Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 182 - UNAMUAMINI SANA

Chapter 182 - UNAMUAMINI SANA

"Unaendeleaje kwa sasa?" Akauliza huku akiketi kwenye kiti wakati yule mwingine akibaki amesimama pembeni

"Naendelea vizuri. Asante" Aretha akajibu akimuangalia Edrian ambaye alimpa tabasamu ya kumhakikishia kuwa yuko salama na hakuwa na sababu ya kuhofu.

"Mr Simunge unaweza kutupa nafasi tuongee na Ar_" kabla Inspekta hajamaliza Aretha akamkatisha

"H..hapana naomba asiondoke"Aretha akasema huku akimwangalia usoni Edrian

"Oooh basi sawa. Nitaanza kuchukua maelezo yako na kisha Mr Simunge utafuata"

Akatoa kijidaftari kidogo na kalamu iliyokuwa imebana pembeni, akainua uso wake na kumwangalia kwa umakini Aretha,

"Aretha, niiite Inspekta Sunday, nitachukua maelezo yako juu ya tukio la utekaji lililotokea mchana leo chuoni. Unaweza kuniambia nini kilitokea mara ulipofika chuo"

Aretha akamuelezea kama alivyomuelezea Edrian hadi ambapo mtu alimfunika na kitambaa puani.

"Kwa hiyo sababu ya Bruno kukushambulia kwa maneno ni ipi?" Inspekta akamuuliza

Aretha akamwangalia Edrian, akampa ishara aendelee

"Alinishutumu kuwa mimi ni...nimeiba mwanamume wa mtu" Aretha akazungumza kwa sauti ya chini

Inspekta akatabasamu kisha akamuuliza "ni kweli Aretha?"

"Inspekta una_" Edrian akapiga hatua akitaka kusema kitu lakini Inspekta akanyoosha mkono kumzuia kisha akamwambia

"Mr Simunge najaribu kupata maelezo na kama kuna tatizo kwenye hilo nitakuomba usubiri nje" akatabasamu na kumgeukia Aretha

"Ni kweli Aretha kwamba ulimchuku_"

"Hapana!!" Aretha akapaza sauti akikataa, akamuangalia Edrian na kisha akashusha pumzi kwa nguvu

"Sio kweli Inspekta, kile ambacho kilimuudhi Charlz hata akamshambulia Bruno ni kwa sababu aliniita kiberenge. Na kama ningekuwa nimemuibia mtu angenifuata mwenyewe kwa ujasiri." Sauti ya Aretha ikadhihirisha hasira ndani yake.

"Sawa, Aretha. Sasa unadhani ni nani anaweza kuhusika na tukio hili?"

Akamwangalia tena Edrian lakini mara hii jicho lake lilikuwa kali kiasi kwamba Inspekta akahamisha macho yake kufuata kule yalikoelekea yale ya Aretha kisha akarudisha

"Kuna kitu nakikosa hapa au?" Akauliza Inspekta

Aretha akamwangalia tena Edrian kisha akarudi kwake Inspekta na kusema

"Sijui nani anahusika?" Akajibu Aretha

"Hakuna yeyote unayemhisi Aretha?" akauliza Inspekta Sunday

"Hapana" Aretha akamjibu, naye Inspekta akatabasamu na kumwambia

"Sina swali zaidi nashukuru. Naomba nipate maelezo yako Mr Simunge kama hutojali"

Edrian akampa ishara ya kukubali akasogea hadi alipoketi Aretha, akaketi pembeni yake..

"Uko sawa kutoa maelezo yako ukiwa na Aretha?" Akauliza Inspekta, Edrian akakubali

Inspekta akamsikiliza Edrian akisimulia namna alivyofika hata kuwaokoa Aretha na Charlz. Alipomaliza kutoa maelezo Inspekta akamuuliza

"Unamaanisha uliwakuta wamelala kitandani wakiwa na nguo zao?" Akauliza Inspekta akimwangalia Edrian ambaye wala hakupepesa macho yake

"Ndio niliwakuta wakiwa wamelazwa kwenye kitanda na nguo walizovaa" mwili wa Edrian kwa ghafla ukakamaa huku viganja vya mkono wake vikikunjwa ngumi na kusababisha mishipa ya mkono kuonekana

Inspekta akatabasamu na kumwangalia Aretha kisha Edrian

"Mr Simunge, Aretha ni nani kwako hata ukaamua kufuatilia mawasiliano yake?"

Edrian akamjibu "Aretha ni mpenzi wangu na ni mke wangu matarajiwa."

Aretha akainama chini kwa aibu huku akitabasamu taratibu..

"Unadhani alikuwa hajitambui wakati yuko na Charlz?" Akamuuliza kwa uchokozi

Aretha akamwangalia Ed kwa jicho la upole huzuni ikiwa wazi usoni kwake

"Hapana, nina uhakika wa asilimia zote hakuwa anajitambua" Edrian akajibu huku akimtazama Inspekta kwa jicho kali

"Una uhakika kwa sababu unamuamini sana Aretha. Najua hata ulipomuona bila nguo bad_" kabla Inspekta hajaendelea sauti kali yenye mtetemo wa radi ilisikika kutoka kwa Edrian ambaye alisimama kitendo kilichomfanya Inspekta nae asimame wakabaki wakiangaliana usoni.

"Inspekta"

"Kuna kitu nimesema ambacho kimekufanya usimame kwa jazba Mr Simunge?" Akauliza Inspekta Sunday akiachia tabasamu lake upande mmoja wa mdomo wake

Edrian akamwangalia Inspekta kwa hasira , "Unataka kupata nini katika unachojaribu kuuliza?"