Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 183 - SIO MARAFIKI

Chapter 183 - SIO MARAFIKI

Edrian akamwangalia Inspekta kwa hasira , "Unataka kupata nini katika hicho unachojaribu kuuliza?"

"Rian" Aretha akamshika mkono kumrudisha nyuma Ed ambaye alisimama akiangaliana na Inspekta. Yule askari aliyekuwa pembeni akapiga hatua kusogea lakini Inspekta Sunday akampa ishara arudi nyuma

Edrian akamwangalia Aretha kisha akaketi, Inspekta akaendelea kusimama huku akitabasamu

"Samahani Mr Simunge, naona unasahau taratibu za kazi yetu, ninachofanya ni sehemu ya kazi yangu. Hii ndio sababu niliuliza kama una uhuru wa kutoa maelezo ukiwa na Aretha"

"Inspekta nakuomba mara moja tu tuongee halafu utaendelea" Aretha akamwambia Inspekta kwa kumsihi

Inspekta akaitikia na kisha akampa ishara askari ambaye alisimama pembeni watoke nje.

Baada ya mlango kufungwa Aretha akaushika mkono wa Ed akamwambia

"Rian, kuna kitu hujaniambia unahitaji kuniambia?. Tafadhali toa ushirikiano kwa polisi ili tujue n_"

"Retha, ninachokisema ndivyo ilivyokuwa, sipendi maswali yasiyo na maana tu, Sunday sio mgeni kwangu ila huwa ana maswali yasiyopasa"

"Rian ulitukuta na nguo au la?" Aretha akauliza huku akimtazama usoni Ed ambaye alimtazama kisha akainua mkono wake na kumgusa shavuni Aretha

"Niliwakuta na nguo princess" Ed akamwambia kisha akashusha mkono wake huku akikunja ngumi, Aretha hakuona ngumi ile akashuka ili akamrudishe Inspekta ndani, lakini Ed akamshika mabega kumzuia alisimama

"Nitaenda Retha" akainuka na kuelekea mlangoni, akatoka na kumkuta Inspekta akiwa amekaa kwenye benchi pembeni ya mlango huku akiandika vitu kwenye kijidaftari chake.

"Mr Simunge, mimi na wewe tunajua maelezo yasiyopotosha ukweli husaidia kufikia ukweli" Inspekta Sunday akainuka mara Ed alipopiga hatua kumsogelea

Ed akasimama, wakatazama kwa muda, kwa namna ambayo usingeweza kujua ni kwa chuki au kwa amani.

"Sunday" Ed akamuita

"Inspekta Sunday my friend" Inspekta akamwambia huku akiachia tabasamu.

Edrian naye akaachia tabasamu akamshika mkono kuonesha kumkubali kuwa ni Inspekta

"Mimi na wewe sio maadui na wala sio marafiki. Ila nina ombi moja tu kwako, tafadhali urudishe ubinadamu wako ulioupoteza kambini. Fanya kazi yako kwa utu"

"Kwa sababu ni Aretha au?" Inspekta akamuuliza huku akiinua nyusi juu

"Ndio, kwa sababu ni Aretha lakini pia ni binadamu kama wengine ambao wanastahili ubinadamu wako" Edrian akaachia tabasamu

"Hahahaha unanifundisha kazi Simunge!!!, hebu tumalize maelezo au tunarudi ndani?" Inspekta akauliza huku akimpa ishara ya kurudi ndani

"Tunarudi ndani ila usinichokoze zaidi" Edrian akajibu na kufungua mlango kisha wakapiga hatua kuingia, lakini Inspekta akamwambia kwa sauti ya kunong'ona kumfanya Edrian ageuke nyuma na kutikisa kichwa

"Tutafutane uniambie ukweli ni mizani yangu imepungua au ni kweli umedakwa kwenye mapenzi?"

********

Mara alipotoka Edrian nje ili kumrudisha Inspekta, Aretha alibaki akitafakari iwapo kile alichokisikia kilikuwa ni ukweli au la.

"Au Rian ananificha ukweli!!!" Akajiuliza Aretha, akajikagua nguo zake hakuona tofauti yoyote

"Nitamuuliza nani sasa???. Kama alinikuta sina nguo oooh Mungu wangu naomba isiwe...isiwe kabisa." Akawaza Aretha huku mikono yake akiifunika usoni mwake. Akakusudia kumuuliza Derrick walau apate ukweli lakini napo pia akajikwaa

"Aaaargh nikimuuliza akanijibu ndio ina maana na yeye aliniona? Oooh haya mambo yananichosha"

"Kile Bruno alikisema mbona kama kuna mtu aliambiwa na mtu?" Akawaza Aretha

"Nina uhakika vita hivi ni matokeo ya Joselyn bila shaka. Au nimwambie Inspekta, aaaah naweza sema ni Lyn kumbe sio, lakini yeye ndio sababu ya matatizo mengi" swali moja kwenda jingine liliendelea kichwani kwa Aretha hadi mlango ulipofunguliwa wakaingia Edrian na Inspekta.

Ed akaelekea pembeni ya Aretha akaketi, "Tunaweza kuendelea inspekta" akamwambia

Inspekta akatabasamu na kumwangalia Edrian

"Kwa maelezo yako Mr Simunge unahisi ni nani anaweza kuwa amehusika na tukio hili?"

Edrian akamwangalia Aretha kisha akarudisha macho kwa Inspekta

"Joselyn Martinez Kussah" Ed akamkazia macho Inspekta ambaye aliachia tabasamu lenye utani ndani yake