upande wa pili ilisikika

"Aaah naendelea vizuri, naongea na__" kabla ya kumalizia akakatishwa

"BM hapa, nimeona nikujulie hali" sauti ya BM ilikuwa ya utulivu kiasi cha kumfanya Aretha kupunguza wasi wasi

'Aah Asante niko salama" akajibu Aretha asijue nini aseme, kimya cha sekunde chache kikapita na alipotaka kuongea Aretha, wakajikuta wakianza kwa pamoja

"Endelea tu" BM akamsihi Aretha

"Ahhh, mm.. Asante kununua zile picha" Aretha akamwambia

"Oooh ninathamini juhudi zako naamini utafika mbali. Kulikuwa hakuna sababu ya kuanza kukukatisha tamaa." BM akamwambia..

"Nashukuru" Aretha akashukuru,

"Kuna kazi nafikiri unaweza kunisaidia kuifanya Jumamosi kama utaona vyema" BM akaleta wazo lake

"Mmmh kazi! Aa__"

BM akamuwahi Aretha "Kabla haujaikataa naomba unisikilize kwanza" akamsihi

Aretha akanyamaza kumpa nafasi aendelee

"Ninahitaji picha tatu muhimu sana ambazo nitazisafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mnada ambao kampuni yangu inausimamia. Na kwa namna niliziona picha zako nina uhakika tunahitaji talanta kama yako. Tutakulipa pesa yoyote utakayotaka" BM akapumua kidogo huku akisubiri mrejesho wa Aretha

"Lakini mimi sina ujuzi mkubwa kama Melissa na Beruya, kwa nini usiwasiliane na hao?"akauliza kwa mshangao

"Aretha kila mchoraji ana namna ya kuchora na kuwasilisha ujumbe wake, namna yako kwa sasa tunataka kuiingiza kwenye soko. Au wewe hauhitaji?"

" Ahhh hapana. Samahani lakini naomba nifikirie kwanza nitakujulisha" Aretha akajitetea

"Sawa, naomba nikupe masaa mawili utanijulisha"

"Haya. Asante" Aretha akashukuru na wakati huo BM alikata simu.

Mara alipokata simu akatafakari kuhusu nafasi hiyo ambayo aliona ni fursa njema kwake. Pamoja na akili yake kukubaliana na fursa hii bado ndani ya dhamiri yake alihisi kutahadharishwa. Alipowaza kumshirikisha Edrian hofu ikamjaa akikumbuka namna ambavyo walitofautiana wakati wa onesho.

"Hawezi kukubali" akawaza

Meseji ikaingia kwenye simu yake,

"Princess, Loy anakuja huko, naomba uingize taarifa zako kwenye hiyo kompyuta. Ni muhimu. Usisahau kula matunda" Nakupenda."

Akatabasamu kisha mkono wake ukachukua ndizi akamenya na kuanza kula huku akimsubiri Loy.

**************

Edrian alihakikisha anafanya kazi zake kwa haraka baada ya kutuma fomu za maombi ya hati ya kusafiria kwa ajili ya Aretha. Alipohakikisha hana kazi nyingine tena, akasimama na kujinyoosha kisha akaweka vitu vyake sawa juu ya meza. Akaelekea maliwatoni.

Alipotoka akachukua mfuko ambao aliuagiza masaa matatu nyuma pamoja na simu yake akatoka. Loy naye alikuwa akiweka vitu vyake sawa ili kuondoka,

"Allan amesharudi?" Akauliza huku akitaka kuelekea ofisini kwake lakini Loy akamjulisha kuwa ametoka nje kiofisi.

"Okay. Jioni njema Loy" akamuaga.

"Nashukuru bosi"

Edrian akaelekea ilipo lifti na kuingia, akaelekea juu alipo Aretha. Mara mlango ulipofunguka Edrian akauangalia tena ule mfuko na kutabasamu halafu akapiga hatua nje ya lifti. Akapanda ngazi na alipokaribia kumaliza ngazi akasikia sauti ya Aretha akiongea na simu. Ghafla akahisi wivu akaamua kusimama pale ili asikie aliongea na nani..

"Sawa nitajitahidi muda huo niwepo" sauti ya Aretha ikasikika

"Haya, Asante kwa kunishirikisha fursa hii" aliendelea Aretha kisha wakaagana na baadae akashusha pumzi kwa nguvu.

Edrian akaelekea alipo Aretha, "huu utulivu nikajua umelala kabisa" akamwambia huku akitabasamu

Aretha akashtuka baada ya kumuona, akatamani amuulize kama alisikia maongezi yote aliyokuwa aliongea

"Aaah umenishtua" akamwambia huku akiinuka

"Hahaha kwani ulikuwa unaniwaza?" Akacheka

"Hapana aa namaanisha ndio lakini umetokezea tofauti na matarajio yangu.. umemaliza kazi?"Aretha akamuuliza mara alipomkaribia