Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 192 - UNA HISIA NA RENATHA?

Chapter 192 - UNA HISIA NA RENATHA?

"Eeeh" Allan akashtuka, wiki mbili bro ni kama mwezi kabisa"

"Hahahaha wala usihofu mtakuwa na komrade mwenzio hakuna kitakachoharibika nina uhakika" Edrian akamhakikishia

Allan akaangalia chini, Edrian akamshtukia kisha akamuuliza, "Allan kuna tatizo"

Akainua macho akamtazama usoni, "Kaka najua utanikemea mara nitakaposema hili nililonalo moyoni"

"Kama nitakukemea, basi ni kwa wema. Au sio?" Edrian akamuuliza huku akiinua nyusi zake juu

Allan akafumba macho taratibu kisha akafumbua, "Bro nina ombi ambalo kama utanisaidia basi nakuhakikishia sitarudia kabisa kuingilia maisha yako."

Edrian akashangaa kusikia Allan kuingilia maisha yake, "Kwa namna gani Allan?"

Allan akashusha pumzi na kuamua kumsimulia makubaliano yake na Renatha na nini kilitokea.

Edrian akamwangalia Allan kisha akakuna kidevu chake na kuinuka kwenye kiti akaenda hadi kwenye usawa wa dirisha akasimama kwa muda akiangalia mandhari ya nje

Ukimya huu wa Ed ulimuweka mahali pagumu Allan, ndani akajilaani kwa nini aliamua kucheza kamari maisha ya mtu ambaye alimchukua yeye na familia yake kuwa ni watu wake.

"Kwa nini uliamua kumuacha akushinde wakati hata mimi sifui dafu kwenye mchezo na wewe?" Sauti ya Edrian ikamtoa Allan kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo.

"Nilifanya hivyo ili kujua nini alikuwa anakificha bro. Kama ningeshinda nisingejua" akajitetea

Edrian akageuka na kumtazama Allan, akajinyoosha, "Ulimuuliza kwa nini anataka kula chakula cha jioni nami?"

"Nilijaribu kumdodosa lakini hakunipa jibu lakufaa. Ila naamini hana nia mbaya" Allan akamjibu Edrian ambaye alijinyoosha na kisha akapiga hatua kurudi kwenye kiti chake

"Allan, unajua kanuni, maisha yangu ni yangu na sikuwahi kufurahia mtu ayaingilie hata kidogo." Kulikuwa na dalili za hasira kwenye sauti ya Edrian iliyomfanya Allan ajiweke sawa kwenye kiti

"Bro ukikataa nitaelewa, japo nia yangu nikujua kile kimejificha kwenye nia ya Renee"

Edrian akamuangalia Allan kisha akamuuliza swali ambalo hata yeye alijishangaa lilimtokaje, "UNAMPENDA?"

"Eeeeeh?" Allan alishtuka aliposikia hilo swali

"Aamh...ninamaanisha una hisia zozote juu ya Renatha?" Edrian akamwambia kwa sauti ya chini

"Ammhh.. hapana, ninahisi tu kuna kitu anakitaka kwako ambacho kinampa msukumo mkubwa kila anapokuona" Allan alipomaliza kuongea ni kama alishtuka

"Aa...Bro...simaanishi namna ile au...aah_"

Kabla ya kumaliza Edrian akamkatisha

"Allan mara nyingine unajua sitakuacha ucheze na maisha yangu au ya mtu mwingine. Je kama angetaka mambo ya ofisi ambayo hayatakiwi kutoka nje?"

Allan akainama chini akilaumu shauku yake ya kutaka kuwa karibu na mtu ambaye tangu alipoanza kazi Edrian aliwaonya kutomuamini.

"I am sorry bro. My curiosity got better of me"

"Hiyo Jumamosi nina mahali ambapo nataka kwenda, nitapita nikitoka. Na kama una hisia zozote juu yake kuwa mwangalifu"

"Eeh" Allan akashtuka aliposikia Ed amekubali

"Unafikiri ataniambia anachotaka!!! Allan, mimi na wewe tunajua karibia michezo yote katika biashara hii. Jambo moja ninalohitaji ni wewe uwepo pamoja nami" Edrian akamwambia huku akianza kubofya vitufe vya kompyuta yake.

"Asante bro, nitafanya hivyo. Nakuahidi ni nitajua nia yake halisi."

"Sawa" Edrian akaendelea na kazi zake huku akitafakari maamuzi ya Allan, akatabasamu kabla ya simu yake ya mkononi kumtoa kwenye kioo cha kompyuta. Alipoangalia ilikuwa ni simu kutoka kwa Captain

Akapokea, "Captain"

"Najua huwezi kuamini aliyehusika na kuharibu zile picha pale ukumbini lakini ninakutumia picha angalia taratibu utaelewa" sauti ya Captain ilimfanya Edrian atabasamu

"Aaaah, it's well."

Simu ikakatwa upande wa pili, Edrian akaangalia kompyuta yake na mara sauti ya ya ujumbe ulioingia ikasikika. Akaelekea kwenye barua pepe akaona kichwa cha habari, "Suprise"

Akafungua kisha akaona faili lilionesha picha za video, akalipakua na mara lilipomaliza akalifungua.

Akaangalia mwanzo mpaka mwisho huku kukiwa na mikunjo kadhaa usoni kwa Ed kabla ya mwisho kutabasamu kidogo. Kisha akachukua simu yake na akampigia Dokta Ivan

"Hellow Ivan" akaongea huku akizungusha kalamu mkononi mwake